Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Safari hii tumesema LITOKE JUA INYESHE MVUA tutapambana kuwavua nguo WABAGUZI WOTE WA UKABILA ,KANDA NA DINI ..

Nguli Ahmed Rajab amemaliza....[emoji120][emoji2956][emoji7][emoji7]

Binafsi ni kijana wa huku bara....nimekuwa nikijitathmini mwenyewe....

Nilipokuwa chuo kikuu nilikuwa kiongozi mwenye kuwakusanya wanafunzi wote na kuondoa unyonge kwa kila aliyejitia na kutiwa unyongeni....

Siku moja niliitwa na kuulizwa kuwa nimetokea Zanzibar ?!!

Nilishangaa sana.....

Mimi ni mnyakyusa kwetu ni Matema Kyela ila nilikulia mkoa mmoja ulio pwani....lafidhi yangu ni ya mtu wa pwani....japo jina linatoa picha kamili ya Unyakyusa wangu....

Nilichokuja kugundua ni kuitwa mswahili kwa kule tu kujitambua thamani yangu ya utu na kumthamini kila aliyekuwa mbele yangu toka nikiwa mdogo kwani nilianza kuzisoma makala za magazeti ya Rai ya akina kamarada Ulimwengu na wenzake nikiwa na miaka 8 tu....

Ubaguzi haupo tu dhidi ya wazanzibari...pia kuna hii tabia ya baadhi ya wazanzibari KUWADHARAU wabara....na kuwaona watu wasiostaarabika kwa kuwaita "machogo" na majina tofauti yenye kukirihisha...hili nalo halina afya kwa raia ndugu wa nchi moja....

Ndg.Ahmed Rajab amefungua "Pandora box"...tuna ulazima wa kufundisha watoto wetu kuondokana na UJINGA wa kujiona bora zaidi ya wengine...

Mh.Mbowe ni miongoni mwa watu wanaosukumwa na UBAGUZI huo dhidi ya mh.Rais Dr.SSH.....

#SayNoToRacism[emoji120]
#SayNoToBigotry[emoji120]
#TaifaMojaWatuWamoja[emoji120]

#SiempreJMT[emoji120]

#MamaAnaupigaMwingi[emoji2956]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Na Ahmed Rajab

KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha.

Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba. Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake. Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China. Wasia wake unasema: “kama hujafanya utafiti, huna haki ya kusema.”

Kuna jambo moja lakini ninaloweza kulisema ingawa halihusiki moja kwa moja na mkataba wenyewe. Linahusika, kwa jumla, na ushirikiano au miamala kama hii inayofanywa katika haya yaitwayo mazingira ya utandawazi. Kwa kawaida, miamala hii hufuata kanuni na taratibu za ubepari uliopevuka. Na ubepari wa aina hiyo huwa na harufu ya ubeberu ambao ndio daraja ya juu ya ukoloni. Ndio maana kuna haja kubwa ya kuipiga darubini na kuichunguza vilivyo mikataba aina hiyo isije ikawa ni ya kuzikaba na kuzitia kwapani nchi kama zetu.

Tusisahau jinsi ukoloni ulivyoanza. Ulikotoka na ulipofika. Makampuni kutoka nchi za Ulaya yalikwenda katika nchi za wengine kusaka bidhaa kama dhahabu, madini ya fedha, karafuu na kungumanga; mwishowe ikazitawala nchi hizo. Kampuni ya Uingereza ya East India Company, kwa mfano, ilihodhi biashara katika nchi za Asia na ikaishia kuzihodhi nchi hizo kiutawala, kwa kuzitamalaki na kuzigeuza koloni. Huo ndio uliokuwa ukoloni asilia. Siku hizi za utandawazi unajigeuza gamba na kuwa ukoloni mamboleo.

Tangu wiki iliyopita mitandao ya kijamii imegeuzwa majaa ya kutupia lawama dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kisingizio cha kuukosoa huo mkataba wa bandari. Kwa ninayoyasikia inaonesha kwamba kweli kuna baadhi ya mambo yasiyokaa sawa katika mkataba huo na yanabidi yarekebishwe. Lakini kusema kweli lawama nyingi zinazovurumishwa dhidi ya huo mkataba ni za upotoshaji. Tena wa makusudi.

DP World, kwa mfano, si kampuni mburu mbatara, chambilecho jamaa wa barazani. Ni jikampuni lenye uzoefu mkubwa sana wa shughuli za bandarini. Miongoni mwa kazi zake ni kusimamia utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu vikiwa pamoja na mazao yanayouzwa nchi za nje. Jikampuni hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kimataifa na lina kampuni tanzu kadhaa katika nchi mbali mbali.

Tangu 2010 DP World imekuwa ya tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni yenye kuendesha bandari. Kwa hivyo, uzoefu wake wa shughuli za bandarini umevuka bahari ya Dubai na umetia gati katika bandari za sehemu tafauti duniani.

Hapa ningependa kuwakosoa wakosoaji wa mkataba wa DP World kwa kusema kwamba sio kweli kuwa kuna vilio katika nchi ambazo DP World imewekeza. Bila ya shaka kumekuwako watu waliokuwa wakilalama lakini sio wenye kulia. Kuna tafauti kubwa baina ya kulalamika na kuangua vilio. Kweli kumekuwako na malalamiko kuhusu uwezekaji huo katika nchi zao.

Hilo ni jambo la kawaida katika utekelezaji wa mikataba ya kiuchumi ya kimataifa. Na ndio maana tumeshuhudia kesi zikifunguliwa katika nchi mbali mbali za kuishitaki DP World kuhusu masharti ya ushirikiano wake na nchi hizo. Kutokana na hayo ni sahihi kabisa kuwa Tanzania iwe na hadhari ili mkataba huo usiwe na masharti yatayoipendelea kampuni ya DP World na kuionea Tanzania. Panahitajika uangalifu mkubwa.

Tusisahau pia kwamba DP World nayo imefungua kesi kadhaa dhidi ya wabia wao katika baadhi ya nchi.

Mwenyekiti na mkuu wa kampuni hii ni mfanyabiashara mashuhuri wa Dubai, Sultan Ahmed bin Sulayem. Kwa muda mrefu babake alikuwa mshauri wa aila ya kifalme ya Dubai.

Sulayem ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Temple kilicho Philadelphia, Marekani. Alihitimu katika miaka ya mwisho ya mwongo wa 1970 na aliporudi kwao alianza kazi akiwa afisa wa forodha.

La kuhuzunisha kutokana na mijadala ya mitandaoni kuhusika na kadhia hii ni kujitokeza tena kwa chuki na ubaguzi wa kikabila na kidini. Ilivyo ni kwamba baadhi ya Watanzania wenye msimamo sahihi wa kupinga ubaguzi wanapofanyiwa Waafrika, huona ni sawa na haki yao kuwabagua watu wa makabila mengine.

Ubaguzi huo haukuibuka tu vivi hivyi. Tuseme kweli: ubaguzi huo umo ndani ya nyoyo za Watanzania wengi hasa miongoni mwa wanasiasa wa Bara na wale wanaojiita wasomi. Baadhi yetu hatukushangaa kwa sababu tumetambua zamani kwamba kuna ukabila wa kukirihisha Tanzania.

Baadhi ya wanasiasa wakuu wa Tanganyika wamekuwa wakiutumia ubaguzi kutufitinisha sisi wanaotuita ndugu zao wa Zanzibar. Furaha yao ni kutuona tukipapurana sisi kwa sisi. Wanaifuata mbinu ya wakoloni ya kuwagawa watu wa taifa moja ili iwe rahisi kuwatawala.

Wenye kutoa matamshi ya kibaguzi si watu ambao ndimi zao ziliteleza. Walijua wanasema nini, kwa mintarafu gani na kwa faida ya nani.

Kuna bibi mmoja alihoji kwamba Tanzania inarudi utumwani. Alifika hadi ya kuthubutu kusema “tunarudi kwenye utawala wa kisultani…angalau tunaweza kutawaliwa na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu.”

Ilivyo ni kwamba huyo bibi anajitia mwenyewe utumwani. Kuhiari ukoloni wa taifa moja kwa kuukataa wa taifa jengine ni kuwa na fikra za kitumwa, za kuridhia na kukubali kutawaliwa na wengine. Mzalendo halisi hupinga ukoloni wa aina zote, wa rangi zote na wa kabila zote. Na hupinga isimu ya ukoloni kwa kutumia njia au nyenzo zozote alizonazo kwa kufanya kinachohitajika.

Tamko la kwamba afadhali tutawaliwe na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu ni tamko lisilo na hata chembe ya uzalendo. Ni ulaanifu wa kibaguzi wenye kuitusi historia yetu na kututukana sote. Inasikitisha, tena sana, kuwasikiliza wenye kujigamba kwamba ni wasomi na wanaharakati wenye kupigania haki wakiropokwa namna hivyo.

Tamko hilo linatukumbusha maneno yaliyojaa ubaguzi wa kikabila na udini yaliyowahi kutamkwa hadharani katika nyakati tafauti na waziri wa zamani William Lukuvi pamoja na Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wanachofanya wakosoaji hao ni kuwatetanisha Watanganyika na Wazanzibari. Na huko huko Tanganyika kwenyewe kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu.

Badala ya kuwa makini na kutoa hoja zenye mashiko ya kimantiki wakosoaji hawa wamekurupuka na, kwa pupa, bila ya kuutalii walianza kuuponda huo mkataba unaotarajiwa baina ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kutumia upotoshaji badala ya ukweli katika utetezi wao.

Panaweza pakawa na sababu za kweli za kuukosoa mkataba huo na kila mwenye kuona taksiri zozote katika masharti ya ushirikiano huo ana kila haki ya kulitoa joto lake. Lakini afanye hivyo kwa hoja zenye kujikita juu ya yaliyo kweli. Si kwa kujitia jazba za ubaguzi.

Wasomi ndio tunaowataraji wawe safu ya mbele kuwapiga darubini watawala na kuwakosoa wanapostahiki kukosolewa. Wanapomuona mtawala yuko hadharani bila ya nguo wanatakiwa wawe na ujasiri wa kupaza sauti na kumwambia, kinagaubaga, kwamba yuko uchi. Lakini wanatakiwa wafanye hivyo pakiwa na ushahidi.

Maswali ya kujiuliza ni kwa nini wakajigeuza wehu na wakacharukwa hivyo? Kwa nini wakachuna nyuso wakaona ni sawa na ni haki yao kuupinda na kuupotosha ukweli? Kwa nini wakatumia lugha ya kibaguzi?

Hawa ni watu wanaojiona kuwa ni wasomi. Ingefaa tuwaonee huruma lau wangelikuwa wanayasema wayasemayo kutokana na ujinga wa kutoujua uhalisia wa mkataba wenyewe. Lakini hawa hawamo katika kaumu hiyo.

Hawa ni maafiriti. Ni maluuni wenye ajenda nyingine iliyo kubwa na ovu na wanayoiengaenga isije ikavuja hadharani na mapema. Mijicho yao imelenga mbali. Inauangalia mwaka 2025 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa mwaka huo nchini Tanzania.

Inavyoonesha ni kwamba wamevinjari kufanya juu chini ili Rais Samia Suluhu Hassan asiwe mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha CCM. Na kama watashindwa katika njama hiyo basi wanataka kuhakikisha pasiwepo tena Rais wa Muungano atayetoka Zanzibar.

Ajabu ya mambo ni kuona mlingano wa dhamira baina ya wanaCCM wenye kumchimba Rais wao na wengine walio nje ya CCM wenye kuicheza ngoma isiyo yao. Wote wanatumia ubaguzi wa kikabila na udini. Kwao, hili ni jambo la kufa au kupona, la pata potea.

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. Ana shahada ya Falsafa kutoka Birkbeck, Chuo Kikuu cha London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.

View attachment 2656186
[emoji2956][emoji2956][emoji7][emoji7]

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ahmed rajab humjui? Ni ile mizee inayolamba miguu waarabu ni mzanzibar huyo
Mungu akusamehe sana kwa kuwa mbaguzi...WEWE NI MBAGUZI....

UBAGUZI NI USHETANI....

Badala ya kujibu hoja yake unatanguliza ARGUMENTUM AD HOMINEM... .

Hivi mbali na ubaguzi ulio nao...ulikwenda shule kusomea "upumbavu"?!![emoji15][emoji15][emoji1787][emoji1787]

Hivi bado Ahmed Rajab anasikilizwa ?
 
MKATABA WA BANDARI UMEONESHA RANGI ZAO

Picha: Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam.

Na Ahmed Rajab

KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai.

Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha.

Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba.

Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake.

Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China.

Wasia wake unasema: “kama hujafanya utafiti, huna haki ya kusema.”

Kuna jambo moja lakini ninaloweza kulisema ingawa halihusiki moja kwa moja na mkataba wenyewe.

Linahusika, kwa jumla, na ushirikiano au miamala kama hii inayofanywa katika haya yaitwayo mazingira ya utandawazi.

Kwa kawaida, miamala hii hufuata kanuni na taratibu za ubepari uliopevuka.

Na ubepari wa aina hiyo huwa na harufu ya ubeberu ambao ndio daraja ya juu ya ukoloni.

Ndio maana kuna haja kubwa ya kuipiga darubini na kuichunguza vilivyo mikataba aina hiyo isije ikawa ni ya kuzikaba na kuzitia kwapani nchi kama zetu.

Tusisahau jinsi ukoloni ulivyoanza. Ulikotoka na ulipofika.

Makampuni kutoka nchi za Ulaya yalikwenda katika nchi za wengine kusaka bidhaa kama dhahabu, madini ya fedha, karafuu na kungumanga; mwishowe ikazitawala nchi hizo. Kampuni ya Uingereza ya East India Company, kwa mfano, ilihodhi biashara katika nchi za Asia na ikaishia kuzihodhi nchi hizo kiutawala, kwa kuzitamalaki na kuzigeuza koloni.

Huo ndio uliokuwa ukoloni asilia.

Siku hizi za utandawazi unajigeuza gamba na kuwa ukoloni mamboleo.

Tangu wiki iliyopita mitandao ya kijamii imegeuzwa majaa ya kutupia lawama dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kisingizio cha kuukosoa huo mkataba wa bandari.

Kwa ninayoyasikia inaonesha kwamba kweli kuna baadhi ya mambo yasiyokaa sawa katika mkataba huo na yanabidi yarekebishwe.

Lakini kusema kweli lawama nyingi zinazovurumishwa dhidi ya huo mkataba ni za upotoshaji.

Tena wa makusudi.

DP World, kwa mfano, si kampuni mburu mbatara, chambilecho jamaa wa barazani.

Ni jikampuni lenye uzoefu mkubwa sana wa shughuli za bandarini.

Miongoni mwa kazi zake ni kusimamia utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu vikiwa pamoja na mazao yanayouzwa nchi za nje.

Jikampuni hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kimataifa na lina kampuni tanzu kadhaa katika nchi mbali mbali.

Tangu 2010 DP World imekuwa ya tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni yenye kuendesha bandari.

Kwa hivyo, uzoefu wake wa shughuli za bandarini umevuka bahari ya Dubai na umetia gati katika bandari za sehemu tafauti duniani.

Hapa ningependa kuwakosoa wakosoaji wa mkataba wa DP World kwa kusema kwamba sio kweli kuwa kuna vilio katika nchi ambazo DP World imewekeza.

Bila ya shaka kumekuwako watu waliokuwa wakilalama lakini sio wenye kulia.

Kuna tafauti kubwa baina ya kulalamika na kuangua vilio.

Kweli kumekuwako na malalamiko kuhusu uwezekaji huo katika nchi zao.

Hilo ni jambo la kawaida katika utekelezaji wa mikataba ya kiuchumi ya kimataifa. Na ndio maana tumeshuhudia kesi zikifunguliwa katika nchi mbali mbali za kuishitaki DP World kuhusu masharti ya ushirikiano wake na nchi hizo.

Kutokana na hayo ni sahihi kabisa kuwa Tanzania iwe na hadhari ili mkataba huo usiwe na masharti yatayoipendelea kampuni ya DP World na kuionea Tanzania.

Panahitajika uangalifu mkubwa.

Tusisahau pia kwamba DP World nayo imefungua kesi kadhaa dhidi ya wabia wao katika baadhi ya nchi.

Mwenyekiti na mkuu wa kampuni hii ni mfanyabiashara mashuhuri wa Dubai, Sultan Ahmed bin Sulayem.

Kwa muda mrefu babake alikuwa mshauri wa aila ya kifalme ya Dubai.

Sulayem ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Temple kilicho Philadelphia, Marekani.

Alihitimu katika miaka ya mwisho ya mwongo wa 1970 na aliporudi kwao alianza kazi akiwa afisa wa forodha.

La kuhuzunisha kutokana na mijadala ya mitandaoni kuhusika na kadhia hii ni kujitokeza tena kwa chuki na ubaguzi wa kikabila na kidini.

Ilivyo ni kwamba baadhi ya Watanzania wenye msimamo sahihi wa kupinga ubaguzi wanapofanyiwa Waafrika, huona ni sawa na haki yao kuwabagua watu wa makabila mengine.

Ubaguzi huo haukuibuka tu vivi hivyi.

Tuseme kweli: ubaguzi huo umo ndani ya nyoyo za Watanzania wengi hasa miongoni mwa wanasiasa wa Bara na wale wanaojiita wasomi.

Baadhi yetu hatukushangaa kwa sababu tumetambua zamani kwamba kuna ukabila wa kukirihisha Tanzania.

Baadhi ya wanasiasa wakuu wa Tanganyika wamekuwa wakiutumia ubaguzi kutufitinisha sisi wanaotuita ndugu zao wa Zanzibar.

Furaha yao ni kutuona tukipapurana sisi kwa sisi.

Wanaifuata mbinu ya wakoloni ya kuwagawa watu wa taifa moja ili iwe rahisi kuwatawala.

Wenye kutoa matamshi ya kibaguzi si watu ambao ndimi zao ziliteleza.

Walijua wanasema nini, kwa mintarafu gani na kwa faida ya nani.

Kuna bibi mmoja alihoji kwamba Tanzania inarudi utumwani.

Alifika hadi ya kuthubutu kusema “tunarudi kwenye utawala wa Kisultani…angalau tunaweza kutawaliwa na Mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu.”

Ilivyo ni kwamba huyo bibi anajitia mwenyewe utumwani.

Kuhiari ukoloni wa taifa moja kwa kuukataa wa taifa jengine ni kuwa na fikra za kitumwa, za kuridhia na kukubali kutawaliwa na wengine.

Mzalendo halisi hupinga ukoloni wa aina zote, wa rangi zote na wa kabila zote.

Na hupinga isimu ya ukoloni kwa kutumia njia au nyenzo zozote alizonazo kwa kufanya kinachohitajika.

Tamko la kwamba afadhali tutawaliwe na Mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu ni tamko lisilo na hata chembe ya uzalendo.

Ni ulaanifu wa kibaguzi wenye kuitusi historia yetu na kututukana sote.

Inasikitisha, tena sana, kuwasikiliza wenye kujigamba kwamba ni wasomi na wanaharakati wenye kupigania haki wakiropokwa namna hivyo.

Tamko hilo linatukumbusha maneno yaliyojaa ubaguzi wa kikabila na udini yaliyowahi kutamkwa hadharani katika nyakati tafauti na waziri wa zamani William Lukuvi pamoja na Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wanachofanya wakosoaji hao ni kuwatetanisha Watanganyika na Wazanzibari.

Na huko huko Tanganyika kwenyewe kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu.

Badala ya kuwa makini na kutoa hoja zenye mashiko ya kimantiki wakosoaji hawa wamekurupuka na, kwa pupa, bila ya kuutalii walianza kuuponda huo mkataba unaotarajiwa baina ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kutumia upotoshaji badala ya ukweli katika utetezi wao.

Panaweza pakawa na sababu za kweli za kuukosoa mkataba huo na kila mwenye kuona taksiri zozote katika masharti ya ushirikiano huo ana kila haki ya kulitoa joto lake.

Lakini afanye hivyo kwa hoja zenye kujikita juu ya yaliyo kweli.

Si kwa kujitia jazba za ubaguzi.

Wasomi ndio tunaowataraji wawe safu ya mbele kuwapiga darubini watawala na kuwakosoa wanapostahiki kukosolewa.

Wanapomuona mtawala yuko hadharani bila ya nguo wanatakiwa wawe na ujasiri wa kupaza sauti na kumwambia, kinagaubaga, kwamba yuko uchi.

Lakini wanatakiwa wafanye hivyo pakiwa na ushahidi.

Maswali ya kujiuliza ni kwa nini wakajigeuza wehu na wakacharukwa hivyo?

Kwa nini wakachuna nyuso wakaona ni sawa na ni haki yao kuupinda na kuupotosha ukweli? Kwa nini wakatumia lugha ya kibaguzi?

Hawa ni watu wanaojiona kuwa ni wasomi.

Ingefaa tuwaonee huruma lau wangelikuwa wanayasema wayasemayo kutokana na ujinga wa kutoujua uhalisia wa mkataba wenyewe.

Lakini hawa hawamo katika kaumu hiyo.

Hawa ni maafiriti.

Ni maluuni wenye ajenda nyingine iliyo kubwa na ovu na wanayoiengaenga isije ikavuja hadharani na mapema.

Mijicho yao imelenga mbali.

Inauangalia mwaka 2025 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa mwaka huo nchini Tanzania.

Inavyoonesha ni kwamba wamevinjari kufanya juu chini ili Rais Samia Suluhu Hassan asiwe mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha CCM.

Na kama watashindwa katika njama hiyo basi wanataka kuhakikisha pasiwepo tena Rais wa Muungano atayetoka Zanzibar.

Ajabu ya mambo ni kuona mlingano wa dhamira baina ya wanaCCM wenye kumchimba Rais wao na wengine walio nje ya CCM wenye kuicheza ngoma isiyo yao.

Wote wanatumia ubaguzi wa kikabila na udini.

Kwao, hili ni jambo la kufa au kupona, la pata potea.

Mohamed Said uko upande upi ?
 
wewe shoga unayesapoti ushoga uliyeweka mstari ambao mashoga wanasema Yesu alisema kuna watu wamezaliwa mashoga, ni upotoshaji, shetani mkubwa we. huu ni upotoshaji. kama haujui, hakuna hata sehemu moja Yesu alisema kuna watu wamezaliwa mashoga.

Matthew 19:10-12​

10 The disciples said to him, “If this is the situation between a husband and wife, it is better not to marry.”
11 Jesus replied, “Not everyone can accept this word, but only those to whom it has been given. 12 For there are eunuchs who were born that way, and there are eunuchs who have been made eunuchs by others—and there are those who choose to live like eunuchs for the sake of the kingdom of heaven. The one who can accept this should accept it.”

nini maana ya eunuchs?, hawa ni watu waliokuwa wanahasiwa ili wawe walinzi wa wake za mfalme au wake wa royal family enzi ya zamani. kwahiyo, alichosema ni kwamba, kuna watu wengine wanazaliwa hawana nguvu za kiume na wengine wanahasiwa. na kuna uwezekano Paulo akawa alikuwa mmojawapo, na paulo huyohuyo kwenye Warumi 1:26 - 27 amepinga vikali ushoga na kuiita ni dhambi jambo jambo linaloonyesha kwamba pamoja na kwamba inawezekana hakuwa na nguvu za kiume lakini hakuwa shoga, hakuruhusu kupumuliwa kama wewe unayesapoti ushoga. paulo hadi amekufa alisema kuna mwiba (yaani impairment) mwilini amemwomba Mungu amponye lakini ameamua kuishi hivyohivyo. wasomi wanasema aliomba MUngu ampe nguvu za kiume lakini hakupata na akaishi kama mtawa maisha yake yote.

MAANA YA EURUCHS NI HII: Eunuchs were men who were castrated in order to be trusted in overseeing the king's domestic interests, especially in protecting king's harems.

Kwa hiyo tafsiri uliyotuletea ya , eunuch , tuambie kuna mtu gani aliyefanywa eunuch katika kanisa lenu hapa Tanzania na duniani kote ???

Pengine ni wewe ndiye mtu wa kwanza uliyefanywa eunuch 😛 😛
 
Mkataba wa Bandari umeonesha rangi zao

Na Ahmed Rajab

KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai. Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha.

Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba. Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake. Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China. Wasia wake unasema: “kama hujafanya utafiti, huna haki ya kusema.”

Kuna jambo moja lakini ninaloweza kulisema ingawa halihusiki moja kwa moja na mkataba wenyewe. Linahusika, kwa jumla, na ushirikiano au miamala kama hii inayofanywa katika haya yaitwayo mazingira ya utandawazi. Kwa kawaida, miamala hii hufuata kanuni na taratibu za ubepari uliopevuka. Na ubepari wa aina hiyo huwa na harufu ya ubeberu ambao ndio daraja ya juu ya ukoloni. Ndio maana kuna haja kubwa ya kuipiga darubini na kuichunguza vilivyo mikataba aina hiyo isije ikawa ni ya kuzikaba na kuzitia kwapani nchi kama zetu.

Tusisahau jinsi ukoloni ulivyoanza. Ulikotoka na ulipofika. Makampuni kutoka nchi za Ulaya yalikwenda katika nchi za wengine kusaka bidhaa kama dhahabu, madini ya fedha, karafuu na kungumanga; mwishowe ikazitawala nchi hizo. Kampuni ya Uingereza ya East India Company, kwa mfano, ilihodhi biashara katika nchi za Asia na ikaishia kuzihodhi nchi hizo kiutawala, kwa kuzitamalaki na kuzigeuza koloni. Huo ndio uliokuwa ukoloni asilia. Siku hizi za utandawazi unajigeuza gamba na kuwa ukoloni mamboleo.

Tangu wiki iliyopita mitandao ya kijamii imegeuzwa majaa ya kutupia lawama dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kisingizio cha kuukosoa huo mkataba wa bandari. Kwa ninayoyasikia inaonesha kwamba kweli kuna baadhi ya mambo yasiyokaa sawa katika mkataba huo na yanabidi yarekebishwe. Lakini kusema kweli lawama nyingi zinazovurumishwa dhidi ya huo mkataba ni za upotoshaji. Tena wa makusudi.

DP World, kwa mfano, si kampuni mburu mbatara, chambilecho jamaa wa barazani. Ni jikampuni lenye uzoefu mkubwa sana wa shughuli za bandarini. Miongoni mwa kazi zake ni kusimamia utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu vikiwa pamoja na mazao yanayouzwa nchi za nje. Jikampuni hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kimataifa na lina kampuni tanzu kadhaa katika nchi mbali mbali.

Tangu 2010 DP World imekuwa ya tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni yenye kuendesha bandari. Kwa hivyo, uzoefu wake wa shughuli za bandarini umevuka bahari ya Dubai na umetia gati katika bandari za sehemu tafauti duniani.

Hapa ningependa kuwakosoa wakosoaji wa mkataba wa DP World kwa kusema kwamba sio kweli kuwa kuna vilio katika nchi ambazo DP World imewekeza. Bila ya shaka kumekuwako watu waliokuwa wakilalama lakini sio wenye kulia. Kuna tafauti kubwa baina ya kulalamika na kuangua vilio. Kweli kumekuwako na malalamiko kuhusu uwezekaji huo katika nchi zao.

Hilo ni jambo la kawaida katika utekelezaji wa mikataba ya kiuchumi ya kimataifa. Na ndio maana tumeshuhudia kesi zikifunguliwa katika nchi mbali mbali za kuishitaki DP World kuhusu masharti ya ushirikiano wake na nchi hizo. Kutokana na hayo ni sahihi kabisa kuwa Tanzania iwe na hadhari ili mkataba huo usiwe na masharti yatayoipendelea kampuni ya DP World na kuionea Tanzania. Panahitajika uangalifu mkubwa.

Tusisahau pia kwamba DP World nayo imefungua kesi kadhaa dhidi ya wabia wao katika baadhi ya nchi.

Mwenyekiti na mkuu wa kampuni hii ni mfanyabiashara mashuhuri wa Dubai, Sultan Ahmed bin Sulayem. Kwa muda mrefu babake alikuwa mshauri wa aila ya kifalme ya Dubai.

Sulayem ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Temple kilicho Philadelphia, Marekani. Alihitimu katika miaka ya mwisho ya mwongo wa 1970 na aliporudi kwao alianza kazi akiwa afisa wa forodha.

La kuhuzunisha kutokana na mijadala ya mitandaoni kuhusika na kadhia hii ni kujitokeza tena kwa chuki na ubaguzi wa kikabila na kidini. Ilivyo ni kwamba baadhi ya Watanzania wenye msimamo sahihi wa kupinga ubaguzi wanapofanyiwa Waafrika, huona ni sawa na haki yao kuwabagua watu wa makabila mengine.

Ubaguzi huo haukuibuka tu vivi hivyi. Tuseme kweli: ubaguzi huo umo ndani ya nyoyo za Watanzania wengi hasa miongoni mwa wanasiasa wa Bara na wale wanaojiita wasomi. Baadhi yetu hatukushangaa kwa sababu tumetambua zamani kwamba kuna ukabila wa kukirihisha Tanzania.

Baadhi ya wanasiasa wakuu wa Tanganyika wamekuwa wakiutumia ubaguzi kutufitinisha sisi wanaotuita ndugu zao wa Zanzibar. Furaha yao ni kutuona tukipapurana sisi kwa sisi. Wanaifuata mbinu ya wakoloni ya kuwagawa watu wa taifa moja ili iwe rahisi kuwatawala.

Wenye kutoa matamshi ya kibaguzi si watu ambao ndimi zao ziliteleza. Walijua wanasema nini, kwa mintarafu gani na kwa faida ya nani.

Kuna bibi mmoja alihoji kwamba Tanzania inarudi utumwani. Alifika hadi ya kuthubutu kusema “tunarudi kwenye utawala wa kisultani…angalau tunaweza kutawaliwa na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu.”

Ilivyo ni kwamba huyo bibi anajitia mwenyewe utumwani. Kuhiari ukoloni wa taifa moja kwa kuukataa wa taifa jengine ni kuwa na fikra za kitumwa, za kuridhia na kukubali kutawaliwa na wengine. Mzalendo halisi hupinga ukoloni wa aina zote, wa rangi zote na wa kabila zote. Na hupinga isimu ya ukoloni kwa kutumia njia au nyenzo zozote alizonazo kwa kufanya kinachohitajika.

Tamko la kwamba afadhali tutawaliwe na mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu ni tamko lisilo na hata chembe ya uzalendo. Ni ulaanifu wa kibaguzi wenye kuitusi historia yetu na kututukana sote. Inasikitisha, tena sana, kuwasikiliza wenye kujigamba kwamba ni wasomi na wanaharakati wenye kupigania haki wakiropokwa namna hivyo.

Tamko hilo linatukumbusha maneno yaliyojaa ubaguzi wa kikabila na udini yaliyowahi kutamkwa hadharani katika nyakati tafauti na waziri wa zamani William Lukuvi pamoja na Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Wanachofanya wakosoaji hao ni kuwatetanisha Watanganyika na Wazanzibari. Na huko huko Tanganyika kwenyewe kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu.

Badala ya kuwa makini na kutoa hoja zenye mashiko ya kimantiki wakosoaji hawa wamekurupuka na, kwa pupa, bila ya kuutalii walianza kuuponda huo mkataba unaotarajiwa baina ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kutumia upotoshaji badala ya ukweli katika utetezi wao.

Panaweza pakawa na sababu za kweli za kuukosoa mkataba huo na kila mwenye kuona taksiri zozote katika masharti ya ushirikiano huo ana kila haki ya kulitoa joto lake. Lakini afanye hivyo kwa hoja zenye kujikita juu ya yaliyo kweli. Si kwa kujitia jazba za ubaguzi.

Wasomi ndio tunaowataraji wawe safu ya mbele kuwapiga darubini watawala na kuwakosoa wanapostahiki kukosolewa. Wanapomuona mtawala yuko hadharani bila ya nguo wanatakiwa wawe na ujasiri wa kupaza sauti na kumwambia, kinagaubaga, kwamba yuko uchi. Lakini wanatakiwa wafanye hivyo pakiwa na ushahidi.

Maswali ya kujiuliza ni kwa nini wakajigeuza wehu na wakacharukwa hivyo? Kwa nini wakachuna nyuso wakaona ni sawa na ni haki yao kuupinda na kuupotosha ukweli? Kwa nini wakatumia lugha ya kibaguzi?

Hawa ni watu wanaojiona kuwa ni wasomi. Ingefaa tuwaonee huruma lau wangelikuwa wanayasema wayasemayo kutokana na ujinga wa kutoujua uhalisia wa mkataba wenyewe. Lakini hawa hawamo katika kaumu hiyo.

Hawa ni maafiriti. Ni maluuni wenye ajenda nyingine iliyo kubwa na ovu na wanayoiengaenga isije ikavuja hadharani na mapema. Mijicho yao imelenga mbali. Inauangalia mwaka 2025 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa mwaka huo nchini Tanzania.

Inavyoonesha ni kwamba wamevinjari kufanya juu chini ili Rais Samia Suluhu Hassan asiwe mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha CCM. Na kama watashindwa katika njama hiyo basi wanataka kuhakikisha pasiwepo tena Rais wa Muungano atayetoka Zanzibar.

Ajabu ya mambo ni kuona mlingano wa dhamira baina ya wanaCCM wenye kumchimba Rais wao na wengine walio nje ya CCM wenye kuicheza ngoma isiyo yao. Wote wanatumia ubaguzi wa kikabila na udini. Kwao, hili ni jambo la kufa au kupona, la pata potea.

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. Ana shahada ya Falsafa kutoka Birkbeck, Chuo Kikuu cha London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.

View attachment 2656186
Rajabu, huwa nakuamini ila kwa hili haupo neutral. Unaegemea uzanzibari na asili yako; uarabu
 
Umeongea saana ila ukweli unabaki kwamba na wewe umeingia kwenye list ya wachumia tumbo!

Umeingia kwenye list ya wadini watetea Samia muislamu kama ilivyo kwa Zitto kabwe na genge lote.

Umeongea saana kwa sababu huna uchungu na Tanganyika!

Nakuuliza jambo moja ili uwaulize wabunge....

Je!
Ni kwa nini walikwenda ziara ya wansyoiita ya mafunzo huko nyumbani kwa Dudu- World au DP World ambako ni Dubai....
Badala ya kutembelea nchi zenye migogoro na Deep World kama Djibout na hizi zifuatazo....msijione wajuaji kuliko watanzania wote...

Ebu tuanzie hapo
ahmed rajab

Ili kujifunza aina na sababu ya chimbuko la migogoro hiyo na kisha kuja kuwa na uwezo wa kulishauri bunge vizuri?

Here is a list of the latest 20 cases versus DP World in international arbitration court:

1. DP World v. Kenya (2022). The International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID) is currently hearing a case brought by DP World against Kenya. DP World is seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Kenya.

2. DP World v. Ethiopia (2022). The ICSID is also currently hearing a case brought by DP World against Ethiopia. DP World is seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Ethiopia.

3. DP World v. Djibouti (2021). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Djibouti. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Djibouti.

4. DP World v. Pakistan (2020). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Pakistan. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Pakistan.

5. DP World v. India (2019). The ICSID dismissed a case brought by DP World against India. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by India.

6. DP World v. Argentina (2018). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Argentina. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Argentina.

7. DP World v. Chile (2017). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Chile. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Chile.

8. DP World v. Uruguay (2016). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Uruguay. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Uruguay.

9. DP World v. Peru (2015). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Peru. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Peru.

10. DP World v. Brazil (2014). The ICSID dismissed a case brought by DP World against Brazil. DP World was seeking damages for alleged breaches of contract and expropriation by Brazil.

It is important to note that these are just a few of the many cases that DP World has been involved in. DP World is a major player in the global port industry, and it has been involved in a number of disputes with governments around the world. These disputes have often been complex and have involved significant financial stakes.

The cases listed above are still ongoing, and it is not yet clear how they will be resolved. However, they provide a glimpse into the challenges that DP World faces as it operates in a number of different countries.
Tutafute maarifa na teknlojia ya kujenga na kuendesha bandari zetu wenyewe, tusitafute wa kutujengea na kutuendeshea.
 
Nimekuwa nikimfuatilia Ahmed Rajab tangu akiandika jarida la kama sio African Now basi ni African Events hadi kuwa mchangiaji kwenye gazeti la Raia Mwema. Hana tofauti sana na mwandishi wa historia ya Tandamti na Kipata Mzee Mohamed Said!
Mara kadhaa huwa nakuwa naye kipindi cha maoni kwenye meza ya duara ya Sauti ya Ujerumani (DW), siku za Jumamosi saa 7 mchana
 
Hizo ni hisia zako tu kuhusu udini lakini Watanzania wote Waislamu kwa Wakristo hawataki huo mkataba wa kubumba bumba kama wewe unakubali mkataba wa hovyo kisa udini basi nenda katubu.
 
Kwa hiyo tafsiri uliyotuletea ya , eunuch , tuambie kuna mtu gani aliyefanywa eunuch katika kanisa lenu hapa Tanzania na duniani kote ???

Pengine ni wewe ndiye mtu wa kwanza uliyefanywa eunuch 😛 😛
hao ni watu wa tamaduni za enzi hizo. walikuwa mabodigadi wa wanawake wanaotoka kwenye ukoo wa kifalme, ili wasiwazalishe walitakiwa kuhasiwa ili wasiwe na nguvu. na ni kweli kuna watu pia wanazaliwa hawana nguvu, ila kuzaliwa kutokuwa na nguvu haimaanishi amezaliwa shoga, hapana. tofautisha hanith na shoda. mahanith wapo wengitu na huwa hawalembui macho kama wewe, ni wanaume wa kawaida tu hawana huo uchoko wenu, ila tu hawana nguvu kumlala mwanamke, hawasimamishi.
 
Ndivyo Yesu alivyosema kwenye hiyo aya ?? Wacha kutuletea hadithi za kanisa ,. Hivi hao wanaofanywa eunuch makanisani kwa tafsiri yako , yaani makanisani kuna body guard wa wanawake na koo za kifalme ????

na pia umesema kuna watu wanazaliwa hawana nguvu yaani watu hao hawazaliwi tena siku hizi ??

Sasa niambie huyo hanith aliyefanywa eunuch kanisani kwenu ni nani ?? au wewe ?+

swali liko pale pale hujalijibu

Kwa hiyo tafsiri uliyotuletea ya , eunuch , tuambie kuna mtu gani aliyefanywa eunuch katika kanisa lenu hapa Tanzania na duniani kote ???

wafalme hawako tena duniani ??

Pengine ni wewe ndiye mtu wa kwanza uliyefanywa eunuch
 
acha ujinga dada. siku hizi hakuna ma eunuch, walikuwepo zamani enzi Yesu alipokuwepo hapa duniani. tafsiri ya enzi hizo ilikuwa ni watu wanaohasiwa ili wawe walizi wa royal family na lengo ili wasifanye nao ngono. mfalme alikuwa na amani walizi wa mabinti zake au wake zake wakiwa wanmehasiwa. hivyo tafsiri ilikuwa ni watu wasiokuwa na nguvu za kiume. sasa Yesu alikuwa anawaeleza watu kwamba, kuna watu wengine wanazaliwa wakiwa mahanith. katika yoote hayo, hakuna sehemu ilimaanisha watu wanazaliwa wakiwa mashoga. najua unatamani iwe hivyo lakini sivyo ilivyo. mistari ya Biblia nimekuwekeeni hapo juu ukiisoma utaelewa.

Mtume Paulo hajawahi kuoa, na alisema yeye ana tatizo mwilini mwake ambalo hakulifafanua na inasemekana yaweza kuwa alikuwa hana nguvu. lakini pamoja na yote, ukisoma Warumi 1:26 amepinga na kulaani ushoga na usagani. Biblia tangu agano la kale kipindi cha sodoma na gomora MUngu amepinga sana ushoga na aliadhibu, hadi Yesu alipokuja na wafuasi wake wote wamepinga ushoga hadi mwisho. ila sina uhakika kama vitabu vingine vinavyoruhusu sunna kama vinapinga ushoga. na huwa sielewi kwanini maeneo yenye imani sana kama zanzibar, tanga na mombasa, au niseme uarabuni yote na waarabu wote wanaogopwa kwa kuingilia kinyume na maumbile. jibu utakuwa nalo wewe mwenyewe kama upo fair katika huu mjadala.
 
MKATABA WA BANDARI UMEONESHA RANGI ZAO

Picha: Sehemu ya Bandari ya Dar es Salaam.

Na Ahmed Rajab

KUMEKUWA na mijadala ya kushangaza nchini Tanzania tangu ibainike kwamba serikali yake inawasilisha bungeni Azimio la kujadili mkataba unaotarajiwa kutiwa saini baina yake na kampuni ya kimataifa ya DP World inayomilikiwa na serikali ya Dubai.

Kiini cha mkataba huo ni Bandari ya Dar es Salaam na nyinginezo zilizo Bara ambayo kampuni hiyo inatarajiwa kuziendesha.

Si dhamiri yangu kuujadili wala kuuhukumu huo mkataba.

Sitofanya hivyo kwa sababu sikuuona na siyajui yaliyomo ndani yake.

Naufata ule wasia maarufu wa Mao Zedong, aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha Kikomunisti cha China.

Wasia wake unasema: “kama hujafanya utafiti, huna haki ya kusema.”

Kuna jambo moja lakini ninaloweza kulisema ingawa halihusiki moja kwa moja na mkataba wenyewe.

Linahusika, kwa jumla, na ushirikiano au miamala kama hii inayofanywa katika haya yaitwayo mazingira ya utandawazi.

Kwa kawaida, miamala hii hufuata kanuni na taratibu za ubepari uliopevuka.

Na ubepari wa aina hiyo huwa na harufu ya ubeberu ambao ndio daraja ya juu ya ukoloni.

Ndio maana kuna haja kubwa ya kuipiga darubini na kuichunguza vilivyo mikataba aina hiyo isije ikawa ni ya kuzikaba na kuzitia kwapani nchi kama zetu.

Tusisahau jinsi ukoloni ulivyoanza. Ulikotoka na ulipofika.

Makampuni kutoka nchi za Ulaya yalikwenda katika nchi za wengine kusaka bidhaa kama dhahabu, madini ya fedha, karafuu na kungumanga; mwishowe ikazitawala nchi hizo. Kampuni ya Uingereza ya East India Company, kwa mfano, ilihodhi biashara katika nchi za Asia na ikaishia kuzihodhi nchi hizo kiutawala, kwa kuzitamalaki na kuzigeuza koloni.

Huo ndio uliokuwa ukoloni asilia.

Siku hizi za utandawazi unajigeuza gamba na kuwa ukoloni mamboleo.

Tangu wiki iliyopita mitandao ya kijamii imegeuzwa majaa ya kutupia lawama dhidi ya serikali ya Tanzania kwa kisingizio cha kuukosoa huo mkataba wa bandari.

Kwa ninayoyasikia inaonesha kwamba kweli kuna baadhi ya mambo yasiyokaa sawa katika mkataba huo na yanabidi yarekebishwe.

Lakini kusema kweli lawama nyingi zinazovurumishwa dhidi ya huo mkataba ni za upotoshaji.

Tena wa makusudi.

DP World, kwa mfano, si kampuni mburu mbatara, chambilecho jamaa wa barazani.

Ni jikampuni lenye uzoefu mkubwa sana wa shughuli za bandarini.

Miongoni mwa kazi zake ni kusimamia utaratibu wa ugavi na usafirishaji wa watu na vitu vikiwa pamoja na mazao yanayouzwa nchi za nje.

Jikampuni hilo limekuwa likiendesha shughuli zake kimataifa na lina kampuni tanzu kadhaa katika nchi mbali mbali.

Tangu 2010 DP World imekuwa ya tatu kwa ukubwa duniani miongoni mwa makampuni yenye kuendesha bandari.

Kwa hivyo, uzoefu wake wa shughuli za bandarini umevuka bahari ya Dubai na umetia gati katika bandari za sehemu tafauti duniani.

Hapa ningependa kuwakosoa wakosoaji wa mkataba wa DP World kwa kusema kwamba sio kweli kuwa kuna vilio katika nchi ambazo DP World imewekeza.

Bila ya shaka kumekuwako watu waliokuwa wakilalama lakini sio wenye kulia.

Kuna tafauti kubwa baina ya kulalamika na kuangua vilio.

Kweli kumekuwako na malalamiko kuhusu uwezekaji huo katika nchi zao.

Hilo ni jambo la kawaida katika utekelezaji wa mikataba ya kiuchumi ya kimataifa. Na ndio maana tumeshuhudia kesi zikifunguliwa katika nchi mbali mbali za kuishitaki DP World kuhusu masharti ya ushirikiano wake na nchi hizo.

Kutokana na hayo ni sahihi kabisa kuwa Tanzania iwe na hadhari ili mkataba huo usiwe na masharti yatayoipendelea kampuni ya DP World na kuionea Tanzania.

Panahitajika uangalifu mkubwa.

Tusisahau pia kwamba DP World nayo imefungua kesi kadhaa dhidi ya wabia wao katika baadhi ya nchi.

Mwenyekiti na mkuu wa kampuni hii ni mfanyabiashara mashuhuri wa Dubai, Sultan Ahmed bin Sulayem.

Kwa muda mrefu babake alikuwa mshauri wa aila ya kifalme ya Dubai.

Sulayem ana shahada ya uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Temple kilicho Philadelphia, Marekani.

Alihitimu katika miaka ya mwisho ya mwongo wa 1970 na aliporudi kwao alianza kazi akiwa afisa wa forodha.

La kuhuzunisha kutokana na mijadala ya mitandaoni kuhusika na kadhia hii ni kujitokeza tena kwa chuki na ubaguzi wa kikabila na kidini.

Ilivyo ni kwamba baadhi ya Watanzania wenye msimamo sahihi wa kupinga ubaguzi wanapofanyiwa Waafrika, huona ni sawa na haki yao kuwabagua watu wa makabila mengine.

Ubaguzi huo haukuibuka tu vivi hivyi.

Tuseme kweli: ubaguzi huo umo ndani ya nyoyo za Watanzania wengi hasa miongoni mwa wanasiasa wa Bara na wale wanaojiita wasomi.

Baadhi yetu hatukushangaa kwa sababu tumetambua zamani kwamba kuna ukabila wa kukirihisha Tanzania.

Baadhi ya wanasiasa wakuu wa Tanganyika wamekuwa wakiutumia ubaguzi kutufitinisha sisi wanaotuita ndugu zao wa Zanzibar.

Furaha yao ni kutuona tukipapurana sisi kwa sisi.

Wanaifuata mbinu ya wakoloni ya kuwagawa watu wa taifa moja ili iwe rahisi kuwatawala.

Wenye kutoa matamshi ya kibaguzi si watu ambao ndimi zao ziliteleza.

Walijua wanasema nini, kwa mintarafu gani na kwa faida ya nani.

Kuna bibi mmoja alihoji kwamba Tanzania inarudi utumwani.

Alifika hadi ya kuthubutu kusema “tunarudi kwenye utawala wa Kisultani…angalau tunaweza kutawaliwa na Mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu.”

Ilivyo ni kwamba huyo bibi anajitia mwenyewe utumwani.

Kuhiari ukoloni wa taifa moja kwa kuukataa wa taifa jengine ni kuwa na fikra za kitumwa, za kuridhia na kukubali kutawaliwa na wengine.

Mzalendo halisi hupinga ukoloni wa aina zote, wa rangi zote na wa kabila zote.

Na hupinga isimu ya ukoloni kwa kutumia njia au nyenzo zozote alizonazo kwa kufanya kinachohitajika.

Tamko la kwamba afadhali tutawaliwe na Mzungu lakini tusitawaliwe na Mwarabu ni tamko lisilo na hata chembe ya uzalendo.

Ni ulaanifu wa kibaguzi wenye kuitusi historia yetu na kututukana sote.

Inasikitisha, tena sana, kuwasikiliza wenye kujigamba kwamba ni wasomi na wanaharakati wenye kupigania haki wakiropokwa namna hivyo.

Tamko hilo linatukumbusha maneno yaliyojaa ubaguzi wa kikabila na udini yaliyowahi kutamkwa hadharani katika nyakati tafauti na waziri wa zamani William Lukuvi pamoja na Samuel Sitta, aliyewahi kuwa Spika wa Bunge la Tanzania na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Wanachofanya wakosoaji hao ni kuwatetanisha Watanganyika na Wazanzibari.

Na huko huko Tanganyika kwenyewe kuleta mtafaruku baina ya Wakristo na Waislamu.

Badala ya kuwa makini na kutoa hoja zenye mashiko ya kimantiki wakosoaji hawa wamekurupuka na, kwa pupa, bila ya kuutalii walianza kuuponda huo mkataba unaotarajiwa baina ya DP World na Mamlaka ya Bandari Tanzania kwa kutumia upotoshaji badala ya ukweli katika utetezi wao.

Panaweza pakawa na sababu za kweli za kuukosoa mkataba huo na kila mwenye kuona taksiri zozote katika masharti ya ushirikiano huo ana kila haki ya kulitoa joto lake.

Lakini afanye hivyo kwa hoja zenye kujikita juu ya yaliyo kweli.

Si kwa kujitia jazba za ubaguzi.

Wasomi ndio tunaowataraji wawe safu ya mbele kuwapiga darubini watawala na kuwakosoa wanapostahiki kukosolewa.

Wanapomuona mtawala yuko hadharani bila ya nguo wanatakiwa wawe na ujasiri wa kupaza sauti na kumwambia, kinagaubaga, kwamba yuko uchi.

Lakini wanatakiwa wafanye hivyo pakiwa na ushahidi.

Maswali ya kujiuliza ni kwa nini wakajigeuza wehu na wakacharukwa hivyo?

Kwa nini wakachuna nyuso wakaona ni sawa na ni haki yao kuupinda na kuupotosha ukweli? Kwa nini wakatumia lugha ya kibaguzi?

Hawa ni watu wanaojiona kuwa ni wasomi.

Ingefaa tuwaonee huruma lau wangelikuwa wanayasema wayasemayo kutokana na ujinga wa kutoujua uhalisia wa mkataba wenyewe.

Lakini hawa hawamo katika kaumu hiyo.

Hawa ni maafiriti.

Ni maluuni wenye ajenda nyingine iliyo kubwa na ovu na wanayoiengaenga isije ikavuja hadharani na mapema.

Mijicho yao imelenga mbali.

Inauangalia mwaka 2025 na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanywa mwaka huo nchini Tanzania.

Inavyoonesha ni kwamba wamevinjari kufanya juu chini ili Rais Samia Suluhu Hassan asiwe mgombea wa urais wa chama kinachotawala cha CCM.

Na kama watashindwa katika njama hiyo basi wanataka kuhakikisha pasiwepo tena Rais wa Muungano atayetoka Zanzibar.

Ajabu ya mambo ni kuona mlingano wa dhamira baina ya wanaCCM wenye kumchimba Rais wao na wengine walio nje ya CCM wenye kuicheza ngoma isiyo yao.

Wote wanatumia ubaguzi wa kikabila na udini.

Kwao, hili ni jambo la kufa au kupona, la pata potea.

Baruapepe: aamahmedrajab@icloud.com; Twitter: @ahmedrajab

Ahmed Rajab ni mwandishi wa kimataifa na mchambuzi. Ana shahada ya Falsafa kutoka Birkbeck, Chuo Kikuu cha London, Postgraduate Diploma (Urbanisation in Developing Countries) kutoka University College, London na shahada ya MA (African Political Economy na Modern African Literature) kutoka Chuo Kikuu cha Sussex.
Kwa hiyo kwa kuwa waarabu ni wa dini.yako wanatakiwa kufunga mikataba yeyote kwa masharti yeyote ya kinyonyaji sisi tukae kimya bila.Hivi Wazanzibari walipofanya mapinduzi walikuwa hawataki nini vile?
 
Back
Top Bottom