Mke amehama chumba tulichokuwa tukilala pamoja

Mke amehama chumba tulichokuwa tukilala pamoja

delako

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2012
Posts
2,902
Reaction score
1,875
Habari wakuu,

Naombeni ushuri maana ni week ya tatu sasa toka mke wangu amehama chumba chetu na kuhamia kwa watoto.

Sababu ya yeye kuhama ni kutokuelewana ambako binafsi naamini ni kwa kawaida ndani ya nyumba

Ni mke wangu wa NDOA ya kanisani kabisa na kwa kuwa naye ananishughulisha basi hata ananunua vyakula vyake na akifika hata kama kuna chakula hali ndani

Toka hiyo kutokuelewana hata kuongea hatuongei zaidi ya Mimi kuongea na watoto au yeye kufanya hivyo pia

Naombeni ushauri wa nini naweza kukifanya ili yeye arudi chumbani au asepe kabisa nijue moja.

Tumeishi wote kwa miaka 12 sasa na tumepata watoto watatu
 
Fanya mpango apate atoke chumba cha watoto aende cha wageni. Zamani ilikuwa ndio kawaida. Ebu ichukulie positive.

Jaribuni kuendelea hivyohivyi kwa siku tisini miezi 3

Tena mfuate mwambie mke wangu naona hii staili mpya tuijaribu labda itawafaa.

Siku ukiwa na hamu naye unamfuata chumbani kwake, akiwa na hamu na wewe atakufuata kwako nayo ni maisha tu.

Miaka ya zamani kuwa na chumba chako, kitanda chako ilikuwa ndiyo dalili ya kwanza ya utajiri
 
Aidha umemkosea na amekwazika sana mkuu, muache hadi hasira zake zitakapokwisha zenyewe. Kidonda au maumivu yanachukua muda kupona.

Jiepushe na fikra ngumu au fikra hasi pia chukulia kwamba kila mmoja yupo likizo. Mambo yatakaa sawa tu mkuu ondoa wasiwasi.
 
Ondoka na vielelezo muhimu mwachie nyumba wewe kaishi mkoa mwingineee ama kwingine. Mahitaji muhimu hakikisha unayatuma kwake. Toa taarifa kwa wahusika wenu pande zote.
Katafte mahali ujitafakari huenda wewe ndo tatizo if yes jirudii if no msamehe saka helaaa huenda kakumbuka old x
 
Ni mke wangu wa NDOA ya kanisani kabisa na kwa kuwa naye ananishughulisha basi hata ananunua vyakula vyake na akifika hata kama kuna chakula Hari ndani

Toka hyo kutokuelewana hata kuongea hatuongei zaid ya Mimi kuongea na watoto au yeye kufanya hivyo pia
  1. Mna umri gani
  2. Ndoa yenu ina muda gani
  3. Mna watoto wangapi
  4. Asili yenu mikoa gani
  5. Elimu yako na mkeo ni kiasi gani
  6. Kipato chako na chake vinatofautiana kiasi gani
  7. Mnaishi mjini au kijijini
  8. Je mnashika nafasi gani za kiuongozi kanisani kwenu
Tuanzie hapo
 
Ni mke wangu wa NDOA ya kanisani kabisa na kwa kuwa naye anajishughulisha basi hata ananunua vyakula vyake na akifika hata kama kuna chakula hali ndani
ANGALIZO: Under normal circumstance, hiyo huwa ni hatua ya Mwisho mwanamke hupitia kabla hajaenda kugongwa nje.

Mkuu hio ni ishara kuwa wewe ndio MKOSAJI, so anatumia hio kama Adhabu. vilevile umeshindwa kumuongoza MKEO (Unamuogopa).

Unapaswa kukemea tabia ya yeye kutokula nyumbani iishe mara moja, bila kujalisha kama wewe ndio umekosea au lah! Solve your problems like a Man. Baba Mkwe aliamini unaweza kumuongoza Binti yake. USIMUANGUSHE.

Be a Man, Focus na ishu za msingi za kifamilia na timiza wajibu wako kama Baba.
 
Back
Top Bottom