Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Ilikuwa ni mwaka gani mkuu
 
Huyu kenge amenidhurumu usingizi wangu😂😂😂nimeshindwa kulala mpaka nimemaliza kusoma kila neno na kila nukta, hata kama ni stori tu ila ina elimu ya kutosha, stori kama hii ilimshatokea jirani yetu live kabisa japo hapo mazingira ni tofauti kwani hiyo ni Dar but hii ilikuwa mkoani huko mpakani mwa M7. Mpaka nikahisi yawezekana hii stori anaesimulia na mtoto mkubwa ambapo wazazi wake ndo walioathirika na hilo baada ya baba yao kufumaniwa na mkewe na mkewe akaona ni heri waachane.

Sema wife yeye aliamua kujigawia mali zote za nyumbani na dukani pamoja na watoto na kuzipeleka kwao.
Mume anarudi toka ugonini (Uganda)anakuta nyumba tupu,nmaduka tupu hakuna cha mtoto wala mama. Mzee akaamua kutulia ili aanze maisha mapya.

Kizaazaa kule ukweni ndo kilileta balaa baada ya babamkwe kukataa kupokea mali alizokuja nazo bintie na ulikuwa msimu wa mvua, fuso zimeshusha mzigo uwanjani kwa mzee (babamkwe)ni kunyeshenyewa mvua kwa kwenda mbele. Sema mzee akatumia busara ya bintie kuingia na wanae ndani kiubinadamu.

Baba akawa na msimamo kwa bintie kurudisha vitu vya watu na watoto kwamba kama maisha yamemshinda arudi kwake kama alivyoondoka.

Kule home jamaa nae akagoma kuifata familia na mali zake. Wakatuma wazee, viongozi wa dini na Serikali kumwombea msamaha mkewe, mwamba anawambia yeye amemsamehe mke wake ila akitaka kurudi kwake aje mwenyewe na watoto tu bila mali kusudi waanze upya kutafuta upya.

Anyway mimi sio good writter ila hiyo ndoa haijawahi kuvunjika tena hadi leo ni wazee sasa kipindi hicho nipo 15yrs sasa nina 45yrs na kijana wake alikuwa rika langu Nadhan kwa sasa yupo 43yrs. Ndo hii imenikumbusha mbali. Kuna baba mkwe wengine Mungu amewajalia hekima na busara😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Dah brother kweli,uli wakomesha for sure😂😂🙌 uli wapa show ya maana,thats how it supposed to be hamna sababu ya kuchekeana kwenye issues kama hizo
 
Uwiiiiii kwa hadithi hii ningeisoma kabla sijawa mke wa mtu ninge ghairi wallah🙌🏼 huyo mkeo anatembeaje mtaani baada ya sekeseke lile. Haya mambo ya kutingisha kiberiti haya sio poa
 
Nilivyosoma hapa, nikajisemea "kweli umepata mke mwema aisee"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…