Mke kwenda kushinda kwao hadi jioni na kurudi na chakula kilichopikwa ukweni, nisawa mume kula hicho chakula?

Mke kwenda kushinda kwao hadi jioni na kurudi na chakula kilichopikwa ukweni, nisawa mume kula hicho chakula?

Mkuu deal na huku kwanza utatue, wanawake wana mambo mengi
Mkuu huko kunaniumiza kichwa Sana nadeal nako kutatua changamoto hiyo
 
Kuna jamaa yangu mmoja ana mke na watoto 2. Jamaa anafanya kazi Mashirika ya U.N so mara nyingi anasafiri mikoani kwa ukaguzi wa miradi. Nyumbani kwa jamaa na kwa wakwe zake ni umbali wa dakika 20 kwa Dala Dala. Sasa jamaa anaposafiri tuu huku nyuma mke anabeba watoto anaenda kukaa nyumbani kwako bila taarifa kwa jamaa.

Hiyo hali iliendelea zaidi ya miaka 3 bila jamaa kujua. Kuna siku jamaa alikuwa Bar fulani maeneo ya karibu na kwa wakwe akakutana na mshkaji wake wa kitambo ambao hawajaonana muda mrefu na ambae pia ni jirani kwa wakwe zake,baada ya salamu jamaa akamuuliza mshkaji vipi mnamgogoro na shemeji? Jamaa akasema hapana,kwanini, jamaa akamwambia mbona namuona kama karudi kwao muda mrefu namuona pale hata Dada zake wengine waliolewa wamerudi. Jamaa akazuga pale kujibu lakini akilini akishangaa hizi taarifa.

Baadae jamaa akafanya uchunguzi na kubaini ni kweli mke wake anatokaga akisafiri,akamuweka chini akamwambia mke akakiri na kusema hatarudia tena. Lakini jamaa akiondoka mke anarudia tena mchezo wake. Jamaa aliponiambia kuomba ushauri nikamwambia cha kufanya wewe zusha safari ya uongo then urudi ghafla,kweli akafanya hivyo akarudi usiku akakuta nyumba imefungwa,nikamwambia sasa asubuhi nenda kwao ukamwambie mbele ya wazazi wake aendelee kukaa hapo mpaka atakapomwambia arudi yeye. Kweli mke alikaa kwao miezi mitatu,kila jamaa akiombwa msamaha kakaza,hadi leo mke akili zimemkaa.
 
Nilimruhusu kwenda shinda kwao kwa maana yakwamba asubuh nimetoka nimekula full ntakula usiku home so maana yake ye aje awahi jioni apike chakula Cha jioni chakula mumewe Sasa kwa akili zake ndio kaja nachakula badala yakuwahi kuja pika
Kumbe huu ujinga umeuanza wewe,utamruhusu vipi mke wako akashinde kwao halafu jioni arudi kwako?
 
Kama unamwamini mke wako ni sawa

Kuna vitu bro potezea wanawake karibu wote wana tabia hizo

Akienda kwenye sherehe km inamuhusu lazima arudi mara na cake mara na kuku,vinywaji.

Itoshe kusema ni tabia za kike zisizo na madhara sana kwenye mahusiano.

Au mama yake mchawi unaogopa limbwata???
Hizi ni akili za Wavulana na si Mwanaume anaejitambua kiakili na maamuzi.
 
Mkuu,inawezakana akienda kwao yeye ndo anapika.

Sasa ameona afanye kazi iwe rahisi,anapika chakula kingi ili kingine aje nacho nyumbani mle.

Hapo sijaona shida yoyote,mbona nikitu kidogo sana,hebu muhurumie kidogo mkeo
Hakuna ujinga kama huo.
 
Watoto 2 hawako wako shule so anamtoto wa mgongoni tu kwasasa..amepata tatizo lamsiba kwao ndani ya hizi wiki tatu Sasa huwa anakwenda kuwajulia Hali nakushinda huko ktkt kipindi hiki Sasa ndio Mara mbili kaja nachakula kilichopikwa huko kwao kuja nacho jion SAA kumi namoja
Kumbe ni x2 tu!!? Vip ulishawai kumwambia kuwa upendi hio tabia?
 
Kama anakupa Mbususu bila tatizo basi we kula msosi huo
 
Acha gubu na wewe mara mbili tu kimbuka anamtoto mgongoni unafikiri yeye hachoki basi mwambie wewe kwa siku hizi utakuwa unapika wewe
Yani hili ni gubu live[emoji1787][emoji1787][emoji1787]mna watoto watatu na hujawahi ona hivi, inamaana ni suala la muda matatizo yakiisha atarudi kwenye hali yake, sometimes wanaume mtuoneage huruma tunachokaga na kazi plus kulea
 
huko ni kukosa heshima kwa mumewe yeye kama mke anatakiwa kutambua jukumu lake.... sio sawa wewe kula hivyo vyakula maana ni sawa nakulishwa viporo.
CHUKUA MAAMUZI KAMA MWANAUME
 
Kuna jamaa yangu mmoja ana mke na watoto 2. Jamaa anafanya kazi Mashirika ya U.N so mara nyingi anasafiri mikoani kwa ukaguzi wa miradi. Nyumbani kwa jamaa na kwa wakwe zake ni umbali wa dakika 20 kwa Dala Dala. Sasa jamaa anaposafiri tuu huku nyuma mke anabeba watoto anaenda kukaa nyumbani kwako bila taarifa kwa jamaa.

Hiyo hali iliendelea zaidi ya miaka 3 bila jamaa kujua. Kuna siku jamaa alikuwa Bar fulani maeneo ya karibu na kwa wakwe akakutana na mshkaji wake wa kitambo ambao hawajaonana muda mrefu na ambae pia ni jirani kwa wakwe zake,baada ya salamu jamaa akamuuliza mshkaji vipi mnamgogoro na shemeji? Jamaa akasema hapana,kwanini, jamaa akamwambia mbona namuona kama karudi kwao muda mrefu namuona pale hata Dada zake wengine waliolewa wamerudi. Jamaa akazuga pale kujibu lakini akilini akishangaa hizi taarifa.

Baadae jamaa akafanya uchunguzi na kubaini ni kweli mke wake anatokaga akisafiri,akamuweka chini akamwambia mke akakiri na kusema hatarudia tena. Lakini jamaa akiondoka mke anarudia tena mchezo wake. Jamaa aliponiambia kuomba ushauri nikamwambia cha kufanya wewe zusha safari ya uongo then urudi ghafla,kweli akafanya hivyo akarudi usiku akakuta nyumba imefungwa,nikamwambia sasa asubuhi nenda kwao ukamwambie mbele ya wazazi wake aendelee kukaa hapo mpaka atakapomwambia arudi yeye. Kweli mke alikaa kwao miezi mitatu,kila jamaa akiombwa msamaha kakaza,hadi leo mke akili zimemkaa.
Labda ilikua upweke jamani . Dah!
Ingeku anaenda kwa mchepuko hapo sawa.
 
Kama ni kwa kipindi hiki ambacho kwao kuna changamoto, Basi ni sawa, lakini ikiwa kila wakati hata wakati ambapo hakuna sababu ya msingi ya kufanya hivyo, Basi kuuziwa mbuzi kwenye gunia kunahusika.
 
kula msosi, acha kutafuta justification kwenye mambo ya kipuuzi.

kama yeye anakula chakula hicho hicho amna shida hapo.
 
Back
Top Bottom