1.
Mkuu haya maneno yanaweza kuwa na ukweli, iwapo utathibitisha hapa kuwa kabla ya kuwa mbunge, Dr. Slaa alikuwa hana kazi yoyote, lakini kama alikuwa nayo basi hii kauli unahitaji kuifuta, maana ni kumpaka matope Dr. Slaa bila sababu ya msingi politically au iwe personally!
Dr. Slaa ni mzaliwa wa Karatu, sio mgeni wa kutoka jimbo lingine, sasa kama ameona ana uwezo wa kuwasidia wananchi wake, na nafasi ipo kupitia Chadema, what is wrong with that? Yaani unasema sisi wananchi tuache kutafuta njia za kuyasaidia majimbo yetu kwa kuwazikiliza baadhi ya viongozi mafisadi wa CCM?
Kwa hiyo unasema kwua viongozi wote wa upinzani waliowahi kuwa wanachama wa CCM waliondoka kwa hasira kwa sababu walijua kuwa hawana chance ya uongozi kule? Kwa hiyo una maana hawa viongozi ni wasalaiti kama anavyosema Makamba? Alichofanya DR. slaa ndiyo hasa demokrasia yenyewe at work!
Labda uifafanue zaidi hii point!
4.
Migogoro ya siasa ipo katika kila chama cha siasa dunaini haikwepeki, na ndio demokrasia yenyewe, sio kwamba viongozi wa chama cha siasa lazima wakubali tu kila wanachoambiwa na wengine, hapa kwa kweli hatumsaidi Dr. Slaa na anything kama hii ishu, ila ninaamini tumefikia mahali tuna-abuse tu kuwepo kwake hapa JF.
Infact recently tumenza kushindwa kuitumia nafasi ya DR. slaa kisiasa na kuwepo kwake hapa na tumeanza kuitumia nafasi yake na kuwepo kwake hapa kama adhabu kwake, nafikiri tunahitaji kufikiria tena umuhimu wa kuwepo kwake hapa JF na tuweze kuitumia nafasi hiyo kwa faida ya taifa badala ya never ending attacks tena personally, that is low!