Mkataba wa Bandari: KKKT muelewe hili kwanza

Apo umenena fact brother! Maana hoja ya mr itafanya watu haswa waumini wa kkkt kukosa imani na kiongozi wetu. Ulivofafanua nimeelewa
 
Mimi siyo muumini wa roman Catholic lakini nimewaelewa sana TEC kwa kuwa na jicho lenye huruma kwa wananchi.
Nilitarajia maaskofu wengine pamoja na mashehe wangeungana kukemea dhuluma hii inayokwenda kuliumiza taifa kwa muda mrefu.
Ni wakati sasa viongozi wa dini waache kuwa waoga wa dola kwani sauti zao zina impact kubwa sana
 
KKKT sio tawi la dhehebu lolote hapa nchni, tunatusahili heshima" kanisa halipingi uwekezaji" tufuatilie hotuba ya mkuu wakanisa letu KKKT sio tumlishe maneno ambayo hayakutamkwa na mkuu wa kanisa. KKKT ni dhehebu linalojitegemea wote wanaoabudu mbezi Luis wameajiliwa huko bandarini!? Kikapu likipita kanisani unashikiwa fimbo kutoa hiyo sadaka si kama unacho ndio unatoa?

Je, kanisa likisema tunapinga uwezekaji ndio waumini wake wanakuwa na uwezo wa kulipa wachungaji wetu hata kwa miezi 3 ikiwa waumini wake hawatakuwa na uwezo wa kumtumikia kanisa kwa sadaka?. Kanisa hili lilikuwepo hata kabla ya miaka yako hiyo 18 uyulioabudu wewe. Minada mingi hamia kwingine kule wake zenu wanatandandika mpaka vitanda vya wachungaji wao
 
Baba ameshasema kwa niaba yetu..sisi ni nani hata tumpinge kiongozi wetu..Amesema kanisa Lina mwamini na lipo pamoja na rais wetu.. Ahsante baba kwa hotuba nzuri..
 
Hebu weka hapa sehemu ambayo askofu Shoo anasema ansunga mkono mkataba wa DPW.
Huyo Shoo mwenyewe amejichanganya, hata alikuwa haelewi anaeleza nini, Mara tulileta mapendekezo yetu, mara naunga mkono jitihada zote na tunaunga mkono uwekezaji! Hali mradi mzee wa watu alijikuta katika wakati mgumu kwa kibano alichojiwekea mwenyewe kwa uropokaji wake.
 

Mkuu bado unakwenda kanisani? Huko ni kujitakia madeni ya lazima. Au unaogopa ukifa utakosa mchungaji wa kukuzika nini? Mbali na kuzikwa na mchungaji siku ya mwisho, hakuna jambo lolote la maana unaweza kupata toka kanisani, bali kanisa linategemea fedha yako kuendesha shughuli zake. Dini ya kweli ni pesa, hizo nyingine ni porojo tu.
 
Juzi kuna mchungaji kaingia kakuta tarazo zimewekwa akasema ziwekwe mpya material yapo tanzania akasema anaagiza yeye nnje ndio mazuri yaani ni upigaji kila kona.
Ogopa matapeli kwa jina la Mungu. Mimi nimestuka muda mrefu. Mungu wa kweli hana shida ya pesa. Huko kanisani bila pesa unaonekana mzigo. Hamstuki tu hao wapigaji wenye majoho?
 
Nimeamini kweli linapokuja suala la hela, mchagga atabaki kuwa mchagga tu! Hii kauli ya Shoo imekaa kimitego sana na kimnuso wa mbesa. Bila shaka mama atakuwa kaingizwa king akajua kwamba shoo yupo upande wa uungaji mkono mkataba wa DPW!

1) "Sisi KKT tunaunga mkono uwekezaji...(Yet nobody is contra when it comes to investing our natural resources provided it abides to the constitutional of URT)"

"Tumeshatoa mapendekezo ya uboreshwaji wa vipengele vya mkataba wa DPW..."(Hapa anamaanisha kwamba mkataba ulikuwa na mapungufu ambayo yanahitaji review)

Sasa kwakuwa Mama anaokoteleza uungwaji mkono juu ya hili sakata, naamini atakuwa kaacha bahasha nzito na nene kwa Shoo.
 
Askofu Shoo hajasema anabariki mkataba wa bandari!! Amesema anaunga mkono uwekezaji!! Na kuna mawazo walishampa tayari rais na akaahidi kuyafanyia kazi!! Kama kanisa lingekuwa linaunga mkono mkataba wa bandari kama ulivyo lisingekuwa na sababu ya kutoa maoni na mapendekezo kuhusu mkataba!!
 
yes haeleweki
 
KKKT, TEC, BAKWATA, CCT na taasisi nyingine za dini hata wananchi walio wengi hawapingi uwekezaji au kwa maneno mengine wanaunga mkono uwekezaji.
Hata hivyo, wapo wanaopinga au kutaka mkataba wa DP world urekebishwe.
Sasa, kama nilivyomsikia askofu Shoo, anamtaka Rais Samia na serikali yake watekeleze ushauri au maoni waliyoyatoa huko nyuma, na atoe neno la kumaliza changamoto/tatizo hiyo inayoligawa taifa. Ameonesha busara ya hali ya juu katika kuzungumzia hilo.
Hata hivyo, ni muhimu kujua kwamba waraka wa TEC haupingi uwekezaji, bali unapinga mkataba wa DP World kama ulivyo.
Twahitaji kumuomba Mungu atuwezeshe kutumia vizuri utashi, fikra na akili nzuri alizotupatia bure.
 
Askofu Shoo unasema unabariki uwekezaji ni uwekezaji gani huo wa kijinga namna hii, unampa mtu Bandari kwa mkataba wa kudumu huo ni uwekezaji au uuzaji wa Bandari?
Wapi Askofu shoo kasema ana support DP world kupewa bandari? Yeye kaongelea uwekezaji basi kaishia hapo kuhusu Dp world kasema wameshapeleka maoni Yao means vifungu vyenye shida wameviainisha na whether or not mkataba ni mbaya au mzuri wamefikisha kwa Mama Sasa kivipi Tena ionekane ame support?

Mimi sio KKKT lakini tupunguze mihemko waTanzania tusilishane maneno
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…