JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mesoni Kashiro (15) Mkazi wa kijiji cha Gelailumbwa, kata ya Gelailumbwa, tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido mkoani Arusha, ameshambuliwa na mume wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.
Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani hapa, Atunagile Chisunga akieleza kuwa watuhumiwa wapo kituo cha polisi Longido na hapo kesho wanatarajia kufikishwa mahakamani huku akisistiza mama huyo yupo kituo cha afya Longido akiendelea kupatiwa matibabu zaidi.
"Huu ni ukatili kabisa kwanza ameolewa akiwa na umri mdogo, wamempiga wakiwa wamemfunga kamba na kumtundika kwenye miti," alidai Chisunga.
Chanzo: Dira
================
Namendea Lesiria, Mkazi wa Kijiji cha Gelailumbwa, Tarafa ya Ketumbeine Wilayani Longido Mkoani Arusha anatuhumiwa kwa kumshambulia mkewe mwenye umri wa miaka 15 na kumsababishia majeraha makubwa.
Namendea anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kushirikiana na rafiki yake chanzo kikitajwa ni binti huyo kumwaga dawa ya mifugo (mbuzi).
Ofisa Ustawi wa Jamii wa Longido, Atunagile Chisunga amesema “Watuhumiwa watapandishwa Mahakamani Septemba 23, 2022, pia mama wa binti tunamshikilia kwa kumkeketa mwathirika.”