Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 166
- 182
Mkazi wa Isamilo Mwanza atuhumiwa kuwabaka na kuwalawiti watoto watano
WATOTO watano wenye umri Kati ya miaka sita hadi saba wamebakwa na kulawitiwa kwa nyakati tofauti katika mtaa wa Isamilo msikitini kata ya Isamilo wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza.
Watoto hao ambao majina yao yamehifadhiwa, ni wanafunzi katika shule ya msingi ya Makongoro na wengine wanasoma shule ya msingi Mkudi.
Watoto hao wamebakwa na kulawitiwa na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Felix Rwechungura mwenye umri wa miaka 50, mkazi wa mtaa huo wa Isamilo msikitini.
Mtuhumiwa huyo inaelezwa amekuwa akiwafanyia watoto hao ukatili huo kwa nyakati tofauti nyumbani kwake ambako ni jirani na nyumbani kwao na watoto hao.
Pia taarifa zinaeleza kwamba mtuhumiwa huyo, mchezo huo mchafu aliyofanyia watoto hao sio mara yake ya kwanza kwani imekuwa ni kaiwada na kwamba tayari miezi kadhaa iliyopita aliwahi kukamatwa na kuachiwa na Polisi kwa tuhuma kama hizo.
Mke wa Felix Rwechungura, Janeth Steven na amekiri mme wake kukamatwa na Polisi jijini humo ambapo amesema tuhuma za mmewe kufanya vitendo hivyo amekuwa akivisikia kutoka kwa majirani zake.
Amesema kuwa mara kwa mara amekuwa akisikia tuhuma dhidi ya mmewe lakini yeye amekuwa akimuuliza mmewe na kukana kujihusisha na vitendo hivyo.
"Tarehe 29 mwezi huu ndiyo mme wangu alikamatwa na Polisi kwa tuhuma hizo, na mimi nimekuwa nikipita kutoka kwenye mihangaiko yangu nayasikia hayo maneno lakini kwa sababu mimi nikimuuliza anakataa nakosa kitu cha kufanya," amesema Janeth.
Amesema yeye muda mwingi unakuta hayupo nyumbani kwake (jirani na nyumbani kwa wazazi wa watoto waliyofanyiwa vitendo hivyo) na kusisitiza kwamba mmewe alikuwa akiwafanyia ukatili huo nyumbani kwao.
Wakizungumza na wasafi wa habari, baadhi ya watoto waliobakwa wamesema kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akiwabaka kwa nyakati tofauti.
Watoto hao ambao ( majina yao yamefichwa) wamesema kuwa Felix amekuwa akiwabaka na kuwalawiti na kuwatishia kuwa atawauwa endapo watamsema kwa wazazi wao.
"Huyu baba amekuwa akitushika na kutupeleka ndani kwake na kutuingizia (anataja) na alikuwa akituambia kama tutasema atatua na kutufanyia vitu vibaya zaidi na tulikuwa tunaogopa kusema," amesema mtoto mmoja.
Regina chacha na Blesia Benedicto ni baadhi ya wazazi wa watoto wamesema kuwa baada ya kupata taarifa hizo walienda kutoa taarifa Polisi na baadae kwenda hospitalini kuwapima watoto hao.
Wazazi hao wameiomba Serikali kumchukulia hatua za kisheria za mtuhumiwa huyo ikiwa ni pamoja na kumfikisha mahakamani ili kuwa fundisho kwa watu wengine wanaofanya vitendo hivyo.
Naye Mjumbe wa Serikali ya mtaa wa Isamilo Msikitini Amina Ramadhan amekiri kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa anashililiwa katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Mwanza.
Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa Shirika lisilo la kiserikali la kutetea Haki za Wanawake na watoto Yassin Ally amesema kuwa alipata taarifa za tukio hilo baada ya wazazi wa watoto hao kumpigia simu.
Amesema wiki moja iliyopita alipigiwa simu na wazazi wa watoto hao, ambapo aliamua kufika katika eneo la makazi yao ili kuzungumza nao ili kufahamu kiundani suala hilo.
Yassin amesema kuwa kutokana na elimu ambayo wamekuwa wakiitoa kwenye jamii imesaidia jamii kutoa taarifa na kuwepo na mwamko na elimu dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwemo ubakaji.
Yassin pia hakusita kuviomba vyombo vya dola kuhakikisha vinachukua hatua za haraka ikiwemo kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo ambaye kwa sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi mkoani humo.
Watoto hao watano waliyobakwa na kulawitiwa wanasoma katika shule za msingi ya Mkudi na Makongoro zilizopo Ilemela na Nyamagana mkoani humo.
Mwisho