Mkataba wa Bandari: KKKT muelewe hili kwanza

Ukisikiliza kwa makini Askofu Shoo hakuunga mkono mkataba wa Bandari!! Amesema walimpa ushauri Samia juu ya huo mkataba na yeye aliahidi kuwa angeyafanyia kazi mapendekezo yao.
Majini yataendesha mradi
 
Asante kwa mada nzuri. Sahihisho kidogo. Sio Roman bali Catholic
 
Kila MTU anakubali Uwekezaji. Ila Mkataba WA huo Uwekezaji unakataliwa Una Mapungufu yafanyiwe KAZI.
 
Kama ni mtihani kajibu kwa kukurupuka hajaelewa katikati ya mistari

Sent from my Nokia C10 using JamiiForums mobile app
 
Hakuna nchi inayokataa uwekezaji, hapa tatizo ni elimu ndogo ya uelewa inayowakabili wengi, sidhani kama wewe unaukataa uwekezaji na ndicho kinachofanyika kwenye klabu za michezo, viwanja binafsi vya nyumba, makampuni na viwanda binafsi, ila kinachojadiliwa ni aina ya mkataba ambao unatakiwa uwe na maslahi pande zote mbili hivyo Shoo asingeweza kusema hatutaki uwekezaji na hakuna mpaka sasa aliyekataa uwekezaji bali kinachokataliwa ni mkataba unaoegemea upande mmoja; si vizuri kujitahidi kupindisha hoja ilimradi usiyempenda aonekane mbaya, weka hapa sehemu aliyosema hawataki au wanataka uwekezaji husika wa DPW.
 
Askofu ni Mtu mkubwa na muhimu sana na anapoongea jambo ajue watu wanamsikiliza kwa makini sana, hivyo hapaswi kuwa mnafiki vinginevyo yeye ndiye atakuwa anawagawa waumini wake na pale alitakiwa aongee kwa mtizamo wake bila ya kuwahusisha watu ambao hajakubaliana nao kwamba wanaunga mkono uwekezaji au vipi achia mbali huo wa DPW, TEC wameonesha msimamo na kutoa walicho kubaliana, maana inaonekana wazi hawakukurupuka waliupitia mkataba, waka pitia maoni ya watu mbalimbali wakiwemo Serikali wenyewe, wakajadiliana na hatimae wakaja na jawabu la nini wamekiona katika yote waliyopitia na kutoa mapendekezo yao katika huo Walaka wao, hao ndiyo hawana unafiki, Nyeupe wanaita Nyeupe na Nyeusi wameita Nyeusi.
 
Well said!!
Viongozi wa KKKT wametumia busara kubwa sana kumwambia SSH kuwa li mkataba lake halifaii!
Ila wasiokuwa na akili hawaelewi!
Hongera sana Askofu Dr. Shoo.
KKKT na TEC wamesimama na wananchi!!
Nina imani hata Nape, Tulia, na watetezi wengine wa DP World wakitumbuliwa Leo kesho watakuwa upande wa TEC na wananchi!!
 
kuanzia sasa, kkkt ndio dhehebu la kikristo lenye urafiki na sisi waislamu. Allah awalinde sana viongozi wa kkkt.

tumswalie mtume....
 
Mleta Uzi hivi umeelewa Kweli alichozungumza Askofu?hivi unajua Kweli kumsikiliza Kwa makini na kuchambua hoja??Kifupi KKKT hawajakubaliana na mkataba wa bandari,unadhani Kwa Nini mama alikuwa anakula kalamu?hebu nenda You tube tulia msikilize baba Askofu wako
 
Yes!sijui watu wameshindwa vipi kuelewa Ile speech iliyojaa hekima na utulivu katika kupinga Huo mkataba.
 
Hivi wewe unaweza kukataa uwekezaji! Mbona wachina wamewekeza marekani na uingereza, tunachozungumzia ni mkataba lazima uwe na maslahi kwa pande zote mbili, msipende kupindisha maneno kwa makusudi.
 
Leo ndio nimeelewa kwanini Marais wakristo wote walitoka Catholic Church.
 
KKKT wametumia uugwana wasimvue nguo mgeni rasmi,ila speech Iko wazi kabisa Kwa mtu yeyote mwenye upeo wa fikra kwamba hawajakubaliana na mkataba, fullstop.
 
Hajasema anaunga mkono dp world,Amesema anaunga mkono uwekezaji kwani Kuna anaepinga uwekezaji?
Sikiliza tena hotuba yake utamwekewa,pale alifinya kimyakimya
Kuna watu kuelewa hata kiswahili tu ni tatizo halafi ndio hao eti na wao wanataka kuujadili mkataba wa DP
 
Vikao vinaendelea Makumira na agenda ya DP world inawezekana ikawepo na tamko likatoka. Tuwe na subra.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…