Mkataba wa Dubai na Tanzania kuhalalisha Kambi 88 za Masetla wa Kiarabu nchini Tanzania?

Hakiondoki kitu. Nanyumbulisha hoja hapa chini ili akili ikuingie:

Kwa kifupi nimeandika hoja ifuatayo:

1. Kuna wakoloni wa aina mbili, yaani mkoloni wa kimapokeo (traditional colonialism) na mkoloni wa kilowezi (setller colonialism), ambapo, mkoloni wa kimapokeo anafika kwenye koloni ili kuteka rasilimali watu na kuitumia kuvuna maliasili na kuhamisha faida kwa ajili ya kuipeleka katika nchi mkoloni, wakati mkoloni mlowezi anafika kwenye koloni kuteka ardhi, watu na rasilimali zao ili kujenga makazi mapya ya kudumu, ama kwa kuwahamisha wazawa au kuwateketeza.

2. Mkataba wa Tanzania-Dubai umetoa haki ya umiliki wa milele wa haki za matumizi (eternal use ownership rights) ya bandari 88 za Tanzania Bara, na pia umetoa haki ya umiliki wa milele wa haki za kuvuna faida (eternal fruits ownership rights) kutokana na bandari 88 za Tanzania Bara, jambo ambalo linaipa Dubai haki ya kuanzisha makazi ya kudumu katika ardhi ya Tanzania, na hivyo kuwa na sifa ya kuitwa mkoloni mlowezi.

3. Kwa hiyo, nikahitimisha kwamba, Mkataba wa Tanzania-Dubai unafungua milango ya kuanzishwa kwa kambi 88 za walowezi wa Kiarabu nchini Tanzania, ambapo kambi hizo zitakuwa kwenye mwambao wa Pwani na kwenye mmaeneo ya mmaziwa ya Tanganyika, Viktoria na Tanganyika.
Leo umeugusa sana moyo wangu.
Dijaeahi kukuunga mkono katika bandiko lako kama leo.

Uishi mama
Ibarikiwe sana.

Tuungane kukemea huu uhayaeani
 
na walivyo waharibifu aisee hakuna sehemu walipita pakawa salama. hata njia ya kati ya utumwa ukiangalia kuanzia pwani, dodoma, kondoa hadi ujiji sehemu walizopita utafikiri laana ilimwagwa, ni maeneo yaliyojaa uchawi, uganga, uzinzi na ukame wa rdhi, njaaa na kukosa elimu.
 
Kongole kwako Mama Amon,

Pamoja na Heshima na nafasi uliyonayo sirikalini, Bado umeamua kuwa MZALENDO.

Tuungane Kwa pamoja kukataa UOVU huu juu ya nchi yetu.

Mungu ibariki TANZANIA.

Amen
Mbona kidogo sana?

Sasa hivi Waarabu walio settle Tanzania kwa enzi na enzi wappo wangapi?

Warangi 90% Waarabu.

Wa iraqw ndiyo hata jina lao loinajieleza.
wanyantuzu?
Wanyaturu kibao Waarabu kabisa.

hhaya anzeni kwanza kubaguwana na wajomba na shngazi zenu.

Mkimaliza mje kwa Wamisri wanaojenga Bwawa, hawajaacha wapwa huko?

Nusy au Zaidi ya Kariakoo ni Waarabu.

Sasa ingia wimbi litakalokuja na DPW
Mradi Ongezea.
 
Privatization
Advantages & Disadvantages

AdvantagesDisadvantages
Resources are efficiently usedPrivate players may enter the market, establishing monopoly
Facilitates healthy competitionLess transparent
Risk-sharing with governmentHigher cost to consumers
No political influence

Faida kubwa ya Ubinafsishaji ni kuongeza Ushindani, hence ufanisi na bei kushuka..., Sasa kama mtu anachukua exclusivity nachelea kujiuliza Faida ni ipi Sasa... Akapewe Bandari ya Tanga Mwingine apewe hii na wengine wapewe nyingine (Kila miaka mitano tunakaa mezani na ku-renegotiate terms).... Kwa akili zetu za mgando hatupaswi kuwaamulia wajukuu ni kama Babu zetu Waasisi walivyosema haya mambo tuyaache kwanza tupate akili (it seems like akili zetu zinarudi - reverse)
 
Mbona kidogo sana?

Sasa hivi Waarabu walio settle Tanzania kwa enzi na enzi wappo wangapi?

Warangi 90% Waarabu.

Wa iraqw ndiyo hata jina lao loinajieleza.
wanyantuzu?
Wanyaturu kibao Waarabu kabisa.

hhaya anzeni kwanza kubaguwana na wajomba na shngazi zenu.

Mkimaliza mje kwa Wamisri wanaojenga Bwawa, hawajaacha wapwa huko?

Nusy au Zaidi ya Kariakoo ni Waarabu.

Sasa ingia wimbi litakalokuja na DPW
Mradi Ongezea.
Hoja dhaifu sana Bi Faiza.
 
Huu ni wongo mkubwa!
Iraqw people are cushitic, not arabic as you tend to purport.
Even a language they speak is classified within Afro-Asiatic Family.
 
View attachment 2675281

Hofu tuliyo nayo dhidi ya Mkataba wa Tanzania-Dubai inao msingi thabiti katika ubaya unaoambatana na historia ya "makoloni ya walowezi wa kigeni" katika Afrika.

Kwa mujibu wa "TPA Handbook, 2019-20," kwenye ukurasa wa tisa, TPA inasimamia bandari 88 zifuatazo:
  1. Bandari 18 zilizo katika Ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi, zikiwemo bandari za Dar es Salaam, Tanga, Mtwara, Kilwa, Lindi, Mafia, Pangani, na Bagamoyo.
  2. Bandari 30 za Ziwa Victoria, zikiwemo Mwanza, Bukoba, Kemondo Bay, Nansio, na Musoma.
  3. Bandari 25 za Ziwa Tanganyika, zikiwemo Kigoma, na Kasanga.
  4. Bandari 15 za Ziwa Nyasa, zikiwemo Itungi, na Mbamba Bay.
Mkataba wa wali uliopitishwa na Bunge unaziweka bandari hizi chini ya Kampuni ya DP World, iliyo mali ya Mfalme wa Dubai. Hatimaye makoloni ya walowezi wa kiarabu yatakuwa kama ramani hapa chini inavyoonyesha.

View attachment 2675295
Ramani ya makoloni ya walowezi wa Kiarabi nchini Tanzania miaka 30 ijayo

Mkataba huo hautaji ukomo wa mahusiano kati ya Tanzania na Dubai. Mikataba ya nyongeza haikuwasilishwa Bungeni ili Wabunge wajue haya ni mapatano ya miaka mingapi.

Sina amani na mkataba huu, hata kama Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, anaendesha elimu ya "kufuta hofu".

Kwa ufupi, hakuna uatata kwamba huu ni mkataba wa kutengeneza "makoloni 88 ya walowezi wa kiarabu" ("88 Arabic settler colonies") nchini Tanzania, kama ilivyokuwa huko Afrika Kusini, kulikokuwa na "European settler colonies"

Kitaalam, "makoloni ya walowezi" (settler colonies) ni makoloni kama makoloni mengine, lakini yanakuwa kama kiraka ndani ya nchi iliyo huru kisiasa katika maeneo baki.

Isipokuwa Ukoloni wa Cape Town, ulioanzishwa mwaka wa 1652, makoloni ya walowezi barani Afrika hayakuanzishwa hadi karne ya 19 na kusababisha utawala wa Wazungu wachache dhidi ya wakazi wengi wa kiasili.

Migogoro kati ya walowezi na wakazi wa eneo hilo ililipuka juu ya rasilimali zinazodaiwa na pande zote mbili, hasa juu ya ardhi.

Mara nyingi, kuondolewa kwa ukoloni kwa makoloni ya walowezi barani Afrika kuliambatana zaidi na migogoro ya kivita. Tuangalie tulikotoka, ili tujua tuko wapi na tunapaswa kwenda wapi.

Makoloni ya walowezi wa Kiarabu ni jambo la kuogopwa kama ukoma. Makoloni ya walowezi wa Kiarabu nchini Tanzania hapana.

Na kama kuna mtu bado hajaelewa mantiki ya hii "hapana" haelewi maana na aina za ukoloni. Basi, namwalika asome ufafanuzi ufuatayo kuhusu swali lifuatalo: Ukoloni ni kitu gani na sio kitu gani? Nalijibu kikamilifu hapa chini.

Ukoloni ni kitu gani na sio kitu gani?

Ukoloni ni hali ambapo nchi moja, ama kwa kutumia nguvu za kijeshi au nguvu za ushawishi wa hoja za kilaghai, hudhubiti nchi nyingine kisiasa, kiutamaduni, kijamii na kiakili, ama kwa asilimia ndogo au kwa asilimia zote, hii ikiwa ni mbinu ya kufanikisha unyonyaji wa kiuchumi.

Wanahistoria wanatofautisha aina kuu mbili za ukoloni.

Kuna, ukoloni unaofanyika kwa mkoloni kuweka makazi ya kudumu kwenye ardhi ya koloni, yaani ukoloni wa walowezi (settler colonialism).

Na kuna ukoloni unaofanyika bila mkoloni kuweka makazi ya kudumu kwenye koloni, lakini kupitia kwa wawakilishi wake wachache wanaoweka makazi ya muda maalum kwenye ardhi ya koloni (traditional colonialism).

Kwa upande mmoja, katika ukoloni unaofanyika bila mkoloni kuweka makazi ya kudumu kwenye koloni, lakini kupitia kwa wawakilishi wake wachache (traditional colonialism), nchi moja hutumia nguvu kuidhibiti nchi nyingine kwa kuwatumia wenyeji kufanya kazi za kitumwa katika kuvuna rasilimali zao wenyewe kwa faida ya wakoloni.

Hapa, Taifa linalofanya ukoloni huongeza mali yake kwa kuwatumia wenyeji kama watendakazi wanaolipwa ujira kidogo sana.

Katika utaratibu huu, tofauti na ukoloni wa walowezi, Taifa linalofanya ukoloni hutuma watu wachache kwenye koloni, kama watawala wanaowawakilisha, kama mameneja wa miradi ya kikoloni pekee, bila kuwahamisha wenyeji katika makazi yao.

Ukoloni huu hufanikishwa zaidi kwa njia ya mashamba makubwa, ambapo wakoloni hujikita kwenye madini au zao moja la kibiashara kama vile pamba, kahawa, tumbaku, mpira, au miwa.

Mfano mzuri wa ukoloni wa aina hii umetokea DRC tangu enzi za Mfalme Leopold II wa Ubelgiji alipoamuru DRC ifanywe koloni lake miaka 1870.

Lakini, ukoloni unaofanyika bila mkoloni kuweka makazi ya kudumu kwenye koloni, kupitia kwa wawakilishi wake wachache (traditional colonialism), huweza kutekelezwa kwa njia tofauti.

Mosi, mkoloni huweza kuwakilishwa na magavana kutoka makao makuu ya serikali ya nchi ya mkoloni.

Pili, Serikali ya nchi mkoloni huweza kuunda kampuni ambayo itafika kwenye koloni na kusimamia maslahi ya mkoloni.

Tatu, serikali ya nchi mkoloni inaweza kuteua kampuni ya kimataifa iliyosajiliwa katika nchi nyingine ili kufanya kazi kama wakala wake katika koloni.

Na nne, serikali ya nchi mkoloni huweza kuteua serikali ya nchi nyingine kufanya kazi kama wakala wake katika koloni, lakini serikali wakala ikawa nafanya kazi hizo kupitia kampuni yake ya kibiashara.

Na kwa upande wa pili, katika ukoloni unaofanyika kwa njia ya mkoloni kuweka makazi ya kudumu kwenye ardhi ya koloni, yaani ukoloni wa walowezi (settler colonialism), kundi kubwa la watu huondoka nchini kwao na kuhamia kwenye nchi nyingine.

Wakiwa katika nchi mpya huweka makazi ya kudumu huko, kujiimarisha kiuchumi kwa kutwaa na kuvuna maliasili walizozikuta, kujijenga kisiasa na kijamii, na hatimaye kuwahamisha, au kuwajumuisha wenyeji katika ustaarabu mpya wa kigeni, au kuwateketeza. Lakini, walowezi hawa hubaki watiifu kwa nchi za kibeberu walikotoka.

Mifano mizuri ya mchi ambazo ni makoloni ya walowezi ni Kanada, Amerika, Australia, Kenya, Argentina, New Zealand na Afrika Kusini. Katika nchi hizi, wageni waligeuka wakazi wa kudumu, na katika baadhi ya nchi hizi wazawa wakateketezwa kabisa.

Kwa kuangalia maudhui ya kifungu cha 4(1) na kifungu cha 20 kama vikisomwa pamoja na kifungu cha 23(4) ni wazi kwamba, mkataba wa awali wa Tanzania-Dubai unatoa “eternal use ownership rights,” “eternal fruits ownership rights.

Katika utaratibu wa kawaida wa miammala ya kiuchumi, hakuna kitu kama “eternal use ownership rights” au “eternal fruits ownership rights.” Kilichopo, na kinachopaswa kuwepo ni “temporay use ownership rights” au “temporary fruits ownership rights” zinazohusu bandari zetu 88, kwa Mfamle wa Dubai, kupitia kampuni yake ya DP World.

Hivyo, kutaja “eternal use ownership rights” au “eternal fruits ownership rights” katika mkataba ni sawa na kutoa “substantive ownership rights,” zinazohusu bandari zetu 88, kwa Mfamle wa Dubai, kupitia kampuni yake ya DP World.

Chini ya mkataba huu naiona Tanzania ikianza safari ya kugeuka koloni la walowezi wa Kiarabu kama ilivyotokea huko Kanada, Amerika, Australia, Kenya, Argentina, New Zealand na Afrika Kusini, japo walowezi wa huko hawaku wa waarabu.

Tunapinga jambo hili kwa nguvu zote.

Nimeambatanisha Handbook (2019/20) hapa chini.
Upuuzi kama huu unawapata watu wenye uelewa mdogo wa dunia ya sasa inavyokwenda.

Muda sio mrefu serikali inakwenda kusaini mikataba ya kibiashara na kampuni ya DPW, hizi ngonjera ziende kwa waalimu wa historia wa darasa la nne shule ya msingi.
 
Kuwa na hoja na kuandika uongo ni sawa?
Kambi za masetla? Dpworld wako Rwanda ..kuna kambi ya masetla?
Dpworld wako Uk na German kote huko kuna kambi za masetla? seriously??
Uzi kama huu wa kipumbavu unakupa picha ya akili nyingi za kitanzania za miaka ya sasa. Huwa hazina mantiki zenye kueleweka, zinapenda kujikita kwenye ujinga na udaku matokeo yake wanaaminisha vitu vya kitoto kama hivi anavyoleta mleta mada.
 
Thread nyingine hiyo, ndeeeefu unaweza kudhani labda kuna jipya ndani. Lkn nna uhakika haina jipya hata bila kuisoma.
Ni mwendelezo wa vijithread vya bandari hali ya kuwa wenye bandari yao wamerulia tuli
 
Watu wanagombania mfumo dah inatisha sana kampuni ambayo ipo nchi nyingi ulaya ije ilete ukoloni Tanzania sema tu ukweli mleta Uzi kuwa una hofu na uislam kupewa nguvu na waarabu na mfumo wenu uliotengenezwa kwa miaka mingi kukosa nguvu hapa kila mtu anatetea maslah yake akitawala raisi mkristu inakuwa Tanzania akitawala mwislam inageuka kuwa Tanganyika duh
Wanayoyadhihirisha ni kidogo sana kuliko waliyoyaficha mioyoni mwao
 
Punguza upuuzi wako, shangazi yako amekosea wacha aambiwe ukweli, kama unaumia hutaki aendelee kusemwa mwambie avunje ule mkataba wa hovyo alioingia kwa ujinga wake.
Ujinga ni tatizo la uelewa wako na chuki ulizonazo kwake. Angekuwa rais ni hayati JPM msingethubutu kuongea chochote na muda huu angekuwa keshasaini mikataba ya biashara kitambo tu.
 
Kuwa na hoja na kuandika uongo ni sawa?
Kambi za masetla? Dpworld wako Rwanda ..kuna kambi ya masetla?
Dpworld wako Uk na German kote huko kuna kambi za masetla? seriously??
Think big,Think outside the box..Fikiri ya kesho kutwa..
 
Uzi kama huu wa kipumbavu unakupa picha ya akili nyingi za kitanzania za miaka ya sasa. Huwa hazina mantiki zenye kueleweka, zinapenda kujikita kwenye ujinga na udaku matokeo yake wanaaminisha vitu vya kitoto kama hivi anavyoleta mleta mada.
Bwana Mtanzania,

Kuna wakati unaweza ukahisi wewe uko sahihi lakini ukweli ni kwamba umepoteza. Itoshe kusema hakuna anayekataa uwekezaji hapa Tanzania. Ninyi mnaoshabikia huu mradi mmeangalia upande wa faida na maslahi bila kuangalia vipengele na aina ya mkataba. Sehemu nyingine zote ambapo mmetoa mifano, DP World imesaini mikataba ya tofauti kabisa na huu wa kwetu.

Mwaka 1994, United Arab Emirates na Uingereza walisaini Bilateral Investment Treaty (BIT) ili kulinda uwekezaji baina ya nchi hizo mbili. Ule mkataba ndiyo umeruhusu concession ya DP World kuendeleza na kuendesha bandari ya London Gateway. Kule Uingereza wamapewa bandari moja tu ya London Gateway. Ule mkataba wetu umekaa vibaya mno na unawapa bandari zetu zote. Mkataba unatupa ukakasi mwingi.

Hivi kweli unadhani hakuna watanzania wanaweza kuendesha bandari za kwenye maziwa makubwa hadi uwape kila kitu hawa wageni ? Mtu mjinga tu ndiyo anaweza kushadadia faida za huu uwekezaji bila kuangalia madhara ya muda mrefu ya vifungu vya sheria.​
 
Back
Top Bottom