Mke na mume tumeleta mashtaka kwenu

Mke na mume tumeleta mashtaka kwenu

Jabakeke

JF-Expert Member
Joined
Apr 18, 2019
Posts
386
Reaction score
361
Tulioana miaka kadhaa iliyopita na tumejaaliwa watoto wawili. Tulioana mke wangu akiwa na mtoto mmoja aliyezaa akiwa kwao. Miaka ya mwanzoni uchumi uliruhusu kutoa huduma hata kwa mtoto wake ambaye anaishi na mjomba wake, baada ya uchumi kuyumba nikamwambia mwenzangu ongea na shangazi yake mtoto amwambie kaka yake aanze kumhudumia mtoto wake.

Nilifanya hivyo kwasababu sikutaka mke wangu awasiliane moja kwa moja na mzazi mwenzake, mke wangu akakataa akasema hawezi kufanya hivyo. Miezi kadhaa akaja akaniambia alishamtafuta mzazi mwenzake ila alimjibu vibaya, hivyo hana mpango wa kumtafuta tena na namba zake amefuta.

Nikamuuliza mbona nilikwambia umtafute dada yake ukakataa, ilikuwaje ukaanza kuwasiliana na mhusika moja kwa moja? Akajitetea yakaisha, lakini moyoni nikawa na mashaka. Ikabidi nianze kufanya uchunguzi kimya kimya nijue kinachoendelea,

Mungu sio mwanasiasa, kuna siku alikuwa ameenda shamba halafu akasahau simu nyumbani. Nikaanza kuipekua ndipo nikakuta simu ambazo yeye alikuwa akimtafuta mzazi mwenzake, pia nilikuta jumbe alizomtumia wifi yake akilalamika kwamba mzazi mwenzake hapokei simu, na baadaye jumbe ambazo zinaonyesha kwamba tayari wamewasiliana na jamaa na kakubali kwamba atakuwa anatoa hela za ada pamoja na mahitaji mengine.

Aliporudi nikamuuliza kwanini unarudia kosa lile lile mara ya pili, mimi ndiye niliyekupa ushauri halafu hutaki kunishirikisha kwanini? Je, nikisema unamtafuta kwa ajili ya usaliti nitakuwa nakosea? Kama kawaida yake akaanza kujitetea, lakini utetezi wake haukuiniingia moyoni, ikabidi nifanye maamuzi haya;

Nikamwambia hivi, "Sitolala na wewe bila kutumia condom usije ukaniletea maradhi, hawa watoto wawili wanatosha ukitaka mtoto kazae na huyohuyo mzazi mwenzako, na mimi nikitaka nitamfuta wa kuzaa naye".

Sasa yeye anadai namnyanyasa, namuonea kwasababu ana mtoto aliyezaa na mwanaume mwingine, na hataki kukubaliana na maamuzi yangu. Ila mpaka sasa wanaendelea kuwasiliana na mzazi mwenzake kuhusiana na masuala ya mtoto wao.

Je, nani mwenye kosa hapo, mimi au yeye?
 
Wewe hapo ndio una Makosa kwa mtazamo wangu. Makosa kivipi?

1. Kuoa (Sijui umri wako ila under 40 mapema sana)
2. Kuoa tayari mtu anamtoto hafu BABA YAKE yupo hai na mzima (inabidi awe alifariki au yupo Milembe)
3. Kumchunguza mke wako.
4. Kutumia condom kwa mkeo iyo dharau aisee. Sijaona lakini mh iyo dharau kubwa.
5..
 
Kutumia condom kwa mkeo ni dharau kubwa,je mkeo kuwasiliana na mzazi mwenzake kwa kificho ni heshima kubwa?
 
Wewe ndio mwenye matatizo, muache huyo mama endelea na maisha Yako.

Kama huwezi kuishi na mwanamke mwenye mtoto ni heri umuache! Ulijua ana mtoto tangu mwanzo, uchumi umebadilika unasema huwezi kumlea mtoto wake. Je ingekuwa ni wanao wote wawili na uchumi umebadilika ungefanyaje?

Huwezi kujisimamia kimaamuzi, umelazimisha mwenyewe waanze kuwasiliana.

Mwisho mwanamke mwenye mtoto hata umpe Kila kitu ila mtoto wake hapati huduma, hawezi kuridhika kuona yeye anaishi vizuri mtoto wake haishi vizuri au hajui kesho ya mwanae. Labda kama mwanamke asiyejitambua.

So wanaume kama hamuwezi kuwatunza wanawake wenye watoto ni heri muwaache tu, msiwaongeze mizigo ya watoto wengine Kisha muanze kuwageuka.
 
Hiyo namba 2,

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kutumia condom kwa mkeo ni dharau kubwa,je mkeo kuwasiliana na mzazi mwenzake kwa kificho ni heshima kubwa?
Mapenzi ni hisia. Sio tu ejaculation. Sasa mkeo, haumuamini, hafu unakula mzigo, mi nitakua akiniwekea style mpya naanza waza usikute hii style jana alimpa jamaa, yaani hisia zitakua mbali sana.. Itakua kama napiga nyeto aisee.
 
Wewe ndiye unamatatizo makubwa au ukosefu wa Akili Kabisa.

Mwanamke mwenye mtoto sio Mkeo pekee yako.
Ukioa mke mwenye mtoto elewa kuwa mzazi mwenzake pia ni Mumewe, mzazi mwenzake, Baba WA m/watoto wake.
Hivyo ni halali yake kuwasiliana Naye Kama sio kumpa haki zake za kindoa.

Usioe single mother Kama wewe sio single father.
Mtalaka hatongozwi.

Mengine yote ni kujifariji kama binadamu
 
Wewe ndio mwenye matatizo, muache huyo mama endelea na maisha Yako.

Kama huwezi kuishi na mwanamke mwenye mtoto ni heri umuache! Ulijua ana mtoto tangu mwanzo, uchumi umebadilika unasema huwezi kumlea mtoto wake. Je ingekuwa ni wanao wote wawili na uchumi umebadilika ungefanyaje?

Huwezi kujisimamia kimaamuzi, umelazimisha mwenyewe waanze kuwasiliana.

Mwisho mwanamke mwenye mtoto hata umpe Kila kitu ila mtoto wake hapati huduma, hawezi kuridhika kuona yeye anaishi vizuri mtoto wake haishi vizuri au hajui kesho ya mwanae. Labda kama mwanamke asiyejitambua.

So wanaume kama hamuwezi kuwatunza wanawake wenye watoto ni heri muwaache tu, msiwaongeze mizigo ya watoto wengine Kisha muanze kuwageuka.
Kwakuwa naye anasoma hizi comments naamini atalifanyia kazi,aniache aendelee na maisha yake,mzazi mwenzake anapotaka kutoa huduma kwa mwanaye sio lazima awasiliane na yeye,kaka yake ambaye anaishi na mtoto yupo kwanini asiwe anawasiliana na huyo? Mke ni ni mume mmoja tu kuwasiliana na wanaume wawili hiyo ni ndoa ya wanaume wawili mimi sipo tayari.
 
Mapenzi ni hisia. Sio tu ejaculation. Sasa mkeo, haumuamini, hafu unakula mzigo, mi nitakua akiniwekea style mpya naanza waza usikute hii style jana alimpa jamaa, yaani hisia zitakua mbali sana.. Itakua kama napiga nyeto aisee.
Sahihi kabisa,nilimwambia hivi akitaka mchezo akanunue condom tutumie namimi nikitaka nitaenda kununua condom,mpaka sasa hakuna aliyekwenda kununua condom ,tunatizamana tu.
 
Wewe ndiye unamatatizo makubwa au ukosefu wa Akili Kabisa.

Mwanamke mwenye mtoto sio Mkeo pekee yako.
Ukioa mke mwenye mtoto elewa kuwa mzazi mwenzake pia ni Mumewe, mzazi mwenzake, Baba WA m/watoto wake.
Hivyo ni halali yake kuwasiliana Naye Kama sio kumpa haki zake za kindoa.

Usioe single mother Kama wewe sio single father.
Mtalaka hatongozwi.

Mengine yote ni kujifariji kama binadamu
Nakubaliana nawewe 100%
 
Funguka zaidi hapa mkuu.

Uliwahi sikia Serikali ikiwalaumu wananchi?
Uliwahi sikia Wazungu wakiwalaumu Waafrika?
Uliwahi sikia Watawala wakiwalaumu watawaliwa?

Unapoingia kwenye mahusiano yoyote hakikisha wewe ndiwe tabaka la juu, unayepewa lawama.
Hakikisha wewe unakuwa mshtakiwa sio mshtaki.

Kama Mwanamke anakusumbua FUKUZA, Kama huwezi MPE kichapo akakushtaki huko atoe lawama yeye sio wewe.

Kulialia mtoto wa kiume ni kumaanisha huna mbinu, huna akili, umezidiwa steps.
 
Tulioana miaka kadhaa iliyopita na tumejaaliwa watoto wawili. tTulioana mke wangu akiwa na mtoto mmoja aliyezaa akiwa kwao. Miaka ya mwanzoni uchumi uliruhusu kutoa huduma hata kwa mtoto wake ambaye anaishi na mjomba wake, baada ya uchumi kuyumba nikamwambia mwenzangu ongea na shangazi yake mtoto amwambie kaka yake aanze kumhudumia mtoto wake.
Wewe ndo mwenye matatizo.

UNAISHI NA MKE WA MTU.

Kubali matokeo kama Yanga
 
Uliwahi sikia Serikali ikiwalaumu wananchi?
Uliwahi sikia Wazungu wakiwalaumu Waafrika?
Uliwahi sikia Watawala wakiwalaumu watawaliwa?

Unapoingia kwenye mahusiano yoyote hakikisha wewe ndiwe tabaka la juu, unayepewa lawama.
Hakikisha wewe unakuwa mshtakiwa sio mshtaki.

Kama Mwanamke anakusumbua FUKUZA, Kama huwezi MPE kichapo akakushtaki huko atoe lawama yeye sio wewe.

Kulialia mtoto wa kiume ni kumaanisha huna mbinu, huna akili, umezidiwa steps.
Tumekubaliana tuje kwenu baada ya mvutano mkali,hatujataka yaende kwa majirani au kwingineko tukawapa faida,naye anafuatilia huu uzi.
 
Back
Top Bottom