DeepPond
JF-Expert Member
- Nov 18, 2017
- 41,728
- 103,997
- Thread starter
- #501
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu uko well off. Big up!Kurud dukan kwangu hapana,
Lile duka nilimkabidhi kijana wa Oda,analisimamia Hadi leo hii
Sema alipopiga Sana kelele nikampa mradi wa bodaboda za mkataba,wanamletea kipande pale nyumbani. Nao ukafa,usimamizi mbovu.
Nowdays anasimamia mradi wa ng'ombe wa maziwa (anauza maziwa) na mradi wa kuuza maji (nna kisima kikubwa Cha maji pale home)
Ndo anapata pesa zake ndogo ndogo za kujikimu akiwa pale pale home[emoji4]
Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna mengi sana kabla ya kupata mke mwema.
Sahh Sana na inatosha hyo ,Kurud dukan kwangu hapana,
Lile duka nilimkabidhi kijana wa Oda,analisimamia Hadi leo hii
Sema alipopiga Sana kelele nikampa mradi wa bodaboda za mkataba,wanamletea kipande pale nyumbani. Nao ukafa,usimamizi mbovu.
Nowdays anasimamia mradi wa ng'ombe wa maziwa (anauza maziwa) na mradi wa kuuza maji (nna kisima kikubwa Cha maji pale home)
Ndo anapata pesa zake ndogo ndogo za kujikimu akiwa pale pale home[emoji4]
Sent using Jamii Forums mobile app
nategemea kuandika wosia alafuHata Mimi wangu alikuwa na hiyo tabia ugomvi kidogo tuachane na tugawane mali, ili kuepusha kelele na ujuaji mwingi toka hapo sijawahi mshirikisha kitu tena, nimenunua ardhi sana na kuna kiasi kizuri sana benki hajui na nilishaapa na kuweka nadhiri kuwa hatajua kitu chochote zaidi ya vile alivyokuwa ananiimbia wimbo tugawane, yeye siku pekee ambayo anakuja kujua ni siku ambayo mm nimetangulia mbele ya haki/kufa ndo hapo atapojua maana nategemea kuandika wosia alafu yeye hataridhi kitu toka kwangu zaidi ya vile alivyokuwa ananiimbia wimbo.
Hivi hii itakuwa ni chai e?DeepPond katika ubora wake
Na hivi ndivyo anavyofungua mwaka
Washenzi sana hawa jamaa na huwezi amini ni wa makanisa ya kilokole kabisaaa na mapepo wanatoa na mpaka dk hii ameona bora nyumba ya mdogo wake ife ili kuficha aibu[emoji2959][emoji2959] nimemuhurumia sana huyu mwenza ila ukiangalia mbele kidogo linaweza kutokea la kutokea kukawa hakuna pakugusa kwa sababu ya mahusiano mabovu hivyo tunaachana kama meli inazama taratiiiibuUlitumia busara Sana kukumbuka mtoto,
Hawa wachungaji wa kizazi kipya nao changamoto Sana
Haiingii akilini anafukia kombe kisa aliefanya Ni.mchungaj mwenzie[emoji3525]
Sent using Jamii Forums mobile app
Hapa unapiga tu unasepa. Ukijifanya kuweka makazi lazima ukione cha mtema kuni [emoji3062][emoji3062][emoji3062]
Hili swali la msingi sana. Mimi mwenyewe nimewaza hapo angeamua kuchukua angekuwa amekomoleka vipi? Ashukuru tu ni mdada ambaye alishikiwa masikio na hao shangazi ila baba yake ana akili. Wangekuwa hawa magume gume mbona ingekuwa sherehe.Hasira zingine buana..sasa angeamua kuchukua hizo mali ndio ungekuwa umemkomoa..?? #CHAI
Una mafua?Kumbe mama G naye alikuwa na akili ya mama J?
Pole saba
Hakuna mkamilifu..ila wote wawili walisimama kwenye nafasi zaoYah!
Kiukweli namshkuru mungu,
Japo kasoro hazikosekan, ila zinahimilika[emoji1431]
Sent using Jamii Forums mobile app
Safi kabisa!DeepPond katika ubora wake
Na hivi ndivyo anavyofungua mwaka
Demu anabugia Jack Daniels kama azam Embe unategemea atakuwa na akili huyu? 🤣 🤣 🤣
Kama ni hadithi ya kutunga basi ni nzuri Sana tena sana. Lakini kama ni kweli haya yalikutokea unastahiki sifa kwa hayo uliyoyafanya kwa ushujaa kabisa. Mungu awe nawe siku zote.IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.
Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.
Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.
Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.
Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.
Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .
Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.
Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.
Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.
Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.
Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.
Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.
Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.
TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.
Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani na Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai tena kuuza duka langu lolote.
Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake, Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU. wengine ni salamu TU,kila mtu kivyake.
Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatulia akawa mcha mungu na MKE mzur Sana.[emoji1431]
Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material mama wa watoto wangu[emoji4]
Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. Michepuko wote nilonao, vichwa maji tupu, mamaJ inclusive.
KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae, Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na alisaisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]
SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA kingine KILICHONIFANYA NIJIVUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]
ASANTENI SANA WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######
NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai talaka wagawane Mali.
NAWASILISHA[ heemoji1431]