Mkataba wa Bandari: KKKT muelewe hili kwanza

Mkataba wa Bandari: KKKT muelewe hili kwanza

Mimi ni muumini wa hili kanisa usharika wa Mbezi Louis, tokea nianze kusali nikiwa sunday school pale ni mwaka wa 18 sasa, katika vitu nlivyogundua ni kwamba haya makanisa hasa Kkkt yanaendeshwa kupitia sadaka za waumini yaani waumini wakisema wasitoe sadaka ndani ya miezi 3 tu hali ya viongozi ipo taabani

Usiposhiriki misa au kutoa Sadaka unaonekana mkosaji, ibada nzima ni michango tu kikapu kuanzia mwanzo hadi mwisho watu wanakamuliwa ni pesa kwenda mbele ila sijui kama wanajua hizo pesa zinapotokea ni wapi

Linapokuja swala la uchumi tunatakiwa tuwe kitu kimoja, kesho kama taifa tukiingia mikataba mibovu alafu kesho tukaja kuivunja nchi ikiingia kwenye madeni mazito haumii mtu mwingine tunaumia wote ndio haya matozo na kodi kubwa walizoweka huu ni mwanzo tu picha linakuja Viongozi wetu wa KKKT ikifika mahali mkaambiwa kuwa hatuna pesa sababu uchumi umeharibika muwe wasikivu maana ibada zenu ni kuomba pesa mwanzo mwisho, hajawajenga wachungaji na wainjilisti kujitegemea kiuchumi mmewajenga kuwakamua waumini kwenye kapu la sadaka.

Askofu Shoo unasema unabariki uwekezaji ni uwekezaji gani huo wa kijinga namna hii, unampa mtu Bandari kwa mkataba wa kudumu huo ni uwekezaji au uuzaji wa Bandari? Kesho akiingia kiongozi type ya Magufuli akauvunja mwishowe DP world wataenda mahakamani halafu tukidaiwa mabilioni ya pesa wanatuwekea Tozo na kodi kubwa tulipe wananchi, wananchi tukishapigika tukija makanisani mikono mitupu muwe waelewa maana kodi kubwa ni chanzo cha kufanya watu wafilisike.

Niwapongeze Roman kwa kuwa wakweli maana mmeona mbali, waumini wenu mnajua kabisa uchumi wao ukiyumba utaleta shida hadi kwenu ila uchumi ukinyooka hata kwa kanisa ni faida kubwa.

Na Mama ajue kuwa hatupingi maendeleo wala uwekezaji ila tunapinga uwekezaji wenye Dalili zote zinazoashiria uuzwaji wa mali zetu, Cha kwanza tunachotaka kujua ili Tumbariki mama kwenye Hili la Do world ni haya

1.Mkataba ni wa muda gani kwa nini kuna viashiria kuwa mkataba ni wa milele usalama uko wapi hapo, unawezaje kumpangishia mtu nyumba yako kwa mkataba wa kudumu?

2.Imekuwaje Ubinafsishe Bandari zote za Bara alafu za Zanzibar uziache Hivi Zanzibar hawapendi maendeleo? kama wanayapenda imekuwaje wao hawamo? Tukumbuke kuwa mikopo yote mikubwa Zanzibar mama hakuwasahau alihakikisha wanapata mgao wao, ila hii anayoiita Neema Zanziar hawapo maana yake ni nini?

3.Dp world kuna kipengele kuwa anapinga kuanzishwa au kuendelezwa kwa bandari mpya hadi yeye apewe taarifa na aamue yeye kubariki hilo?, Hivi fikiria kampuni ya bia ya TBL,TCC Zilipoingia ubia na wazungu wangeweka sheria kuwa hakuna kampuni yoyote ya bia itakayoruhusiwa kuanzishwa au kuzalisha bia, Ila ni TBL Pekee yao ndio mwenye hiyo kazi hebu fikiria hivi viwanda vyote pinzani vinavyoiingiza kodi kubwa serikali mfano wazee wa Serengeti Light think TBL angeweka kipengele leo Serikali ingepoteza mapato makubwa kiasi gani kwa kumlilia mtu mmoja

Endapo wazungu wa TANZANIA CIGARETTES COMPANY wangesema enzi hzo kuwa mkataba usomeke kuwa hakuna kampuni yoyote itakayoruhusiwa kufanya biashara ya kuuza sigara au kuzalisha zaidi yetu hivi think hivi viwanda pinzani visingekuwepo hali ingekuwa vipi na ni kwa nini Mkubali kusaini mkataba ambao unapinga uanzishwaji au uendelezwaji wa Bandari mpya hadi Dp ato idhini hapa ndipo shida yetu ila tukihoji mnasema tunaligawa Taifa jibuni hizi hoja.

2.a
Umesahau viwanda vya sukari
 
Ukisikiliza kwa makini Askofu Shoo hakuunga mkono mkataba wa Bandari!! Amesema walimpa ushauri Samia juu ya huo mkataba na yeye aliahidi kuwa angeyafanyia kazi mapendekezo yao.
Askofu akamalizia na kibwagizo ambacho nadhani kilimlenga mkwere kuwa " TUNAPOWAKOSOA MNATUAMBIA TUNACHANGANYA SIASA NA DINI"!
Ukiwa na akili ndogo utasema Dr Shoo kaunga mkono mkataba wa Bandari.

Nashukuru wenye akili kubwa tumemwelewa Shoo bado anamkumbusha Dr Samia kufanyia kazi ushauri uliotolewa na TEC,BAKWATA..........

DR Shoo katumia hekima kubwa katika kufikisha
 
DR Shoo katumia hekima kubwa katika kufikisha ujumbe kwa serekali na hasa Rais Dr Samia.
 
Sisi
Nyie mnapotosha sijui kwa manufaa ya nani.
na nani tunapotosha? issue pale ilikuwa ni DP world, na hakuna aliye muuliza, amelikoroga mwenyewe badala ya kujikita kwenye maadhimisho amejitia kitanzi mwenyewe kwa kiherehere chake, matokeo yake Rais mwenyewe akawa mjanja akapindua meza!
 
KKT hawawezi kutufikia sisi Roman kwa michango!Ila Sijakubaliana na walichokifanya TEC pamoja na Uroman wangu.Ule ni "uhuni"
 
Kkkt kwenye vikapu hawajambo. Unaweza kukuta unazunguka Mara tano na baada mnada unapigwa na michango ya jumuiya ipo ya kutosha. Waumini mnageuka kuwa miradi.
Kwenye Jumuiya nako kuna sadaka mbili, moja ya Jumuiya na nyingine Usharikani.....
 
Toka mwanzo wa sakata hili hakuna aliyepinga uwekezaji kilichopingwa ni aina ya mkataba na kasoro nyingi ambazo, zitaiumiza nchi. Hata wanasheria wengi walilalamikia hilo. Nimemsikiliza Askofu Shoo vizuri alichokisema KKKT inaunga mkono uwekezaji, kuhusu mkataba alimwambia Rais, alipokutana nao walimshauri mambo ya kurekebisha na aliahidi angefanyia kazi.
Kuhusu sadaka, kwanza nina mashaka na ulutheri wako, Kuna mahali umesema mnapokuwa na MISA, ukweli walutheri tuna ibada na hatuna Misa, hiyo ibada ya Misa utaikuta RC au Anglican high church.
Aidha makanisa mengi ya kilutheri tuna utaratibu wa kusomewa taarifa ya fedha angalau kila baada ya miezi mitatu. Mchungaji hajipangii mshahara au posho, hupangwa na Kamati za fedha.
Michango yote kanisani ni hiari na inatakiwa ukiamua kutoa, utoe kwa moyo.
Wingi wa sadaka, kila sadaka Ina sababu yake, na mambo mengi washarika hushirikishwa.
Sikatai kuwepo kwa ukiukwaji wa matumizi ya fedha, hilo si jambo la ajabu, wanaoendesha na kusimama kanisa/ Usharika ni wanadamu wa kawaida, mapungufu hayawezi kukosekana.
 
ok
 
Hajasema anaunga mkono dp world,Amesema anaunga mkono uwekezaji kwani Kuna anaepinga uwekezaji?
Sikiliza tena hotuba yake utamwekewa,pale alifinya kimyakimya

Chukueni tahadhari msijejikuta bila kujua ni manabii wa baal chini ya yezebeli.
 
Back
Top Bottom