Mke anaruhusiwa kukopa fedha kama mume hatunzi familia

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 imeruhusu mke akope fedha anunue mahitaji ya familia kama mumewe hatoi fedha za matumizi.

Kifungu cha 64 (1) cha sheria hiyo kinasema mke ana haki ya kukopa fedha kwa ajili ya matumizi ya kuhudumia familia kwa jina la mumewe na mume ana wajibu wa kulipa deni hilo.

Pia, sheria hiyo imeweka wazi kuwa mke ana haki ya kutumia fedha za mume wake zilizo mikononi mwake au kubadilisha mali inayohamishika ya mume kuwa fedha na kutumia fedha hizo.

Wakili wa Ofisi ya Mawakili wa Kujitegemea ya Avis Legal, Henry Mwinuka alilieleza HabariLEO kuwa ikitokea mume bila sababu za msingi akaacha kuhudumia familia yake mke ana haki ya kuchukua mkopo kwa ajili ya kuhudumia familia tu na kwa kiwango ambacho fedha hizo zinahitajika kununua mahitaji muhimu kwa ajili yake na watoto wadogo wa ndoa yanayolingana na uwezo wa kifedha na mtindo wa maisha wa mume wake.

Mwinuka alisema kama mwanamke ataingia kwenye ndoa na madeni ya mkopo basi madeni hayo hayatahesabika kama madeni ya mume wake bali ni madeni yake mwenyewe.
“Ikiwa mwanaume hahudumii na hana sababu ya msingi ya kutohudumia mke na watoto mke anaweza kwenda kukopa kwa jina la mume na deni hilo litachukulia kuwa ni la mwanaume na atapaswa kulilipa,” alisema.

Aliongeza: “Madeni yale ambayo mwanamke ameingia nayo kwenye ndoa hayo mwanaume hayamuhusu yaani madeni yako ni yako haliwezi kuwa deni la mume wako”.

Chanzo: Habari Leo
 
Daah wanaume tumekabiwa juu kila mahali.

Mifumo yote imewekwa kutunyonya mpaka tufe mapema kwa stress.

Kwa sasa ninawaheshimu wanaume wote wanaoficha sehemu ya mali zao kusikojulikana kwa ajili ya usitawi wao binafsi huko mbeleni endapo watatendwa isivyofaa.
 
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 imeruhusu mke akope fedha anunue mahitaji ya familia kama mumewe hatoi fedha za matumizi.

Kifungu cha 64 (1) cha sheria hiyo kinasema mke ana haki ya kukopa fedha kwa ajili ya matumizi ya kuhudumia familia kwa jina la mumewe na mume ana wajibu wa kulipa deni hilo.

Pia, sheria hiyo imeweka wazi kuwa mke ana haki ya kutumia fedha za mume wake zilizo mikononi mwake au kubadilisha mali inayohamishika ya mume kuwa fedha na kutumia fedha hizo.

Wakili wa Ofisi ya Mawakili wa Kujitegemea ya Avis Legal, Henry Mwinuka alilieleza HabariLEO kuwa ikitokea mume bila sababu za msingi akaacha kuhudumia familia yake mke ana haki ya kuchukua mkopo kwa ajili ya kuhudumia familia tu na kwa kiwango ambacho fedha hizo zinahitajika kununua mahitaji muhimu kwa ajili yake na watoto wadogo wa ndoa yanayolingana na uwezo wa kifedha na mtindo wa maisha wa mume wake.

Mwinuka alisema kama mwanamke ataingia kwenye ndoa na madeni ya mkopo basi madeni hayo hayatahesabika kama madeni ya mume wake bali ni madeni yake mwenyewe.
“Ikiwa mwanaume hahudumii na hana sababu ya msingi ya kutohudumia mke na watoto mke anaweza kwenda kukopa kwa jina la mume na deni hilo litachukulia kuwa ni la mwanaume na atapaswa kulilipa,” alisema.

Aliongeza: “Madeni yale ambayo mwanamke ameingia nayo kwenye ndoa hayo mwanaume hayamuhusu yaani madeni yako ni yako haliwezi kuwa deni la mume wako”.

Chanzo: Habari Leo
Hakika HIZI Ndoa kweli ni NDOANO!
 
Sheria ya Ndoa ya Mwaka 1971 imeruhusu mke akope fedha anunue mahitaji ya familia kama mumewe hatoi fedha za matumizi.

Kifungu cha 64 (1) cha sheria hiyo kinasema mke ana haki ya kukopa fedha kwa ajili ya matumizi ya kuhudumia familia kwa jina la mumewe na mume ana wajibu wa kulipa deni hilo.

Pia, sheria hiyo imeweka wazi kuwa mke ana haki ya kutumia fedha za mume wake zilizo mikononi mwake au kubadilisha mali inayohamishika ya mume kuwa fedha na kutumia fedha hizo.View attachment 3699407 Wakili wa Ofisi ya Mawakili wa Kujitegemea ya Avis Legal, Henry Mwinuka alilieleza kuwa ikitokea mume bila sababu za msingi akaacha kuhudumia familia yake mke ana haki ya kuchukua mkopo kwa ajili ya kuhudumia familia tu na kwa kiwango ambacho fedha hizo zinahitajika kununua mahitaji muhimu kwa ajili yake na watoto wadogo wa ndoa yanayolingana na uwezo wa kifedha na mtindo wa maisha wa mume wake.

Mwinuka alisema kama mwanamke ataingia kwenye ndoa na madeni ya mkopo basi madeni hayo hayatahesabika kama madeni ya mume wake bali ni madeni yake mwenyewe. “Ikiwa mwanaume hahudumii na hana sababu ya msingi ya kutohudumia mke na watoto mke anaweza kwenda kukopa kwa jina la mume na deni hilo litachukulia kuwa ni la mwanaume na atapaswa kulilipa,” alisema.
Aliongezea “Madeni yale ambayo mwanamke ameingia nayo kwenye ndoa hayo mwanaume hayamuhusu yaani madeni yako ni yako haliwezi kuwa deni la mume wako”.
Mwisho akasema sheria hiyo inatambua mali za wanandoa kama mali zote zilizopatikana kihalali ikiwemo nyumba, shamba, magari, kiwanja, kampuni, biashara na mali nyinginezo

Source; Habari Leo
Sheria ya ndoa hapa nchini haiendani na uhalisia wa nyakati za sasa
 
Mnadhidi kuwaponza hao viumbe wauliwe! Kutakuwa na uthibitisho gani kuProve kama apewi huduma ye na watoto? maana wasije kutumia mwanya wa hiyo sheria iliyotungwa na midume bwege kutaka kuwatiwa madeni waume zao and then ilete
 
Back
Top Bottom