Kuna jamaa yangu mmoja ana mke na watoto 2. Jamaa anafanya kazi Mashirika ya U.N so mara nyingi anasafiri mikoani kwa ukaguzi wa miradi. Nyumbani kwa jamaa na kwa wakwe zake ni umbali wa dakika 20 kwa Dala Dala. Sasa jamaa anaposafiri tuu huku nyuma mke anabeba watoto anaenda kukaa nyumbani kwako bila taarifa kwa jamaa.
Hiyo hali iliendelea zaidi ya miaka 3 bila jamaa kujua. Kuna siku jamaa alikuwa Bar fulani maeneo ya karibu na kwa wakwe akakutana na mshkaji wake wa kitambo ambao hawajaonana muda mrefu na ambae pia ni jirani kwa wakwe zake,baada ya salamu jamaa akamuuliza mshkaji vipi mnamgogoro na shemeji? Jamaa akasema hapana,kwanini, jamaa akamwambia mbona namuona kama karudi kwao muda mrefu namuona pale hata Dada zake wengine waliolewa wamerudi. Jamaa akazuga pale kujibu lakini akilini akishangaa hizi taarifa.
Baadae jamaa akafanya uchunguzi na kubaini ni kweli mke wake anatokaga akisafiri,akamuweka chini akamwambia mke akakiri na kusema hatarudia tena. Lakini jamaa akiondoka mke anarudia tena mchezo wake. Jamaa aliponiambia kuomba ushauri nikamwambia cha kufanya wewe zusha safari ya uongo then urudi ghafla,kweli akafanya hivyo akarudi usiku akakuta nyumba imefungwa,nikamwambia sasa asubuhi nenda kwao ukamwambie mbele ya wazazi wake aendelee kukaa hapo mpaka atakapomwambia arudi yeye. Kweli mke alikaa kwao miezi mitatu,kila jamaa akiombwa msamaha kakaza,hadi leo mke akili zimemkaa.