Inajirudia historia.
Zamani wakoloni walifika kwa kubahatisha wakitumia majahazi na merikebu katika pwani za nchi geni na kuwalaghai watu walioowakuta.
Leo hii sisi wenyewe tunajipeleka hadi kwao kuwalilia waje waokoe jahazi kuwa tumishindwa kuendesha kampuni, shirika la umma na kuwa wizara husika haina maono ya kuwezesha waTanzania waendeshe mfano bandari n.k
Ama kweli historia inajurudia sisi kukimbilia nchi za kaskazini na mashariki ya kati na Mashariki ya mbali kuwa wenyewe hatujiwezi .
Ghengis Khan wa Mongol, waTuruki, WaDachi na waAzetc wa kale walisema ogopa sana wageni wanaoonekana wakija kwenu huku wakiwa wamepanda farasi au wamefika pwani kwa vyombo kama majahazi au merikebu.
Watu hawa wageni wa kutoka mbali hadi kuifunga safari hiyo ujue wana kitu wanakitafuta maana hawawezi kukatiza nyika, majangwa, milima, mabonde au bahari kuu za Hindi, Atlantic, Pacific kwa ajili ya matembezi huku wameacha familia, wake, watoto, wazazi na kwenda nchi ngeni
Merikebu ya kutoka Portugal iliyotumika kukusanya taarifa zilizopelekea kutawala makoloni nchi za mbali
A 15th century Portuguese caravel. it had three masts and a lateen or triangular sail which allowed the caravel to sail against the wind
Conquerors: How Portugal Forged the First Global Empire by Roger Crowley (2015)
Sisi tunapokea bila tahadhari yoyote na kuwahesabu kuwa hawa ni wadau wa maendeleo kuwezesha tujikwamue tulipo kwana. Tunaongozwa na kauli za niamini, nina nia njema nimekuja kuwakomboa kutoka katika kila changamoto ya kijamii kuanzia muachane na miungu yenu ya mizuka, zolelanga tuwachimbie visima vya maji, elimu isiyoendana na uwezo wa kuwakwamua mlipo kwama hadi mpige hatua.
Kifupi tume sarenda mioyo, akili na historia yetu na kusahau kwa makusudi mazima kuwa tuliweza kupambana na mazingira yetu mfano tukichimba visima vya maji vijijini kwa ujuzi tuliorithi kutoka kwa mababu bila kutegemea mfadhili wa kutoka nje, tulilima, kutunza mazingira na kujichimbia mifereji ya kumwagilia mashamba n.k n.k Leo hii hatujiwezi kabisa tumekuwa na ulemavu usio wa kuzaliwa wala ajali ya kuangukiwa na jabali n.k