Mke akikufumania fanya yafuatayo ili akusamehe

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Habari wakuu,

Leo nawaletea mbinu ya kivita ambayo unaweza kuitumia kwa mkeo ili akusamehe kiulaini, mfano kama kakufumania, kakukuta na SMS za michepuko, au kosa lolote kubwa ambalo limeleta ugomvi na linatishia uhai wa ndoa au mahusiano yako,

Tumeambiwa Tuishi nao kwa akili,

Njia nzuri ya kumfanya akusamehe na asahau ni kutumia mbinu ya kuishitua akili yake ghafla, unaihamisha kutoka kwenye ugomvi kwenda kwenye jambo lingine kama jinsi ambavyo treni hubadiri njia stesheni na wewe utabadili akili yake hivyo hivyo.

Mfano Kakufumania nyumbani kwako na anatishia kuondoka, nenda mbali kidogo na nyumbani kusanya watu watatu au wanne wapange kuhusu tukio unalolipanga, mfano AJALI ya boda boda, mpe simu au namba za mkeo mtu mmoja kisha ampigie simu mkeo ampe taarifa kuwa Umepata ajali ya boda boda (umegongwa na boda boda) hujitambui na umepoteza fahamu wametoa laini kwenye simu yako ndio wamekuta jina lake wakaona wampigie.

Baada ya hapo akianza kuja eneo la tukio hakikisha nguo zako zinavumbi zinaonyesha ulikuwa chini na ikibidi zipake damu ya mbuzi au ngo'mbe.

Akifika hapo akukute ulishazinduka jifanye unaugulia maumivu, kisha mtu mmoja ajifanye shuhuda aanze kuelesea tukio lilivokua na asisitize ulikuwa unaonekana mtu mwenye mawazo sana.

Baada ya hapo nendeni wote nyumbani mkapumzike.

Ongezea mbinu nyingine, zinaweza kukusaidia siku moja​
 
Unajua maumivu na hali wanakua nayo hawa viumbe wakikutana na hali kama hiyo mkuu?

Kwanza akishtukia unamfanyia usanii mwingine ndio unazidi kuharibu kabisaaa.

Nilihudhuria kile kikao kikuu kilichosisitiza ukikamatwa kataa katakata, usifanye kosa la kukubali. Nikauliza swali, hata kama kuna ushahidi wa kila aina usiopingika nikatae tu? Nilivyoendelea kuuliza nikatolewa kwenye mkutano chini ya ulinzi mkali.

Achilia mbali kutengeneza ajali ya magumashi, hata kama imetokea ya ukweli anaweza kufika hapo akakumalizia kabisa upotelee jehanam.
Na uwe na bahati apokee simu kama haja ku block.

Ndio maana kupunguza usumbufu, sasa hivi wanahifadhi viberiti na petroli, hawataki ujinga. Wanakupa mazoezi ya moto wa huko unakoenda.

Unapigwa home and away.
 
Taabu yote ya nini?

Omba msamaha tu maisha yaende.

Kwanza utakuta mke wako ndo kachepuka na kakubambika watoto ambao DNA itathibitisha si wako.

Tuishi kwa akili tu.

Mie naamini kwenye kuomba msamaha japo chama chetu kinapinga kabisa hili jambo na niliwahi kutolewa kwenye mkutano mkuu kwa kushauri bora watu waombe msamaha.

Hizi drama zinachochea hasira tu. Anaona kabisa wewe sio mtu wa kuacha hizo mambo, unamfanya kama mjinga, hiyo inaongeza majanga zaidi.

Lingine hao watu unaowahusisha kwenye tukio la kisanii watawaambia tu wengine au wao iko siku wanaweza kutumia hilo jambo dhidi yako, inabidi uwe mtumwa ili mkeo asije kuujua ukweli.
 
Mkikaaa kwa kutulia na wake zenu bila kuchepuka hamtafumaniwa [emoji57]

Hii ajenda tuiweke pembeni kwanza, tunaweza kujaza server za JF bila kufikia muafaka.

Ila mkiendelea kutupiga petrol akili zitarudi.
 
Habari wakuu,

Leo nawaletea mbinu ya kivita ambayo unaweza kuitumia kwa mkeo ili akusamehe kiulaini, mfano kama kakufumania, kakukuta na SMS za michepuko, au kosa lolote kubwa ambalo limeleta ugomvi na linatishia uhai wa ndoa au mahusiano yako,

Tumeambiwa Tuishi nao kwa akili,

Njia nzuri ya kumfanya akusamehe na asahau ni kutumia mbinu ya kuishitua akili yake ghafla, unaihamisha kutoka kwenye ugomvi kwenda kwenye jambo lingine kama jinsi ambavyo treni hubadiri njia stesheni na wewe utabadili akili yake hivyo hivyo.

Mfano Kakufumania nyumbani kwako na anatishia kuondoka, nenda mbali kidogo na nyumbani kusanya watu watatu au wanne wapange kuhusu tukio unalolipanga, mfano AJALI ya boda boda, mpe simu au namba za mkeo mtu mmoja kisha ampigie simu mkeo ampe taarifa kuwa Umepata ajali ya boda boda (umegongwa na boda boda) hujitambui na umepoteza fahamu wametoa laini kwenye simu yako ndio wamekuta jina lake wakaona wampigie.

Baada ya hapo akianza kuja eneo la tukio hakikisha nguo zako zinavumbi zinaonyesha ulikuwa chini na ikibidi zipake damu ya mbuzi au ngo'mbe.

Akifika hapo akukute ulishazinduka jifanye unaugulia maumivu, kisha mtu mmoja ajifanye shuhuda aanze kuelesea tukio lilivokua na asisitize ulikuwa unaonekana mtu mwenye mawazo sana.

Baada ya hapo nendeni wote nyumbani mkapumzike.

Ongezea mbinu nyingine, zinaweza kukusaidia siku moja​
Duuh. Wanaume wa Dar mna shida sana. kwani akiondoka shida ipo wapi
hizo ni mbinu za hali ya chini sana za mtu muoga
 
Mie naamini kwenye kuomba msamaha japo chama chetu kinapinga kabisa hili jambo na niliwahi kutolewa kwenye mkutano mkuu kwa kushauri bora watu waombe msamaha.

Hizi drama zinachochea hasira tu. Anaona kabisa wewe sio mtu wa kuacha hizo mambo, unamfanya kama mjinga, hiyo inaongeza majanga zaidi.

Lingine hao watu unaowahusisha kwenye tukio la kisanii watawaambia tu wengine au wao iko siku wanaweza kutumia hilo jambo dhidi yako, inabidi uwe mtumwa ili mkeo asije kuujua ukweli.
Mkuu umeoa?
 
Basi mkeo mpole na mcha Mungu

Lakini yameshawahi kunikuta na balaa lake sitaki kulikumbuka. Nilikiri ila kwa mbinu za kijasusi ambazo siwezi kuziweka hapa.

Hadi leo najiuliza hiyo akili ilitoka wapi? Lakini hapo ni baada ya kukiri ili kumfanya arudi nyumbani tukayajenge. Huko ndio mchezo ulienda kutekelezwa sasa.

Mbinu bora na isiyo na shaka, baki njia kuu.
 
Lakini yameshawahi kunikuta na balaa lake sitaki kulikumbuka. Nilikiri ila kwa mbinu za kijasusi ambazo siwezi kuziweka hapa.

Hadi leo najiuliza hiyo akili ilitoka wapi? Lakini hapo ni baada ya kukiri ili kumfanya arudi nyumbani tukayajenge. Uko ndio mchezo ulienda kutekelezwa sasa.
Mkui hio mbinu ya kusingizia ajali au kulazwa hospitali nayo inaweza kufanya kazi trust me
 
Back
Top Bottom