Sio kweli, wapo wanasiasa ambao ni committed kama Dr. Slaa, Hon. Zitto na the likes pia wapo wanasiasa ambao ni wasanii, wanajulikana hakuna haja ya kuwataja. Msanii anajulikana kwa maneno na matendo.
Mungu ibariki Tanzania
Utafanya kosa la karne kujaribu kumwamini MWASIASA anapoibua UOVU wa mwanasiasa mwenzake.
Pila utafanya kosa la karne kujaribu kuamini ama kumtafsri mtu kutokana na maandikp yake badala ya matendo.
Mimi ningekuomba unieleze ILANI ya hao wapiganaji iliyowaingiza 2005 bungeni ni mangapi wameyatekeleza waliyo waahadi wananchi ktk majimbo yao?
[/SIZE]
mkamap,
Unaongelea watu gani, could you be a little more specific ? Kumbuka watekelezaji mliwaweka wenyewe madarakani na wanaongoza serikali. Kazi anayoifanya Dr. Slaa na wale wote waliojitolea mhanga kutetea wananchi na kukemea uovu ndani ya jamii si kazi ndogo. Isije ikawa na wewe uko kwenye kundi linaloeneza ujinga wa siku zote wa kuwabeza wapinzani ati wamefanya nini huku madaraka mmewanyima na badala yake mmechagua uozo kama tunavyoshuhudia. Kumbuka usemi kuwa ni heri jeshi la kondoo linaloongozwa na simba kuliko jeshi la simba linaloongozwa na kondoo.
Kithuku,
Mkuu wangu weee! hata kama una machungu na Chadema kama chama basi usiwapake tope hata watu wenye mahusiano na wana Chadema...
Inazidi kunisikitisha sana mkuu hasa pale napokuona wewe, Masatu, na Mkamap mnapojaribu kuharibu majina ya watu kwa sababu tu wanatoka upande wa pili...
Iweje kweli siasa ni Usanii?.. au labnda mimi ndiye nisiyejua maana ya Usanii maanake navyofahamu mimi Sanaa ni Maigizo ama mchoro/mchongo unaoashiria uhai fulani..Lakini sanaa pekee haina ukweli ama hali halisi, kama vile tungo za hadithi ktk maandishi.
sasa ikiwa kweli Dr. Slaa, mkewe na hata Zitto ni wasanii inatupeleka wwapi ktk ukweli wa matukio yote yaliyozungumzwa. Je, ina maana hakuna kitu kama hicho isipokuwa hawa jamaa wametunga na kutuchorea samaki ukutani?..
Jamani jamani, msiwe wapinzani kiasi kwamba mnapotosha hata wananchi mahala ambapo maslahi ya nchi yetu yananazidi kuporwa na watu ambao nyie wenyewe kwa nafsi zenu hamkubaliani nao ama hampendi yanayotokea...Hata kama nyie ni makada wa CCM inabidi mpongeze vitu kama hivi na kuonyesha kwamba wapo watu ndani ya CCM wanaumia na kuchukia rushwa kama wananchi wengine..
Hivi kweli madai ya hayo mamilioni anayozungumzia mama huyu mnaona kuwa ni mchezo wa usanii? hakuna kilichotokea isipokuwa anatafuta sifa jukwaani?..
Kwani wakati wanaomba kura walikua wana waimbia sera gani wananchi? ni hao ma ORYA wetu humu.
SERA zao wenyewe zimewashinda wakaona AHAA UFISADI ndipo pakutokea
wakaona tutoke vipi ehe wakasema lazima tutoke kwa mgongo wa FISADI.
Unapomtafuta nyoka uvunguni anza kutwanga tochi kutokea miguuni kwako SASA ma WARYA wetu ngoja nichukulie KIGOMA badala ya kupiga kelele miundo mbinu mbofumbofu barabara kama za ng'ombe zikiendana na korasi ya UFISADI.
wao wameibwaga hiyo maana wameona ni ngumu kutoka nayo maana ya UFISADI kutoka nayo ni rahisi zaidi.Haya mkuu MWALIMU mzuri ni MDA
1.
Mkuu haya maneno yanaweza kuwa na ukweli, iwapo utathibitisha hapa kuwa kabla ya kuwa mbunge, Dr. Slaa alikuwa hana kazi yoyote, lakini kama alikuwa nayo basi hii kauli unahitaji kuifuta, maana ni kumpaka matope Dr. Slaa bila sababu ya msingi politically au iwe personally!
Dr. Slaa ni mzaliwa wa Karatu, sio mgeni wa kutoka jimbo lingine, sasa kama ameona ana uwezo wa kuwasidia wananchi wake, na nafasi ipo kupitia Chadema, what is wrong with that? Yaani unasema sisi wananchi tuache kutafuta njia za kuyasaidia majimbo yetu kwa kuwazikiliza baadhi ya viongozi mafisadi wa CCM?
Kwa hiyo unasema kwua viongozi wote wa upinzani waliowahi kuwa wanachama wa CCM waliondoka kwa hasira kwa sababu walijua kuwa hawana chance ya uongozi kule? Kwa hiyo una maana hawa viongozi ni wasalaiti kama anavyosema Makamba? Alichofanya DR. slaa ndiyo hasa demokrasia yenyewe at work!
Labda uifafanue zaidi hii point!
4.
Migogoro ya siasa ipo katika kila chama cha siasa dunaini haikwepeki, na ndio demokrasia yenyewe, sio kwamba viongozi wa chama cha siasa lazima wakubali tu kila wanachoambiwa na wengine, hapa kwa kweli hatumsaidi Dr. Slaa na anything kama hii ishu, ila ninaamini tumefikia mahali tuna-abuse tu kuwepo kwake hapa JF.
Infact recently tumenza kushindwa kuitumia nafasi ya DR. slaa kisiasa na kuwepo kwake hapa na tumeanza kuitumia nafasi yake na kuwepo kwake hapa kama adhabu kwake, nafikiri tunahitaji kufikiria tena umuhimu wa kuwepo kwake hapa JF na tuweze kuitumia nafasi hiyo kwa faida ya taifa badala ya never ending attacks tena personally, that is low!
Mkuu hawa watu wanajua wanafanya makusudi.Inasikitisha mtu mwenye uelewa mkubwa kama KJ kutoa matamko kwama haya.Nafikiri fundisho alilotoa Rais Thabo Mbeki litachukua mda mrefu kwa waafrika kuelewa,lakini tunaenda taratibu maana Tanga tayari wameshaelewa somo kwa kuchagua madiwani wa CUF licha ya vitisho vya Katibu wa Mkoa wa CCM aliyesema wakichagua upinzani miradi ya maendeleo haitapelekwa.Wananchi hawa wametoa somo kwa viongozi ambao bado wamegubikwa na mfumo wa chama kimoja kifikra.
Mimi naomba Dr Slaa na FMES msikatishwe tamaa na watu wa aina hii,kazi yenu ni ya kitume.Manabii wote wa mungu walipingwa sana,licha ya kwamba walikuwa wanawahubilia njia sahihi za kupata baraka kutoka kwa mwenyezi mungu.Matokeo hayo ya Tanga na Maswa ambako CHAUSTA imeshinda ni matokeo ya juhudi zenu za kuwakomboa wananchi kifkra.
Nawaombeni nyie wote wenye kuweka mbele maslahi ya taifa letu,hakika mtashinda kwa sababu hamkinzani na dhamira zenu.Hao wanaoshabikia ufisadi wanapingana na dhamira zao,sanasana wanasukumwa kukidhi tamaa ya miili yao sio fikra na dhamira zao zinasutwa rohoni mwao.
Masatu,
Mkuu acha zako hizo yaani unataka kunambia kama wewe ni Muislaam/mkristu, baadhi masheikh/Mapadre wakiwa wazinifu basi huna haja ya kuwalaumu wao bali dawa ni kuondoka dhehebu hilo?..
Unachoamini ni hao masheikh au kitabu?..
Hakuna mtu anayepinga katiba ya chama, ilani ya chama wala sera za chama isipokuwa chama kimeshikwa na watu wasioamini wala kuongoizwa na kitabu..
Mama Slaa ni mmoja kati ya waumini wanaofuata kitabu na wanasema ukweli hata kama ukweli huo unawaumbua baadhi ya viongozi wa juu.
Masaki,
Bila shaka mkuu, Ni mfano tu unaolingana na matakwa yako kwa nini Mama Slaa bado yuko CCM ikiwa imejaa mafisadi..Anachofanya ni kujitenga na kundi baya linaloharibu jina la chama.
Its simple Chadema wanaamini CCM imejaa mafisadi, imechoka na haiwezi tena kuongoza. Kamanda wetu ana share kitanda na mmoja wa hao Mafisadi ambao deepdown anaamini CCM ni wameharibika beyond repair.
Swali: Huyu Mama anafanya nini huko CCM kama si usanii? Does this sound to b rocket science?
Neno imejaa mafisadi, haina maana kwamba wote ni mafisadi unless wangesema kuwa wote ni mafisadi, lakini hawakusema hivyo unless kuna something I am missing!