This is a Typical case of a Plausible Deniability. And, that of Denying the antecedent.
Kipindi cha uhamasishaji wa Umma umeisha, na sasa tunaingia hatua tofauti.
Walitufanya tufahamu tatizo(la kutungwa), au kwa lugha nyingine, kwamba wale waliokuwemo (Wazalendo)hawakuwa Wazalendo, na matokeo yake tumeona yanayofanyika. Tumepigwa!
Walitushirikisha kwa Ulaghai na watu walipoanza kushirikiana na kushikamana wakageuka na wakaanza kushambulia mshikamano wetu. Matusi yanarudi na lugha za kiutenganishi, makabila, uweusi, udini oh mwisilamu wewe mkristo yule n.k n.k Tumepigwa!
Sasa wameleta seti mpya kabisa, ya kuanza kutetea ukoloni mamboleo. Ati amelaghahiwa? hakuna rushwa huko? Kweli?
Kwamba tukubali huu mkataba ulivyo?
Kwanini asitoke aseme wewe Mlaghahi, wewe umekula rushwa, wewe haufai? Isitoshe ni hodari wa Teua Tengua Nini kinamshinda?
Nafikiri ni muhimu kusisitiza kuwa kwa sasa Mkataba huu haufai kabisa, hatuhitaji kuurekebisha, yani utupiliwe mbali.
Nikweli sasa, Mkataba huu unawatenganisha Wazalendo na Wanaojali Nchi na Rasilimali zake na wale Wazalendo feki Wanaotumiwa, yaani mavibaraka wa Mabeberu wanotaka kutunyonya na Kututawala.
Tuukatae Mkataba huu na Uwekezaji wa aina yeyote ule unaoenda kumshusha Mwafrika.