Mke akikufumania fanya yafuatayo ili akusamehe

Mke akikufumania fanya yafuatayo ili akusamehe

Mkui hio mbinu ya kusingizia ajali au kulazwa hospitali nayo inaweza kufanya kazi trust me

Sijakataa, ila kwa umri wangu na mambo yangu itakua kucheza chini ya kiwango, imekaa kitoto sana. Umejiuliza utakavyokua unawapanga hao jamaa mshirikiane nao kutengeneza huo usanii wanakuchukuliaje?

Na unauhakika hawatawaambia wengine hiyo siri? Ikivuja ikamfikia mkeo si utakua unazidi kuharibu?

Acha hiyo mbinu iwafae wengine lakini binafsi siwezi kabisa hata kuifikiria.
 
Baada ya kukufumania tumekubaliana yafuatayo
1)Usikiri kosa lako kabisaa
2)piga show Kali na romantic
3)Mnunulie hata zawadi labda kanga viatu au dera
Hapa mwanamke atasahau kila kitu hata jina lake mwenyewe😜😜😜
 
Baada ya kukufumania tumekubaliana yafuatayo
1)Usikiri kosa lako kabisaa
2)piga show Kali na romantic
3)Mnunulie hata zawadi labda kanga viatu au dera
Hapa mwanamke atasahau kila kitu hata jina lake mwenyewe😜😜😜
We jidanganye tu wanawake akili zao wanazijuaga wenyewe tu, unaweza hisi umetatua tatizo kumbe umewekwa kikaangoni anasubiria mda ufike akupige tukio na ww
 
Unajua maumivu na hali wanakua nayo hawa viumbe wakikutana na hali kama hiyo mkuu?

Kwanza akishtukia unamfanyia usanii mwingine ndio unazidi kuharibu kabisaaa.

Nilihudhuria kile kikao kikuu kilichosisitiza ukikamatwa kataa katakata, usifanye kosa la kukubali. Nikauliza swali, hata kama kuna ushahidi wa kila aina usiopingika nikatae tu? Nilivyoendelea kuuliza nikatolewa kwenye mkutano chini ya ulinzi mkali.

Achilia mbali kutengeneza ajali ya magumashi, hata kama imetokea ya ukweli anaweza kufika hapo akakumalizia kabisa upotelee jehanam.
Na uwe na bahati apokee simu kama haja ku block.

Ndio maana kupunguza usumbufu, sasa hivi wanahifadhi viberiti na petroli, hawataki ujinga. Wanakupa mazoezi ya moto wa huko unakoenda.

Unapigwa home and away.
Mimi nimependa jinsi ulivyotolewa kwenye kikao mkuu!
 
Back
Top Bottom