Mke mwenye miaka 15 aumizwa vibaya na mume kisa kumwaga dawa ya mbuzi

Mke mwenye miaka 15 aumizwa vibaya na mume kisa kumwaga dawa ya mbuzi

Sina ufahamu wa sheria kama wewe. Swali langu ni kwanini wahanga wengi ni wale walio tembea na wanafunzi chini ya miaka 18 na si waliooa chini ya miaka 18?
Wewe binafsi nna uhakika umeona ndoa hizo nyingi tu na zipo wazi. Inamaana jamaa alitongoza na akakubaliwa na akaamua kufunga nae ndoa. Pia kwa wanafunzi ni hivyo hivyo, alitongoza akakubaliwa wa kafanya yao.
JE unamaamisha kama mwanafunzi alimkubali "kwa ridhaa yake" jamaa amtafune, jela haita muhusu??
Huwenda nikapata kufahamu mengi kupitia wewe
... "ndoa" za under 18 zinapatikana zaidi katika maeneo ya vijijini tena vijiji ambavyo uelewa hususan wa mambo ni mdogo hivyo ni nadra kuripotiwa katika vyombo husika ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Kwa upande wa wanafunzi ni rahisi kujulikana (japo sio wote) kwa sababu katika mazingira ya shule (wasomi) tabia na mwenendo wa mhusika vikibadilika ni rahisi kufuatiliwa na hata wenyewe hutajana. Pia, ikumbukwe wanafunzi wa kike hufanyiwa vipimo kuona hali zao; wajawazito hujulikana kirahisi katika mazingira ya aina hii.

Neno "ridhaa" kwa mwanafunzi (na under 18) ondoa; halipo litakuponza bure! Hayo makundi mbele ya sheria hayana ridhaa.
 
Sheria za Tanzania, ukioa mwenye miaka 15 na hasomi, hapo sawa. Ila ukifanya mapenzi na mwanafunzi wa kike mwenye miaka 15 unafungwa miaka 30 kwa ubakaji mtoto [emoji23]
Contradiction inaanzia kwenye sheria za ndoa za serikali, mila na kidini
 
Mesoni Kashiro (15) Mkazi wa kijiji cha Gelailumbwa, kata ya Gelailumbwa, tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido mkoani Arusha, ameshambuliwa na mume wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.

Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani hapa, Atunagile Chisunga akieleza kuwa watuhumiwa wapo kituo cha polisi Longido na hapo kesho wanatarajia kufikishwa mahakamani huku akisistiza mama huyo yupo kituo cha afya Longido akiendelea kupatiwa matibabu zaidi.

"Huu ni ukatili kabisa kwanza ameolewa akiwa na umri mdogo, wamempiga wakiwa wamemfunga kamba na kumtundika kwenye miti," alidai Chisunga.

Chanzo: Dira

================

Namendea Lesiria, Mkazi wa Kijiji cha Gelailumbwa, Tarafa ya Ketumbeine Wilayani Longido Mkoani Arusha anatuhumiwa kwa kumshambulia mkewe mwenye umri wa miaka 15 na kumsababishia majeraha makubwa.

Namendea anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kushirikiana na rafiki yake chanzo kikitajwa ni binti huyo kumwaga dawa ya mifugo (mbuzi).

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Longido, Atunagile Chisunga amesema “Watuhumiwa watapandishwa Mahakamani Septemba 23, 2022, pia mama wa binti tunamshikilia kwa kumkeketa mwathirika.”
Inasikitisha mnoo

Sent from my SM-A135F using JamiiForums mobile app
 
Violence Genes flow
Arusha jinsia zote wakatiri tu.
#Nasubiri kutukanwa🤣
 
... hiyo tafsiri yako. Sheria iko hivi; kumwingilia kimwili mwenye umri chini ya miaka 18; au kumwingilia kimwili mwanafunzi (hadi sekondari); au kumwingilia kimwili mwanamke bila ridhaa yake hayo yanaangukia katika kosa la ubakaji.

Makundi matatu yametajwa hapo (a) chini ya miaka 18 (b) mwanafunzi (c) mwanamke bila ridhaa.

Utaona neno "ridhaa" halijatumika kundi (a) na (b); hakuna kisingizio kwamba "alikubali mwenyewe" kwa sababu makundi hayo yanahesabiwa hayana ridhaa mbele ya sheria. Kundi (c) linawahusu wale wenye 18+. Katika mazingira ambayo mahakama itathibitisha ulifanya mapenzi na mwanamke bila yeye kuridhia mf. umemnywesha kilevi kisha ukamwingilia inaangukia katika ubakaji.

Kwa case ya thread hii, ikithibitishwa "mume" wa huyo "mke" aliwahi kumwingilia na kwa kuwa "mke" ana under 18 (i.e. 14/15), then, automatically, mbele ya sheria, amekuwa akimbaka. Hivyo 30 yrs in prison inamhusu.
Sheria ya ndoa ni miaka mingapi?
 
Kwani sheria ya MWAKA 1971 ya kwamba msichana anaweza kuolewa akiwa na miaka 15 kwa ruhusa ya wazazi ilifutwa?????.
 
Hao jamaa huko mbele wanaangalia nini? Au ameumizwa pia kwa upande wa mbele??
 
Miaka 15 si yuko form two?.mbona mdogo sana hata akili haijakua jamani. Ndo aje avumilie mateso yote mpk afikie umri wetu si mwili umekua na ramani wote au kufa kabisa
 
Yote hii ni tatizo la vijiji serikali kuwaachia watu wa huko waishi kama wanyama, semina, Sheria na kuwabadilishia mazingira kwa lazima Ili waondoke katika unyama na kuishi kama watu hata haya matukio yangejulikana kwa haraka, kingine huko vijijini imeonekana wanazaliana kama wanyama na watoto hawahesabiki watoto wa binadamu wanaopaswa kulelewa na kupewa elimu na malezi ni mwendo wa kuishi kama wanyama na kuonekana hawana umuhimu wowote wa kuandaliwa kuwa taifa la kesho lenye kujitambua hii nayo iangaliwe kama hawawezi uzazi wa mpango basi wafungwe vizazi baada ya watoto wanne kutumia Ili kuondoa haya maisha yao ya kinyama na hata hao watoto wakija mjini huwa wanatabia za kinyama kama wazazi wao kitu ambacho kitaharibu taifa la kesho, hapo tunaona ni mtoto wa kike na ndoa za utotoni na Hana uchumi wowote Wala elimu lakini hata mtoto wa kiume wa huko vijijini hapewi elimu zaidi nikufundishwa awe na nguvu kama mnyama kitu ambacho akija mjini anatumia hizo nguvu kuwa jambazi na huko kijijini nikuchapana kama wanyama na wakikuwa wanakuwa wanyama wazee.
 
Mesoni Kashiro (15) Mkazi wa kijiji cha Gelailumbwa, kata ya Gelailumbwa, tarafa ya Ketumbeine wilayani Longido mkoani Arusha, ameshambuliwa na mume wake Namendea Lesiria kwa kushirikiana na rafiki yake ambaye jina halijafahamika kwa kosa la kumwaga dawa ya mfugo aina ya mbuzi.

Ofisa Ustawi wa Jamii wilayani hapa, Atunagile Chisunga akieleza kuwa watuhumiwa wapo kituo cha polisi Longido na hapo kesho wanatarajia kufikishwa mahakamani huku akisistiza mama huyo yupo kituo cha afya Longido akiendelea kupatiwa matibabu zaidi.

"Huu ni ukatili kabisa kwanza ameolewa akiwa na umri mdogo, wamempiga wakiwa wamemfunga kamba na kumtundika kwenye miti," alidai Chisunga.

Chanzo: Dira

================

Namendea Lesiria, Mkazi wa Kijiji cha Gelailumbwa, Tarafa ya Ketumbeine Wilayani Longido Mkoani Arusha anatuhumiwa kwa kumshambulia mkewe mwenye umri wa miaka 15 na kumsababishia majeraha makubwa.

Namendea anadaiwa kutenda kosa hilo kwa kushirikiana na rafiki yake chanzo kikitajwa ni binti huyo kumwaga dawa ya mifugo (mbuzi).

Ofisa Ustawi wa Jamii wa Longido, Atunagile Chisunga amesema “Watuhumiwa watapandishwa Mahakamani Septemba 23, 2022, pia mama wa binti tunamshikilia kwa kumkeketa mwathirika.”
Ashtakiwe kwa kosa la unyanyasaji na kosa la kuoa katoto tena na wazazi wa bint washtakiwe.
 
Back
Top Bottom