Mke wa mgombea wa CHADEMA Manyoni : Nilimwambia Polisi naomba usimuue mume wangu lakini alimpiga risasi nne

Ubinafsi utakuja kukuponza mkuu. Leo yanatokea kwa hao unaowaita wa Mbowe kesho yatakurudia na hapatakuwa wa kupaza sauti kwa ajili yako. UBAYA hauna macho.
Mwaka kesho sio mbali. Walichowafanyia wapinzani kwenye uchaguzi huu watafanyiana kwenye uchaguzi ndani ya chama. Wataibiana kura na watauana. Apandacho mtu ndicho atakachovuna.
 
Vijana nawaambia kila siku acheni kutumika na wanasiasa kesho utamkuta Mbowe ikulu wewe umeacha familia inateseka
Pumbavu mkubwa wewe...

"Kutumika na wanasiasa" maana yake nini...?

Yaani mtu wa CHADEMA kugombea uongozi (tena uenyekiti wa kitongoji tu) usio na mshahara wala posho ili kushindana na CCM ndiyo iwe kosa la polisi kimuua kijana huyu..?

Alichofanya kijana huyu kutumia haki yake ya kikatiba na kisiasa kugombea uenyekiti wa kitongoji kwa tiketi ya CHADEMA ndiyo "kutumika na wanasiasa" unavyoelewa wewe...?

Narudia tena kukuambia👇👇 kuwa...

You're very ignorant and stupid at the same time....!!!
 
Vijana nawaambia kila siku acheni kutumika na wanasiasa kesho utamkuta Mbowe ikulu wewe umeacha familia inateseka
Mjinga sana wewe,mtu kutumia haki yake kama mwananchi kugombea nafasi ya uongozi ndiyo kutumika na Mbowe? Je hao wagombea wa ccm nao wanatumika na Samia au nani? Kama kutumika ni hao maaskari ndiyo wanatumika na kujipendekeza kwa kuua na kuumiza masikini wenzao kwa kuhongwa vihela vidogo vidogo na mabwana zao ccm huku maisha yao yakiendelea kuwa magumu huku wakilazwa kwenye makazi duni kama mbwa.
 
Vijana nawaambia kila siku acheni kutumika na wanasiasa kesho utamkuta Mbowe ikulu wewe umeacha familia inateseka
Mbowe anaingiaje wakati mtu anagombea kitongoji.... kwani hayo ni maandamano au uchaguzi?
 
Sijazungumzia watanzania nimewazungumzia wapinzani (chadema).
Wanaamini siasa ni rahisi kiasi hicho ndiyo maana wakifanyiwa vitendo viovu wanalalamika na hawapati Masada wowote.
siasa za kuuana???
 
Wakuu,

Nimekutana na video ya mke wa Mgombea kupitia Chadema wa Kitongoji cha Stand, kata ya Mkwese, Jimbo la Manyoni Mashariki George Juma Mohamed akielezea namna ambavyo polisi walimkamata na kumuua mume wake kwa kumpiga risasi nne.

Mama huyu anasema kuwa aliwaomba polisi wasimuue mumewe lakini polisi walimpiga mume wake risasi nne na hivyo mume wake alifariki dunia

Pia alisema kuwa mwanae aliona jinsi baba yake alivyouwawa kikatili na polisi.

Soma pia: Manyoni: George Juma Mohamed, Mgombea wa CHADEMA auawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia tar 27, 11, 2024

=========================================

Naomba niishie hapa. Nisije nikaandika zaidi nikaharibu.

Ila haya mambo yote huwa yana mwisho na mwisho wake huwa sio mzuri

View attachment 3166595
Mmh hii nchi hii
 
Waafrica hatuwesi siasa za kistaarabu, kifupi civilization hatuiwezi maana sisi tuna vinasaba vya wanyama yaani kiasili sisi ni wanyama. Sisi tuna tofauti kubwa saana na binadamu wenye ngozi nyeupe.

Yanayoendelea Msumbiji & Angola na kwengineko Africa ni maana halisi ya uafrica wetu.
 
Well said.
 
Wakuu,

Nimekutana na video ya mke wa Mgombea kupitia Chadema wa Kitongoji cha Stand, kata ya Mkwese, Jimbo la Manyoni Mashariki George Juma Mohamed akielezea namna ambavyo polisi walimkamata na kumuua mume wake kwa kumpiga risasi nne.

Mama huyu anasema kuwa aliwaomba polisi wasimuue mumewe lakini polisi walimpiga mume wake risasi nne na hivyo mume wake alifariki dunia

Pia alisema kuwa mwanae aliona jinsi baba yake alivyouwawa kikatili na polisi.

Soma pia: Manyoni: George Juma Mohamed, Mgombea wa CHADEMA auawa kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia tar 27, 11, 2024

=========================================

Naomba niishie hapa. Nisije nikaandika zaidi nikaharibu.

Ila haya mambo yote huwa yana mwisho na mwisho wake huwa sio mzuri

View attachment 3166595
It is a painful story on the global, ni uchungu mkubwa
 
Back
Top Bottom