Mkazi: Siondoki Bonde la Msimbazi bila fidia ya angalau bilioni moja

Wewe unaathirika nini asipohama? Yupo hapo kwa sababu viongozi wapuuzi wametumia madaraka yao kuwaweka hapo.

Wanastahili kuelimishwa kwanza kisha taratibu zingine kufuata.

Vumbapu kabisa
Waelimishwe au wapewe taarifa?

Taarifa imeshatoka kwamba wao ni wavamizi kwa hiyo hawakustahili fidia. Hata hicho wanachopewa ni huruma tu na wala siyo stahiki yao.

Hapo kinachotumika ni sheria.
 
Yaan miaka yote waliyokaa hapo hawakuwa wavamizi? Ila leo baada ya mafuriko ndo wamekuwa wavamizi na taarifa inatoka?

Hayo mafuriko yameanza mwaka huu tyuuh?
 
Wananchi wanaoishi bonde la Msimbazi waliokumbwa na mafuriko wametoa maoni yao baada ya Rais Samia kutangaza wapewe fidia huku ya ardhi ikiwa milioni nne huku jumla wengine wakipata jumla ya milioni sita wakihoji wanaenda kufanyaje ili wapate kiwanja na nyumba huko wanapoenda.

Kijana mmoja amesema hawezi kuondoka kwake kwa fidia iliyotajwa huku mwingine akisema wameambiwa hakuna sheria inayomlazimisha Rais kulipa fidia bali ni huruma ya Rais.

Serikali ilipokea bilioni 463 kwa ajili ya mradi wa bonde la mto Msimbazi ikiwemo ujenzi wa daraja na kuboresha matumizi ya ardhi katika bonde hilo, nusu zikiwa msaada na nusu mkopo.

Sasa si atamezwa, atusombwa na kuondolewa na maji kwa fedheha, uharibifu, maumivu na pengine kuhatarisha uhai wake mwenyewe?

Au ndio ile mkataa pema....

Nawahurumia sana, Allah awafanyiee wepesi wafikie muafaka mwema na Serikali....
 
Wananchi wanaoishi bonde la Msimbazi waliokumbwa na mafuriko wametoa maoni yao baada ya Rais Samia kutangaza wapewe fidia huku ya ardhi ikiwa milioni nne huku jumla wengine wakipata jumla ya milioni sita wakihoji wanaenda kufanyaje ili wapate kiwanja na nyumba huko wanapoenda.

Kijana mmoja amesema hawezi kuondoka kwake kwa fidia iliyotajwa huku mwingine akisema wameambiwa hakuna sheria inayomlazimisha Rais kulipa fidia bali ni huruma ya Rais.

Serikali ilipokea bilioni 463 kwa ajili ya mradi wa bonde la mto Msimbazi ikiwemo ujenzi wa daraja na kuboresha matumizi ya ardhi katika bonde hilo, nusu zikiwa msaada na nusu mkopo.

Nakumbuka hawa watu enzi ya utawala wa mzee wa Msoga walipewa viwanja Mabwepande na mabati juu sasa leo Serikali inawalipa fidia gani
 
Yaan miakaa yote waliyokaa hapo hawakua wavamizi? Ila leo baada ya mafuriko ndo wamekua wavamizi na taarifa inatoka?

Hayo mafuriko yameanza mwaka huu tyuuh?
Walishaambiwa wahame na wakapewa viwanja Mabwepande, wakadai kule ni porini (sasa hivi ni mjini) wakavikataa wakarudi hapo.

Sasa hivi wameambiwa wahame wapewe milioni 4 kila mmoja, halafu anainuka mmoja anabana pua "nataka bilioni 1".

Ulitaka Serikali ifanye nini?
 
Nakumbuka hawa watu enzi ya utawala wa mzee wa Msoga walipewa viwanja mabwe pande na mabati juu sasa leo serikali inawalipa fidia gani
Unapotosha kwa faida ya nani. Hizo nyumba na hao watu ni Duni waache Serikali iwape fidia itakayowasaidia sio mnawakandamiza kwa chuki, wivu na upotoshaji.
 
Nakumbuka hawa watu enzi ya utawala wa mzee wa Msoga walipewa viwanja mabwe pande na mabati juu sasa leo serikali inawalipa fidia gani
Viwanja vile wengine waliviuza kwa bei ya kutupa, na kuna wale waligoma kabisa.

Ya sasa siyo fidia kwa sababu hawastahili fidia bali wanapewa kifuta jasho ambacho nacho wakikataa pia watahama tu.
 
Unapotosha kwa faida ya nani . Hizo nyumba na hao watu ni Duni waache I serikali iwape fidia itakayowasaidia sio mnawakandamiza kwa chuki , wivu na upotoshaji
Hakuna upotoshaji. Yupo sahihi. Sema labda enzi hizo hukuwa na access na media
 
Huyo mtaka bilioni Serikali anaijua au anaisikia kwenye redio.
Kwanza atapewa kesi ya ubakaji, mashahidi kutoka Bukoba, Arusha na SUMBAWANGA watakuwa walimuona akifanya tendo, wengine watasema hiyo sio Mara yake ya kwanza.

Wakati anapambana kuokoa maisha yake wazee wa busara kutoka klabu ya jirani na hapo watamfuta akiwa selo na kumuambia asiwe mjinga.

Mimi nitacheza na majirani lkn serikali, hata mjumbe Nampa shikamoo.
 
Wawape viwanja ni milioni 25 kila mtu, milioni nne hela ya beer hiyo.
 
Na watu wakishaondolewa wote hapo
Serikali isivunje hizo nyumba zote
Wasibakishe hata pagala

Ova
 
Wananchi wanaoishi bonde la Msimbazi waliokumbwa na mafuriko wametoa maoni yao baada ya Rais Samia kutangaza wapewe fidia huku ya ardhi ikiwa milioni nne huku jumla wengine wakipata jumla ya milioni sita wakihoji wanaenda kufanyaje ili wapate kiwanja na nyumba huko wanapoenda.

Kijana mmoja amesema hawezi kuondoka kwake kwa fidia iliyotajwa huku mwingine akisema wameambiwa hakuna sheria inayomlazimisha Rais kulipa fidia bali ni huruma ya Rais.

Serikali ilipokea bilioni 463 kwa ajili ya mradi wa bonde la mto Msimbazi ikiwemo ujenzi wa daraja na kuboresha matumizi ya ardhi katika bonde hilo, nusu zikiwa msaada na nusu mkopo.

subiri upigwe tanganyika jeki!!
 
Back
Top Bottom