Moisemusajiografii
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 43,960
- 77,533
Ooh... Lord,have mercy! Ameanza marembuzi? Fanya hivi:Funga kula siku tatu mfululizo. Piga maombi makali. Kemea. Kumbuka,wakati huo chakula chako kiwe maji na tende tu nyakati za jioni tu. Utashinda.Hiyo ya mwizi nimeipenda naona leo nimepita tena kaongeza na kurembua macho. Angejua kuwa nimemuanzishia uzi huku ...........
Mkuu asante kwa ushauri ntafanyia kazi maana kaomba na namba ya simu ili nikipotea anitafute.Ooh... Lord,have mercy! Ameanza marembuzi? Fanya hivi:Funga kula siku tatu mfululizo. Piga maombi makali. Kemea. Kumbuka,wakati huo chakula chako kiwe maji na tende tu nyakati za jioni tu. Utashinda.
Barikiwa mtumishi..Kitendo cha kubaini kuwa huo ni mtego bora uuache...ni heri kuonekana kuwa mjinga kwa mtazamo wa mtu mmoja au 2 na kuuonekana mwerevu kwa watu wengi zaidi, utajijengea heshima na baraka mbele za Mungu.
Ubarikiwe mtumishi...Bibilia inasema ikimbie zinaa, Huyo mwanamama anataka akualibie future yko.
Mtego huoKama mada inavyojieleza wadau. Nina rafiki yangu ambaye anamiliki Mini supermarket. Na pale amemuweka mke wake aisimamie. Mara kwa mara mimi hufika pale kwa ajili ya kufanya manunuzi na kumuungisha rafiki yangu. Kama mwezi mmoja uliopita huyu mama ambaye ni shemeji akaniambia shemeji leo nimekuota. Nikachukulia ni hali ya kawaida ya mfanyabiashara kuvutia mteja. Siku tatu baadae wakati nalipia manunuzi yangu akaniambia tena huku akishangaa na kuniuliza, inakuaje niote nafanya mapenzi na wewe wakati nimelala na mume wangu? Mara ya pili sasa nakuota. Kwa jinsi nilivyo mstaarabu nikaazimia kuacha kufika dukani hapo. Sasa juzi rafiki yangu akaniuliza shehe mbona umeacha kuniungisha shemeji yako anasema hakuoni siku hizi. Au umepata sehemu yenye huduma bora kuzidi kwetu? Nikamwambia nachelewa kutoka kazini. Tukaishia hapo. Sasa maswali ninayojiuliza na kuomba msaada kwa wadau ni haya. Inawezekana kweli mwanamke akamuota mwanamme mwingine wakati amelala na mumewe? Na inawezekana kuwa huyo mwanamke ametamani kuchepuka na mimi na akaamua kutunga uongo ili aninase kirahisi? Na swali la tatu ni je hakuna uwezekano kuwa hiyo ni mpango uliopangwa baina ya wawili hao ili wanifumanie na kunichomoa kiakiba changu? Naomba kuwasilisha..