Mke wa mtu ananiomba niigize kama jamaa yake

Mke wa mtu ananiomba niigize kama jamaa yake

Usijaribu kujiweka matatani sababu ya akili ya mwanamke. Anachodhamiria kukifanya sio chepesi kama jibu alilokupa.
Anasubiri zahama itokee aishie kusema "jamani sikujua kama mume wangu ni katili hivi"
 
Na ww mwambie unaweza kuplay role ya kama baba mkwe wake vizur tu kama atakubari
 
"Hawezi kukufanya chochote bana yule mimi namjua" haya ndio maneno yake anayoyarudiarudia kila mara ninapomsisitizia kuwa siwezi kufanya hivyo...Huyu Dada tuna ukaribu naye kibiashara na sina uhusiano nae wa kimapenzi na wala sitarajii kufanya hivyo.

Mumewe tunafahamiana juujuu tu ila naye ameshajiridhisha kuwa sina hatari yoyote kwa mkewe zaidi ya kazi.

Ingawa Mwana Dada haweki wazi sana ni nini lengo lake la kutaka ionekane hivyo zaidi ya kusema tu anataka ampe jamaa tumbo joto bila kujali madhara gani yanayoweza kunikuta mimi "Muigizaji".

Nikimuuliza anataka nifanye nini husema anataka niwe namrudisha nyumbani kwake usiku na Mumewe ajue kuwa alikuwa na mimi, ingawa yeye atakuwa anamwambia alikuwa na mimi kikazi huku akijua wazi Jamaa atapatwa na jekejeke...na hilo ndio haswa lengo lake.

Ukisikia mtihani ndio huu.
Ukisikia mtihani ndio huu.
 
Na wewe utafumuliwa malinda kwa kuigiza hivyo hivyo
 
We hujui kuwa huo ni mpango wao (mume na mke) wanakutengenezea deal ili jamaa akufumanie na hiyo biashara wakutaifishe, we kweli hamnazo kabisa, zakuambiwa changanya na zako.
 
Kabisa, ila kuushinda ni kutotekeleza hilo takwa la Mwanadada.
Sorry kama nitakukwaza,
Nadhani hata wewe haupo timamu kwa asilimia zote,hivi hili nalo kwa mtu mzima tena mfanyabiashara unahitaji kushauriwa na MTU..
Kweli Tz ya uchumi wa kati imepatwa .
 
Usikubali kuigiza.....bora ule mzigo tu ili siku ya kutolewa marxnda, utolewe kihalali.
 
Back
Top Bottom