Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Mke aliomba talaka tugawane Mali, nilichomfanyia hajawahi kurudia tena

Duh asee kaka pole na hongera sana maana hili jambo lilinianza hata mimi nilipofungua kampuni yangu ilibidi nibadili shares sabab ilikua bado changa na imeanza kuleta mambo mengi ya mali acha tu nimesoma hadi nimejikuta nalia [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]

Sent from my moto g power (2021) using JamiiForums mobile app
Pole Sana mkuu,
Ni kipind tu kinapita ktk maisha
Unaumia,unasahau na maisha yanasonga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ila wanawake ni kama wamezaliwa na ujinga wa asili hivi

Ni nadra sana kumkuta mwanamke anawaza hata miaka 2 mbele.

Miaka 3 nyuma,wife kuna kipindi wakati naanza maisha nilisema nimshirikishe mke wangu kwenye mipango

Basi nikawa napiga deal mixer kazi kwa mwezi Nampa 700k mara M.1 sometimes 650k..

Hapo achana na budget ya emergency ambayo Kila mwezi nilikuwa naweka 250k.

Sasa siku nayopewa termination of contract najua kabisa emergency funds Nina km 5.8M huku kwingine najua nina kama 14M.

Nikajisemea hapa sitaki tena Ajira nitaendelea na mishe zangu, Sasa namwambia wife mkataba wangu umeisha hautaongezwa zilete zile hela tufanye mahesabu tujue tunaanza wapi..

Nashangaa mtu anatoa machozi, mimi moja kwa moja nikajua mke wangu kaumia kusikia Sina Kazi nikaanza kubembeleza mbona akiba tunayo na kazi zipo nyingi sana kwenye fani yangu!!Ni vile tu mi sina mpango wa kuajiriwa baada ya mda nikamwambia lete hela tufanye mahesabu akaenda kuchukua kama 650k kaweka kitandani,mi nikamwambia lete zote akasema ndo hizo zimebaki....

Kumbuka mi najua nina 20M. Kasoro hivi aisee hasira zilinipanda ghafla pumzi ikawa inakaba km nataka kupata presha hivi aiseeee pembeni kulikuwa na kastuli flani hivi napendaga kuwekea simu usiku nikiwa nalala, kuna roho iliniingia ya kikatili nilitamani nishike kistuli nimbamize nacho Cha kichwa bahati nzuri niligeuka kumuangalia sura yake na mke wangu ana sura ya kipole sanaaa na kamwili kake kalivyo kadogo plus mimi nishawahi kufanya mazoezi makali ya boxing nikisema nipige liver shot moja naweza hata kuua...

Nikatoka nikaenda kukaa sebuleni kwanza nawaza si ningemuumiza sana!!hivi presha ndo inashika vile!nilijiogopa sana kwakweli.Sijawahi kumpiga toka tumeanza mahusiano ila nikapata picha kwanini wanaume wanapigaga wake zao tena bora mwenye mkono wa kupiga makofi maana atakuwa anapiga kdg kdg,mimi niliwazA kumuumiza yaani ukimuona unasema eee huyu mwanaume kweli katili..nilijiogopa sana kwakweli.

Siku 3 sijui nifanye nini kusema popote naona aibu siwezi mwambia mama yangu siwezi kusema kwao siwezi mwambia rafiki yangu yaani nimekaa nalo moyoni natoka naenda kushinda Bar nikifika tu mlango wa nyumbani hasira zinawaka moto ,kazi sina akiba yangu ya mambo yangu ilikuwa ni 3.5M plus 650k tu Hela yote ndo wife kawapa ndugu zake wafungue biashara, nyingine kajenga choo Cha baba yake nyingine kanunua mavitu Yao ya kike.

Niliumia sana sanaaaaaa kilichokuwa kinaniuma ni mwanamke ambaye nimeoa aje anisaidie maisha ndo anakuja nishusha,mwanamke ninayemshirikisha kila kitu ndo anakuja kuwa adui yangu,nimemaliza mkataba na ndo hapo hapo napokea taarifa km hiyo.Sina mtu wa kumshirikisha kitu maana wakumshirikisha ndo huyo kazingua.

Mda wote nawaza ukatili tu sasa kimtu chenyewe hataukipiga kofi vzr kinazima.Nssf nilikuwa na 27M.pssf nilikuwa na 11M.Nikasema nianze kule kwanza.

Changamoto nilikuwa nayo kipindi kile ni nawezaje kukaa nae chini kupanga nae maisha mwanamke wa namna hii na je maisha nitapanga na nani? Nawezaje kumfungulia Biashara mwanamke wa namna hii??Nani nitaongea nae stress zangu za maisha?Nani atanifariji pale Mambo yakuwa yakienda mrama?Nani anayenionea huruma kama sio mke wangu?Kifupi alinitisha sana sababu niliamini nipo salama halafu nikagundua nahitaji kuwa makini maana sio kweli kwamba nipo salama.

Huyu mwanamke sijawahi kuprove kunisaliti na ana heshima kiasi chake nadhani hapo ndo alipoponea,mi nilikuwa willing kuvunja ndoa ila hivyo vitu viwili ndo deal breaker kwangu basi nikapata mafao nikaweka sehemu kazaa nikawa naingiza 3M. Per month Maisha yakarudi sawa.

Sijawahi kumwambia ila Nikampa adhabu kuu mbili sitakaa nikufungulie biashara,sitakaa na wewe kujadili maendeleo ya familia,tupige story tucheke tule tulale ila my next move itakuwa siri yangu siku zote...

Kiukweli hili jambo lilinifanye nisiwazingatie kabisa wanawake, Mungu aliposema tuishi nao kwa akili alijua kabisa hawa watu hajawapa akili ya utambuzi,Sasa km mwanaume nae huna akili basi familia inakosa mwenye akili...
Duuuh hahahaaa nisamehe mkuu kwa kucheka ila hamna namna nimejikuta tu nacheka!!!
From 20M to 650k! Huyo kiboko!
 
DeepPond Man, you're extremely intelligent and great storyteller. Kudos.
Kama itakupendeza tufahamishe mkeo anamchukuliaje Mama J? Au kakubaliana na hali?
 
DeepPond Man, you're extremely intelligent and great storyteller. Kudos.
Kama itakupendeza tufahamishe mkeo anamchukuliaje Mama J? Au kakubaliana na hali?
Kwasasa
wife anajua nilishaachana na mamaJ MDA sana

Kuna kipind mamaJ alijichetua sana,
Anataka kuolewa kwa Lazima nikakataa,
Akaanzisha varangati ili kujitambulisha kusudi kwa wife kama mke wangu mdg,

Yaan mamaJ anamchokoza wife kusudi, Wife akareact wakarushiana Maneno Sn.
Sasa wife kujibizana sana hawezi,kapata depression mpk kalazwa hospitali.

Ikabd kumfata mamaj na kumuwasha makofi na kumpiga block Moja kwa Moja asinizoee. Ila

Sema maelezo yake marefu sn,
Uzi wake umo humu, miaka ya nyuma

hebu ngoja nikafukue ukaupitie kwny timeline




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Aseeehh ..pole mnooo!
Mdogo wangu anapewa na mmewe pesa almost mwezi mzima km 3m juzi kamuomba kampa 600k.... aseeehh nimemkunjaa sikujali ukubwa wake mmewe kaogopa kumpiga kanipigia simu ananiambia ntaua mimi dada(hua ananiita dada badala ya shemeji)nikaenda dar ghafla nimemzibua nimerudi niliko,na nimemuambia usimshirikishe chochote pesa weka benki
Wanawake tunafeli somewhere haswa hapo kutunza pesa za waume zetu
Na vitu kama hivi ndo unasikia mwanaume kafa,Mali zimepotea sijui marafki wamedhulumu yaani mambo kama haya..

Mwanamke anashindwa kujua umuhimu wake km mke matokeo yake mume anaogopa hata kumwambia siri za msingi
 
IKAFIKA KIPINDI
Akawa anakuja dukan anakaa chini na mtoto mgongoni kibarazani analia anaomba msamaha sn nimsamehe sn kwa yote aliyonikosea. Anaahidi atajirekebisha Ni shetani alimpitia.simjibu chochote akichoka kuomba msamaha anaondoka zake.

Kuna siku kashinda dukan asbh mpk saa 11 jioni na mtoto mgongoni anabembeleza. Mpk nafunga anabembeleza anabubujikwa na machozi, nilivofunga nikaenda nyumbani. Usiku kaja, kakuta geti halijafungwa kasukuma kaingia ndani na kwenda dirishan kwangu chumban analia anabembeleza nimsamehe. Nikamkaushia.

Kaenda Hadi dirisha la bi.mkubwa analia kakosa anaomba asamehewe.
Bi mkubwa nae akakausha Ila alivoondoka nikashangaa na asivompenda huruma ikamuingia nae akawa ananisihi nimsamehe turudiane. Nikamwambia bi.mkubwa achana nae uyo,hafai.

Tumeenda ukimya juu ya ukimya,
Wife akadili na mzee, kumbe akawa Anaenda kuomba msamaha ofsin kwa mzee. Mzee alipoona imekua kero akaniita na kunambia uyu mwanamke kila Mara anakwenda ofsn kwake kumuomba msamaha na anadai shangaz zake ndo waliomponza anajutia kilichotokea. Naonaje suala la kumsamehe. Nikasema mzee Mimi simtaki tena. Mzee akasema sawa Kama nmeamua hivyo. Ikaisha.

Baada ya miez 3 tangu Lile vurugu. naendelea na shughuli zangu nishaanza msahau wife, mzee akanambia jumapili tutakua na kikao Cha familia saa 10 mchana usichelewe kurudi uwepo. Nikasema sawa. Nikajua yatakua mambo ya familia yetu tu. Kweli Nmefika nyumbani mapema.

Gafla Niko chumban bi mkubwa kaja nigongea kua MDA tayar nije seblen.
Ile Natoka nafika seblen,nawaona wale shangazi zake wameketi, ikanibidi kurudi zangu chumbani na kukaa kitandani nikajiinamia kwa uchungu. Ikawa Kama wamenitonesha upya kile kidonda .

Mzee kaja kaniinua na kunambia twende seblen kila kitu kitakua sawa.
Kweli nmeinuka kinyonge nmeenda seblen nmekaa na mzee kochi Moja kubwa la Watu watatu.

Gafla shangaz Yao mmoja aliekua na mdomo akaja niangukia chonde chonde nimsamehe kwa yaliyopita.
Mzee akaniangalia usoni, nikaona mzee kama anatuma ujumbe kua anajiskia viby jins mmama yule mtu mzima anavolia. Wale wengine wakawa wanasema samahani yaishe yaishe. Babamkwe nae akasema imefkia mahali wife mpk anataka kujiua nyumbani kwao, alishameza hadi vidonge Mara mbili kajifungia chumbani anataka kujiua yye na mtoto. Wakavunja mlango kumnusuru.

Kama familia wanaomba radhi, wametukosea Sana, wanaomba radhi Sana. Anawasiwasi wanakoelekea atampoteza binti Yake na mjukuu wake, binti yake anazurula kila siku mjini na mtoto mgongoni anasema anaaga kaja kuomba msamaha na hasamehewi na kichwa chake kishachanganyikiwa sahv kilivyo tusije kushangaa kagongwa na Gari yeye na mtoto wote wamefariki. Mzee kaniangalia usoni.

Sijakaa sawa, kumbe wife alijificha jikoni nae kaja analia Hadi kamasi macho yamevimba na mtoto wake mgongoni kaniinamia anaomba msamaha. Mzee kaniangalia Tena usoni Tena na kunipa ishara ya nimsamehe. Nikatikisa kichwa kukubali.

Mzee kamuinua wife na kumkalisha kushoto kwake, Mimi kulia kwake.
Akasema kua Hawa wote Ni wanangu. Nyie wote nendeni kila kitu kitakua sawa. Basi wageni wale wakatawanyika.

Tukabaki familia yetu, wife na mtt. nikawa ndani ya siku 2 simuongeleshi.
Bi mkubwa akanisihi yaishe niongee na mzazi mwenzangu, mzee nae akanisihi yaishe bhana. Basi siku ya 3 wife kaja chumbn kwangu kavaa kimitego analia anaomba msamaha.
Kwasababu moyoni nishamsamhe na nilivommiss siku nyng sijapiga show.
Basi ugomvi wetu ukaishia pale.

Baada ya wiki pale home,
Mzee akatutaftia nyumba nyingine kubwa zaidi na kutupangishia kua tukakae uko pale kwa wapangaji tuhame. Alivotupeleka kule tunakutana na vile vitu vyetu tulivosomba na canter vipo vimerundikwa TU sebleni. Wife akaanza kuvipanga upya na maisha yakarejea Kama zamani.

TANGU HAPO miaka mingi imepita na WIFE HAJAWAI TENA KUTAMKA KAULI ILE YA TUGAWANE MALI.

Na pia,
Tangu ugomvi huo alirudi kua mama wa nyumbani na Hadi leo hii nnapoleta Uzi huu hajawai tena kuuza duka langu lolote.

Pia,
Nilikata mguu kabisa na magomeni kule kwa mashangazi waswahili wale.
Japo wanadai ugomvi ulishaisha ila nmekua karibu na ndugu wa wife kule upande wa mama ake na upande wa baba ake, Maelewano mazur Nmebaki na baba mkwe wangu TU. wengine ni salamu TU,kila mtu kivyake.

Nihitimishe kwamba
kile kipind kilipita na kilikua Cha mafunzo sn kwetu kutukomaza na Siwez kumhukumu sn wife maana umri wake ulkua bado mdogo sn, afu mazingira ya uswahili alikokulia kwa mashangazi wale yalimharibu.
Nashkuru upande wa mama ake walinisaidia sn kumshape wife akatulia akawa mcha mungu na MKE mzur Sana.[emoji1431]

Kwasasa
MKE wangu kiumri na kitabia amekua sana. Naweza kusema Ni MKE bora kabisa maishani, naeweza kukaa mbele ya Wanaume wenzangu waliooa nami nakajivunia kua Nmeoa mke bora kabisa na pure wife material mama wa watoto wangu[emoji4]

Na huwa nawaza Sijui ningekaza ningempoteza kipind kile sijui ingekuaje maisha yangu, maana kila nnakogusa Ni chenga tupu. Michepuko wote nilonao, vichwa maji tupu, mamaJ inclusive.

KINGINE,
Najivunia Sana baba mkwe wangu nilie nae, Ni mkwe asiyependa mambo ya kipuuzi kabisa na alisaisaidia Sana kumshape wife miaka 5 ya changamoto ya ndoa yangu.[emoji1431]

SIKU NIKITULIA NTASHUSHA TENA KISA kingine KILICHONIFANYA NIJIVUNIE HUYU BABA MKWE WANGU KATIKA KUMNYOOSHA WIFE WANGU[emoji4]

ASANTENI SANA WAKUU[emoji1431]
#######mwisho######

NB:
Kuna la kujifunza Hapa wakuu
Uzi huu nmeuleta baada ya kuguswa na Uzi wa mdau mmoja mwenye kisa Kama changu, ugomvi wa kibiashara na mkewe, Kisha mkewe akadai talaka wagawane Mali.

NAWASILISHA[emoji1431]
Big up brother, hakika kisa chako kinafundisha mno, japo ulimkazia sana my wife wako.
 
Nipo hapa napiga balimi ila hizo story zako zimenitoa[emoji25], sijui kwanini
 
Na vitu kama hivi ndo unasikia mwanaume kafa,Mali zimepotea sijui marafki wamedhulumu yaani mambo kama haya..

Mwanamke anashindwa kujua umuhimu wake km mke matokeo yake mume anaogopa hata kumwambia siri za msingi
Kabisaa yaani wanawake sometimes tunaharibu wenyewe last year ndugu wa ukoo tumezika alikua mhasibu kanisani akakabidhiwa 7m na mchungaji akafika nyumbani hakupeleka benki siku akampa mkewe ahifadhi maana Kuna ujenzi unaendelea church,siku hyo anaambiwa ma mchungaji tuletee mzigo j2 tuendelee anafika home anamuambia mkewe naomba zile fedha ,daaahhhh ,mke Hana Hata sh.kumi zote hazijulikani zilipo mwanaume akkaanza kufoka watoto wakawa wanaskia ule mzozo anamuambia pesa za kanisa hizo ntasema Nini Mimi analalamika ghafla kafika sebuleni Yuko watoto wanashangaa dingi kadondoka kafa on the spot!!!it was sad moment na watoto ndo walisimulia Hali ilivyo
So wanawake sisi tuna shida Sana
 
Kabisaa yaani wanawake sometimes tunaharibu wenyewe last year ndugu wa ukoo tumezika alikua mhasibu kanisani akakabidhiwa 7m na mchungaji akafika nyumbani hakupeleka benki siku akampa mkewe ahifadhi maana Kuna ujenzi unaendelea church,siku hyo anaambiwa ma mchungaji tuletee mzigo j2 tuendelee anafika home anamuambia mkewe naomba zile fedha ,daaahhhh ,mke Hana Hata sh.kumi zote hazijulikani zilipo mwanaume akkaanza kufoka watoto wakawa wanaskia ule mzozo anamuambia pesa za kanisa hizo ntasema Nini Mimi analalamika ghafla kafika sebuleni Yuko watoto wanashangaa dingi kadondoka kafa on the spot!!!it was sad moment na watoto ndo walisimulia Hali ilivyo
So wanawake sisi tuna shida Sana
 Masikini...
Huyo dada atajuta maisha yake uote!!

Au labda kuna wake ambao huhisi hela zitaishia kwa michepuko ndio maana huamua kuzifuja.
 
Back
Top Bottom