Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Mkasa: Wema ni akiba, usiache kutenda wema

Mkuu Dadii , kupotea njia ni wakati wa kwenda tu, huwezi kupotea njia wakati wa kurudi. Labda uamue kujipoteza.

Yeye afichaye dhambi zake hatafanikiwa, bali yeyote aziungamaye na kuziacha hupata rehema. Amebarikiwa mtu ambaye siku zote humcha BWANA, bali yeye afanyaye moyo wake kuwa mgumu huangukia kwenye taabu.
hakika
 
Nimetamani sana ungekuwa unasimulia nikiwa mbele yako nakusikiliza.
🤣🤣🤣🤣 usingeelewa hata, bora umesoma. Ukikaa na mimi nina tabia za Charles Champlin kama unamjua.
Umeniinspire kwa mengi mazuri lakini pia nimepata elimu sehemu ambazo hazikuwa sawa na namna ya kuziepuk
Nashukuru kwa appreciation yako, ndilo lengo langu kuleta huu mkasa hapa. 🙏
Mkuu MUNGU akubariki mno na heshima nyingi sana ziende upande wako
emoji120.png
Amina. Na kwako pia
Ningepata dhambi kubwa sana kama ningepita bila kutoa comment.
Feedback zinasaidia na wengi kujifunza.
Aisee bonge moja la story, ina kila kitu ndani. Nimetumia ziku nzima kuisoma (nimecancel ratiba zangu zote).
Aise pole sana, mkasa ulivo mrefu umesoma siku moja?. Hongera, umenikumbusha kuna kipindi niliangalia legend of the seeker, nilianza saa 2 asubuhi mpaka kesho yake. Big up
 
Asante sana Benbulugu
Nimefurahi kusikia umefatilia, natumai umepata la kijifunza.

Kwa upande wangu, niliona mwanga mpya maishani mwangu, naishi huo ujumbe niliowapa.
Naomba kuuliza swali mheshimiwa je??changamoto nikubwa au ndogo kiasi gani kuzaa watoto kwa wamamatofauti tofauti??je maswala ya upendo kati yao nawatoto watumbo moja kuhisi wnaahaki kuzidi wengine???..ukipata nafasi nijibu hili tafadhali mkuu.
 
Mpendwa msomaji.

Kama ulisoma mkasa[emoji116]
(Nilivyo Okoa Maisha Ya Watalii toka Finland).

Huu ni mkasa kamili wa kisa kile. Nilielezea visa vichache kwa ufupi, lengo lilikuw kuonyesha msaada niliotoa kwa wafin.

Hapa utapata historia nzima ya maisha yangu na mwendelezo wa ule mkasa na wale watalii in details. Ni mkasa mrefu, ila nitajitahidi kumaliza kwa wakati.

Angalizo: Lengo ni kujifunza, kupitia mapito ya wenzetu, sina maana ya kutaka kuonyesha nilicho nacho, wala sina nia ya kujikweza. Imani yangu ni kupitia mkasa huu, kuna watu watapata jambo la kujifunza, kuna watakao burudika, nk.

******'
Tahadhari:

Picha zilizo tumika katika mkasa huu zimegawanyika katika makundi mawili:-

Kundi la 1:
Hazina uhusiano na mkasa huu, nimeziweka kama Mfano wa yale ninayoyaeleza yanavyofanana na picha husika.

(Mfano: Muonekano wa Rosemary , Zainabu na Zaituni n.k)

Kundi la 2:
Zina uhusiano na mkasa huu, ila sikuzipiga mimi, ziko mtandaoni. (Mfano: majina ya Airport, maduka, hotel n.k)

Majina yote ya watu yaliyotumika sio halisi, yamebuniwa kuleta radha, Wahusika wanayo majina yao halisi.

Maelezo mengine yote ni matukio na majina halisi ya maeneo husika.

Note 'disguised'
*********************

Utangulizi.

Katika maisha tunakutana na changamoto nyingi, mateso, kukatisha tamaa, umasikini, chuki, hasira, uongo, usariti, na mengine mengi.

Ndio maana kuna maandiko yanasema

"ulimwenguni kunayo dhiki nyingi"

Huu ni mkasa unaohusu familia moja ya mzee Anthony na mke wake Antonia. Baada ya changamoto, mateso na manyanyaso mengi, hatimae Anthony anafanikiwa kuandikishwa shule, jambo ambalo baba yake hakuwa ana litaka.

Anthony anapata msaada wa kulelewa na rafiki wa baba yake, malezi ambayo baba yake hakuona umuhimu wa kumpa.

Hatimae Anthony anafanikiwa kuanza maisha mapya, anapata watoto ambao anajitahita kuwapitisha njia salama na malezi bora.

Kijana mdogo anaonekana kipenzi cha wazazi, lakini anapata heka heka kipindi cha masomo yake, yaliyopelekea kuwa mbali na wazazi wake.

Mzee Anthony anawakabidhi vijana wake majukumu, je watayatimiza?

Mama anakataa kijana wake asiende kuishi ulaya, je atasikilizwa?

Fuatana nami katika mkasa huu kwani kuna mengi ya kujifunza, kuburusisha na kusikitisha.

Kiitos

***********

1939

Part One
Anthony
Anthony amezaliwa mwaka 1939 katika kijiji cha 'X', wilaya ya 'X' mkoa wa 'X'. Haiba yake ni mpole.

Ni mtoto yatima , mama yake alifariki Anthony akiwa na miaka mitatu tu. Aliugua malaria kutokana na umbali kutoka hapo kijijini ''X'' mpaka hospitali ya wilaya 'X', alipoteza maisha akiwa njiani.

Anthony amelelewa na baba yake kwa msaada wa bibi yake, bibi yake alifariki Anthony alipofikisha miaka 7. Akabaki na bana pekee.

Baba yake Anthony alioa mke mwingine, mke mdogo hakumpenda Anthony, alimtumikisha na kumtuhumu mambo ya uongo.

Siku moja mzee George alitembelewa na rafiki yake mzee John, mzee John alikuwa anaishi kijiji 'X' kiko jirani na kijiji 'X' anakoishi mzee George .

Mzee John alimkuta Anthony akifanya kazi ya kutwanga kisamvu, mama yake mdogo amekaa anakula karanga, Ilikuwa ni majira ya saa 10 jioni.

Kumbe toka asubuhi mtoto wa miaka 8 hakuwa amekula, mama yake wa kambo alipika chakula mchana akala peke yake kikaisha, mtoto aliporudi toka machungani ndio akapewa kazi ya kutwanga kisanvu, kisha kipikwe ndio ale.

Baba yake aliyajua yote hayo ila alipuuza kwa madai kuwa anamfundiasha maisha. Mzee George hakuwa amempeleka shule Anthony japo ana miaka 8.

Mzee John hakupendezwa na mazingira anayoishi Anthony, alijaribu kumshauri rafiki yake, lakini haikusaidia.

Mzee John hakupendezwa na majibu ya rafiki yake, akaomba apewe yule mtoto ili akamsomee kwake, mzee George kwa kuona anapunguziwa mzigo alikubari. Mzee John aliondoka na Anthony huku akiahidi kumpeleka shule.

***
Anthony akiwa kwa mzee John alikuwa mtoto mtiifu, mzee John na mke wake walimpenda sana. Walikuwa na watoto wawili, Paul na Antonia. Paul alikuwa darasa la 1 shule ya mission. Antonia alikuwa ni binti mdogo.

Anthony aliandikishwa shule ile ile ya mission aliyokuwa anasoma Paul, alikuwa mtiifu sana nyumbani na shuleni. Walimu wake walimpenda.

****

Akiwa darasa la 3, walipokea taarifa ya kifo cha baba yake, nyumba yao ilishika moto akiwa amelala ndani, kutokana na ulevi mzee George alishindwa kujiokoa , akachomwa na ule moto mpaka mauti.

Mke wake alifanikiwa kukimbia, ila hakurudi tena pale nyumbani. (kulikuwa na tetesi ndie aliwasha ule moto , sababu haikujulikana).

Anthony akawa amepoteza wazazi wote wawili, akabaki yatima. Mzee John aliendelea kumlea kama mwanae bila kumbagua, alipomaliza darasa la nne, mzee John alihamia mkoa wa Arusha na familia yote.

Waliishi kijiji cha ngurudoto wilaya Meru. Akiwa arusha aliendelea kuwa kijana mwema. Alipofikisha umri wa kuoa, alimshirikisha mzee John kama baba, mzee alimwambia anapenda amuozeshe binti yake maana iliona atamfaa zaidi. Hakupenda amruhusu kuoa kabila la wenyeji wao.

Kipindi hicho Antonia alikuwa na miaka 16, ilikuwa mwaka 1962, mzee John aliamua kumuozesha kijana wa rafiki yake ili amtunzie baba yake jina, alimpa binti yake Antonia awe mke wake.

Baada ya kuoa kimira , Anthony aliamua kuhama pale nyumbani, alihamia kijiji ''X'' mkoa ''X''. Maisha mapya ya ndoa yalianza rasmi.
**********
View attachment 2552603View attachment 2552605
winston20 na nana_ karibuni.
Hadi nawaonea wivu kwa namna mtakavyofaidi huu uzi.
 
Mzee kwanza hongera kuiwakilisha vyema nchi huko mambele, ulianzia India ukapita Ulaya, Arabuni na Amerika, kama stori ingendelea nadhani ungefika Asia.
Barikiwa sana.
 
Asante mkuu, hawapendi kukususia mtoto, tatizo ni kipata kidogo ndio maana wanataka mshirikiane.

Wapo hapa hapa bongo wenye pesa zao, unawzalisha tunamalizana, shida yao mtoto.
Daaaaah yashanikuta hayo mzee mwenzangu kila nikimfikilia yule man'gati wangu....issue kdg tu kazimia hili la kumletea mtoto anajua ntauwa bule mtoto wa watu.
Basi hata nikiambiwa ntalea mwenyewe natokea mlango wa uani.
 
Back
Top Bottom