Nafikiri tatizo lenu liko kwenye pesa. Mwanaume unatakiwa kujua majukumu ya kulea familia, kama ada, chakula, kujenga nyumba, kununua magari, mafuta ya magari yooote ni ya kwako.
Kamwe hutakiwi kutegemea mwanamke au kuulizia kipato cha mwanamke. Fedha za mwanamke ni kwa ajili yake na familia yake lakini pia ukiwa unatimiza majikumu yako ata kusupport mwenyewe bila kumuomba katika viti kama mavazi ya watoto, mapambo ya ndani, nguo zenu n.k. Hayo yote anatakiwa afanye kwa kujisikia siyo kulazimishwa.
Mnapokosea nyie vijana wa siku hizi ni kutafuta mke mwenye kazi halafu mnamtegemea atimize majukumu ya nyumbani. Hapo amesha kuchoka kwamba unamtegemea yeye.
Ndo maana wanasema mwanaume anaweza kukaa na mke asiye na kazi throughout life time, lakini mwanamke hawezi kukaa na mume asiye na kazi hata kwa mwaka tu.
Mkeo amechoshwa na tabia yako ya kupenda mteremko katika uendeshaji wa familia. Cha kufanya chukua majukumu yako usimuuloze kuhusi hela zake.