Mke mwema anatoka kwa Bwana sasa kwanini asiwe na bikira yake?

Sawa kwahiyo ukimkuta mke wa mtu ana vigezo vyote hivyo kasoro bikra anakuwa sio mke mwema tena na anatoka kuzimu au?
Sasa mke wa mtu atakuwa na bikira vipi? Mwanamke anakuwa bikra kabla hajaanza mapenzi akianza ngono tu bikra hutolewa na mara1.

Akiwa hana bikira maana yake amekosa sifa za mke mwema mke mwema fani mdangaji?

Kuhusu kutoka kuzima kama unaamini hivyo siwezi kukupangia mimi naamini anatoka kwenye familia isiyo na malezi thabiti.
 
kwani biblia imekwambia mke mwema ni lazima awe na bikra?
Ndio ndo kigezo cha mke mwema.

“mke mwema anatoka kwa Bwana” ina maana kwamba mke mzuri (mwenye tabia njema, upendo, heshima na hekima pia aliyejitunza) ni baraka kutoka kwa Mungu, si kitu kinachopatikana tu kwa juhudi za kibinadamu pekee.

Hii kwa mjibu wa andiko la mithali 31
 
Kwenye hiyo mithali 31 kuna neno bikra limetajwa? mbona unataka kulazimisha?
 
Hiyo ni tafisiri yangu ya maana mke mwema. Daima mungu alivyo mwema hawezi kukupa used kama kweli unaamini kwenye hilo andiko
tafsiri yako sio biblia. Mada zako huwa zina walakini sana na huwa unatafuta trend tu mtandaoni. Kama biblia imeruhusu mwanamke mjane au aliyeachika aolewe sembuse binti asiye na bikra? Jamaa yangu naomba uachane na mambo ya kuhoji imani za watu,tafuta mada zingine fikrishi.
 
Ndiyo, kasome waebrania 13:4, na pia kuna mifano kama kumbukumbu la Torati 22:13–21 inayoonesha uzito uliowekwa kwenye ubikira kwa mwanamke.
Mkuu nataka twende taratibu, mtu alikuwa mzinzi amefikisha miaka 20 akaamua kuokoa,kuokoka maana yake akaokolewa,akawa safi,akaacha uzinzi akawa mtu wa Bwana,je huyo nae hataolewa kisa hana bikra ili hali Bwana amemkubali na akawa wa Bwana? shida mnatafsiri vibaya Biblia. Nikifa MkeWangu Asiolewe
 
Mtoa mada yupo na point asipuuzwe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…