Mkazi wa Mpanda akutwa kajiunganishia maji chumbani kwake

Mkazi wa Mpanda akutwa kajiunganishia maji chumbani kwake

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Hii Nchi Kila mtu akipata angle au gape la kutumia basi anatumia bila kupoteza muda.

=========

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mpanda (MUWASA) imemkamata Yusuph Singu mkazi wa mji wa zamani kwa tuhuma za kujiunganishia maji chumbani kwake kinyume na taratibu.

Katika utetezi wake Mzee Yusuph amesema maji hayo wameanza kutumia 2013 baada ya kununua nyumba 2003 ambayo ilikua imeunganishwa maji chumbani huku mke wake akidai baada kuugua mume wake alimwambia atumie maji hayo kutokana na kushindwa kubeba ndoo ya maji.

Majirani wanasema wahajui kama maji anayotumia mwenye nyumBa hayalipiwi.

Kwa upande wake Afisa manunuzi MUWASA Michael Salema amesema baada ya ukaguzi wamegundua baadhi ya maeneo maji yanatoka kinyume na utaratibu.

Aidha amesema ukaguzi huo ni endelevu na wataendelea kuwachukulia hatua wale wote watakaobainika kuharibu miundombinu au kuchepusha maji kwa lengo la kukwepa kulipa bili.
 
Back
Top Bottom