Jabakeke
JF-Expert Member
- Apr 18, 2019
- 386
- 361
Tulioana miaka kadhaa iliyopita na tumejaaliwa watoto wawili. Tulioana mke wangu akiwa na mtoto mmoja aliyezaa akiwa kwao. Miaka ya mwanzoni uchumi uliruhusu kutoa huduma hata kwa mtoto wake ambaye anaishi na mjomba wake, baada ya uchumi kuyumba nikamwambia mwenzangu ongea na shangazi yake mtoto amwambie kaka yake aanze kumhudumia mtoto wake.
Nilifanya hivyo kwasababu sikutaka mke wangu awasiliane moja kwa moja na mzazi mwenzake, mke wangu akakataa akasema hawezi kufanya hivyo. Miezi kadhaa akaja akaniambia alishamtafuta mzazi mwenzake ila alimjibu vibaya, hivyo hana mpango wa kumtafuta tena na namba zake amefuta.
Nikamuuliza mbona nilikwambia umtafute dada yake ukakataa, ilikuwaje ukaanza kuwasiliana na mhusika moja kwa moja? Akajitetea yakaisha, lakini moyoni nikawa na mashaka. Ikabidi nianze kufanya uchunguzi kimya kimya nijue kinachoendelea,
Mungu sio mwanasiasa, kuna siku alikuwa ameenda shamba halafu akasahau simu nyumbani. Nikaanza kuipekua ndipo nikakuta simu ambazo yeye alikuwa akimtafuta mzazi mwenzake, pia nilikuta jumbe alizomtumia wifi yake akilalamika kwamba mzazi mwenzake hapokei simu, na baadaye jumbe ambazo zinaonyesha kwamba tayari wamewasiliana na jamaa na kakubali kwamba atakuwa anatoa hela za ada pamoja na mahitaji mengine.
Aliporudi nikamuuliza kwanini unarudia kosa lile lile mara ya pili, mimi ndiye niliyekupa ushauri halafu hutaki kunishirikisha kwanini? Je, nikisema unamtafuta kwa ajili ya usaliti nitakuwa nakosea? Kama kawaida yake akaanza kujitetea, lakini utetezi wake haukuiniingia moyoni, ikabidi nifanye maamuzi haya;
Nikamwambia hivi, "Sitolala na wewe bila kutumia condom usije ukaniletea maradhi, hawa watoto wawili wanatosha ukitaka mtoto kazae na huyohuyo mzazi mwenzako, na mimi nikitaka nitamfuta wa kuzaa naye".
Sasa yeye anadai namnyanyasa, namuonea kwasababu ana mtoto aliyezaa na mwanaume mwingine, na hataki kukubaliana na maamuzi yangu. Ila mpaka sasa wanaendelea kuwasiliana na mzazi mwenzake kuhusiana na masuala ya mtoto wao.
Je, nani mwenye kosa hapo, mimi au yeye?