TANZIA Mke wa Clatous Chama afariki dunia

TANZIA Mke wa Clatous Chama afariki dunia

Pumzika mahali salama shemeji yetu
 
Salaam Wanasimba wenzangu


Niwape hongera nyingi kwa ushindi mkubwa tulioupata leo kule Ruangwa dhidi ya Namungo na kiukweli njia ya ubingwa kwa sasa ni nyeupe zaidi upande wetu !!

Nimeamua kuandika ujumbe wangu kwenu ukiwa makhsuus baada ya Nyota wetu wa kimataifa Mzambia Cleoutus Chama ,kupata msiba mzito wa kuondokewa na mkewe leo mjini kitwe Zambia

Ktk miaka ya karibuni hatujawahi kama klabu kuondokewa na mke wa mchezaji wetu na sote tunajua umuhimu wa mke ktk maisha yetu ,,
Hili ni pigo kubwa sana kwa kiungo huyo bora kabisa Afrika kwa sasa ,,

Lazma itamuathiri kisaikolojia na hapa ndio dhumuni hasa la waraka wangu huu,,

Njia pekee ya kumfariji ni walau Wanasimba kupitia Magroup yenu ya Watsapp kutoa ubani wa rambirambi kwa fundi huyo anaetupa raha kila uchwao ,,hii itamuongezea nguvu mno na kujua Wanasimba wanamthamini kiasi kikubwa ,,,

Muhimu mtakachotoa kiwe cha hiyari na kisha baada ya kumaliza mnaweza kutuma kwa namba hii rasmi ya klabu 0742771311,,,

Na baadae CEO na Mwenyekiti wetu wamkabidhi legendary huyu wa Simba pole yetu

Upande wetu kama Klabu tumejopanga kwenda kuungana na Chama kwenye maziko ya mkewe kule Zambia na tutashiriki kwa kila namna kumfariji Maestro wetu tunaempenda mno!!

Niwaombe tangazo hili lisambazwe ktk Magroup yote ya Watsapp ya Simba na mwisho wa kupokea mchango huu ni Tarehe tatu ya mwezi wa sita yaani Alhamis ijayo usiku ,,

Hope Wanasimba wenzangu tutashirikiana na mwenzetu ktk majonzi yake kama yy anavyotupa furaha ya moyoni siku zote ,,


SIMBA NGUVU MOJA


WENU MSEMAJI WENU
HAJI S MANARA
BUGHATTI
 
Kwani kafa chama mkuu si kafa mkewe na nimetoa RIP?
Ni kweli lichama silipendi itoshe kusema hivyo
Mkuu uchawi Kama umekuzidi ,mrudie Mungu option bdo ipo.kutapika uhalo kwa kiumbe mwenzio ni kufuru .
Izo nyasi unazokula badala ya kuvuta zinakupa ujasiri uliopitiliza
 
Mungu Mwenyezi aipokee roho ya marehemu aiweke mahali pema peponi Amina
 
Ndo hapo sasa isije ikawa kuna makafala yanayotolewa bila wao kujua. Michezoni siku hizi kuna ushetani mwingi sana. Makampuni ya kamari,pombe na sigara ndio wadhamini wakuu wa michezo. Vipi km wao ndo wanahusika kwenye haya??
Hata timu zao pia zinaweza husika pengine hata wao wenyewe.
 
Back
Top Bottom