Mke aiba namba za siri za mumewe na kujitumia pesa kila mwezi na kujinunulia vocha kila siku. Nimemwambia amwache usiku huu huu

Ahsante mkuu, umeongea vema kabisa!!
 
Kwa hiyo unaweza kumvumilia mke kicheche (malaya), muongo, ana roho mbaya au mshirikina (mchawi) lakini mwizi tu ndio huwezi kumvumilia?

Mi bana tabia yoyote katika hizo hapo juu napiga chini tu, potelea pote. Naweza samehe labda mchafu au hajui kupika. Najua impact yake sio kubwa na twaweza kurekebishana.
 
Hebu kuwa serious kidogo bhana. Hivi hilo ni kosa la kushadadia kuachwa mtu kweli?. Mshauri yafuatayo huyo jamaa Yako:-
1) ampe namba za Siri zote za benki na mitandao ya sim na ampe ruhusa ya kujitumia akiwa na shida.
2) ampe Hela ya matumizi yake ya kila siku huwezi niaminisha kuwa jamaa eti anamtunza wife wake, na wife anaiba buku LA vocha acha masihara bhana.
3) kama Kuna Hela ya watu imeingia au yeye siku hiyo Hana Hela amwambie mkewe na uzuri wa Hawa viumbe ukiwajali tu waelewa sana
4) waweke malengo ya pamoja na mkewe Ili mkewe ajue haya. Hela iliyopo inamatumizi hii. Hili litasaidia kupunguza mke kuwa anauhitaji wa matumizi binafsi wakati anajua Kuna hili litatusaidia wote.
 

Hawa watakua ni wavulana. Wanaume wengi wa siku hizi ni wavulana. Wasamehewe bure.
 

Kama you don’t give a ‘dam’ ungekataa kabisa kumshauri chochote.
 
Busara iwaongoze wewe na jamaa yako.Mtu alikuwa anachukua bila ruhusa kwenye mfuko wake mwenyewe.Kazi ni kwenu.
SWALI LA KIPUUZI:
-Vipi kama huyo mwanamke angekamatwa anaiba nyumba ya jirani?
 
Mke mwizi wa pesa ndogo ndogo haachwi , kwa upande wangu hizo uamuz huo utakuw wa chin kabsa ambao utagharmu future ya watoto

Labda amuache kwakuw alimkuta kashanzaa nje [emoji1][emoji1][emoji2]
 
Naunga mkono hoja AMWACHE HARAKA SANA Kama Ana uwezo huo wa kuiba ipo siku Atampiga tukio kubwa
 
Unamwambia amwache Mke wake wakati wewe Mke wako upo nae na matatizo ya wanawake hayajatofautiana ni vile haujajua tuu mkia wake kauficha chini roho za kibongo hizo mwambie huyo muhuni ampe hela ya Vocha mke wake kuacha mke kwa sababu ya Vocha aisee ujue hakuna ndoa hapo ni Somali life vita vita tuu...
 
Naunga mkono hoja AMWACHE HARAKA SANA Kama Ana uwezo huo wa kuiba ipo siku Atampiga tukio kubwa
Kuishi na mtoto wa mama mkwe hakuhitaji ukurupukaji na haraka ya hivyo.Mwishowe mtakuja kuoa vimbwenerehi.Tunataka tuuone ukubwa wenu kwa vitendo.Tuthibitishieni kwamba mmekua kimwili na kiakili.
 
Uzi huu utapelekea Siri nyingi za kambi kujulikana kwa wanaume.

Wake wengi huwaibia wanaume zao hela.

Na wanaume ni wadhaifu kwenye kutunza Na kukumbuka.

Ni wasaulifu sana.

Tena kwa Mwanaume mlevi Ndiyo kabisaaa [emoji108]

Wake wengi ni majambazi .

Wengine hadi anajenga kwa Siri kwa kumuibia mumewe [emoji108]
 
Hapana amkanye tu mbona case ndogo hiyo je angeshepuka ingekuwaje kama maamuzi ndio hayoo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…