And now this,
*Kikwete atuma rambirambi (Mwananchi)
Fidelis Butahe
JESHI la Polisi Kanda ya Dar es Salaam limeomba ushirikiano kutoka kwa wananchi ili kusaidia kumkamata mtu anayetuhumiwa kumuua mke wa balozi mwandamizi wa zamani wa Marekani, Andrew Daraja.
Anna Daraja, mke wa balozi huyo, aliuawa juzi nyumbani kwake Kimara Temboni kwa kuchomwa kisu kifuani na mtu ambaye
anatuhumiwa kuwa ni James Mabakuri, 22, ambaye alikuwa mhudumu wa shamba.[/quote]
Nani anamtuhumu,.. soma hapa chini. Inaonekana ni magazeti tu ndiyo yenye kumtuhumu na Polisi.
Kaimu kamanda wa polisi wa Kanda ya Dar es Salaam, Charles Kenyera alisema kuwa polisi wamekuwa wakimfuatilia mtuhumiwa tangu tukio hilo litokee lakini hawajafanikiwa kumpata mtuhumiwa.
Watoke hapa, kwani walifanikiwa kiasi gani kumpata dereva aliyesababisha ajali ya Waziri Salome Mbatia? au wanafikiri tushasahau?
"Tangu litokee tukio hili la mauaji tumekuwa tukimtafuta mtuhumiwa kwa kuwa yeye alikuwa akiishi katika nyumba ile na baada ya mauaji hakuonekana na hajulikani yuko wapi," alisema Kenyera.
Labda waache kumuita mtuhumiwa kwanza.. hata ningekuwa mimi kama sikufanya hivyo na katika mazingira hayo na kila mtu ananiita mtuhumiwa nitatimka! Mmesahau "The Fugitive"?
"Tunaomba wananchi wanaomfahamu kijana huyo pamoja na mwajiri wake kushirikiana na Jeshi la Polisi ili tuweze kumkamata... nasema hivi kwa kuwa polisi hatuwezi kumfahamu bila kuwepo kwa ushirikiano kumpata itakuwa kazi ngumu, tunaamini kuwa malengo yake yalikuwa ya kinyama."
Polesi acheni ushamba; acheni kumuita mtuhumiwa, hakikisheni usalama wake, na mumtie moyo huko aliko kuwa atapata nafasi ya haki ya kuelezea upande wake. Huko aliko huyo kijana kama hakuhusika na anajua kilichotokea asijitokeze hadi Polisi wabadilishe kumuona ndiye mhusika wa mauaji!
Kamanda Kenyera alisema kuwa Februari 14 mwaka huu Balozi Daraja alimuaga mke wake kuwa anasafiri kwenda Muheza, Tanga na kumuacha na mhudumu wa shamba ambaye alikuwa akiishi kwenye nyumba hiyo.
"Balozi Daraja aliporejea alifika getini na kugonga geti, lakini hakuna mtu yeyote aliyefungua ndipo dereva wake alipoamua kuruka uzio na kwenda kufungua mlango lakini alipoingia ndani alikuta mwili wa marehemu ukiwa gereji huku kisu kikiwa kimechomwa kwenye titi, mpaka sasa hatujafanikiwa kwa lolote ila tunamshuku huyu kijana kwa nini atoweke baada ya kutokea mauaji,"alisema Kenyera.
Excuse me.. what about the phone call kuwa Amb. Daraja alipiga kutaarifu ujio wake. Simu ya marehemu imepatikana?
Vyombo vya habari jana vilimnukuu kamanda wa polisi wa Kinondoni, Elias Kalinga akisema kuwa baada ya kuhakikisha mama huyo amekufa, mtuhumiwa alifanya upekuzi kwenye nyumba hiyo, ikiwa ni pamoja na chumba cha balozi na kuiba kiasi cha Sh2 milioni na kutoweka kusikojulikana.
Haiingii akilini. Yaani, anamuua mtu halafu ndio anatafuta kama kuna fedha? Au alishajua kuwa zipo fedha ndio akafanya hicho kitendo? Lakini on the other hand, kama huyo kijana alikuwa anataka fedha tu, na yuko na huyo mama angeweza kabisa kuiba hizo fedha na kutoweka bila kuua? don't you people use some neurons!?
"Tunatarajia kuondoka Alhamisi kueleleka Muheza kwa mazishi kwa kuwa kijana wangu atafika kabla ya siku hiyo. Huyu kijana ninamshuku ila siwezi kusema kuwa yeye ndio aliyeua lakini akipatikana na uchunguzi ukafanyika ndio ukweli itajulikana," alisema Daraja.
what what what?? kumbe Balozi Daraja hamtuhumu mtumishi wake kuwa ndiye aliyefanya kitendo hicho? so kwanini Polisi wanafikiria hivyo? Change the strategy you morons! Mnampa muda muuaji au wauaji kujificha zaidi!