Mke amehama chumba tulichokuwa tukilala pamoja

Wakwako tu huyo, kusanya vifaranga weekend peleka kwa bibi jumapili kawachukue. Mtoe mkeo out moja matata, ikiwezekana mkalale nje somewhere romantic.. mbembeleze, muombe msamaha hata wa uongo. Unamjua kuliko sisi wanajamvi.
 
Kuna mpuuzi huko ashamshika mapembe! Kwa kifupi unato-mbewa huko nje....Hapo anataka uhuru ili awe huru zaidi na mtu wake.....Mpe akitakacho kabla hajakuletea ukimwi.
 
Daah sasa hapo mnawafundisha nn watoto? Ni aibu emu jitathiminini muyatatue matatzo yenu hapo tunashindwa kukushaur bcz haujatupa kisa mpka kutokea hio hali na pia lazma tusikilize pande zote mbili. JITATHIMININI!!!!!!!
 
Aisee kweli wanaume tumetofautiana sana, yaani mimi nilivyo wife hata nimkosee kwa kiwango gani, siku akifanya huo ujinga kwamba akalale kwa watoto wiki tatu na anakula anakokujua, mlango alioingilia ndio atakaotokea kurudi alikotoka. Hili kwangu analijua na hata siku moja hawezi kujitikisia kiberiti
 
Duuuh miaka kumi na mbili bado ujamjua Vizuri mke wako hadi unakuja uku kuomba ushauri 😴😴

Bora kuishi na sheteni unaye mjua kuliko malaika usie mfaham
 
endelea kua boya bro mkeo ana maamuzi juu ya nyumba yako for real na ikumbukwe bado sijaoa ila sizani kama mke anaeza hama chumba changu eti kisa 🤣🤣my people I'm not ready for marriage
 
Kaka watoto zako ndio ndugu zako.
Mke ni rafiki na unajua siku zote urafiki unaweza ukafa muda wowote na kupata rafiki mwingine wa kukufariji na kukusaidia.

Watoto zako ndio ndugu zako lakini kama unauhakika hao ni watoto wako pia.
 
Ningekuwa mimi ndio mume,ningemwambia kuhamia kwa watoto ni kunivunjia heshima mbele ya wanangu,ni bora akaenda kwao kwanza kama ana hasira sana
 
Aisee mbona wakongwe kabisa?

Kaa chini na wife mzungumze.

Mazungumzo yenu ndio yataamua kuishi pamoja au kuachana.

Zungumzeni.
 
Wakwako tu huyo, kusanya vifaranga weekend peleka kwa bibi jumapili kawachukue. Mtoe mkeo out moja matata, ikiwezekana mkalale nje somewhere romantic.. mbembeleze, muombe msamaha hata wa uongo. Unamjua kuliko sisi wanajamvi.
Wangu hakuna out utakayompeleka akaenda bila kusettle dispute kwanza.

Hajui kabisa kupandisha furaha kama kuna kesi
 
Kapange chumba sehemu kwa muda atanyoosha maelezo alafu utampa utaratibu unaoutaka alafu wanaume sikuhizi tumekua wapole hizi ndio adhari za kuwategemea wanawake kiuchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…