Mke wa ndoa anaposema maneno haya anamanisha nini ?

Mke wa ndoa anaposema maneno haya anamanisha nini ?

Iko hivi mwaka 2008 tulibahatika kupata mtoto bila ndoa 2014 tukapata mwingine bila ndoa ila mwaka 2016 tukabariki ndoa na sasa tunaishi kwenye ndoa ya watoto watatu sasa hivi huyu mke amekuwa na maneno makali ya kuchoma moyo na mwili
mfano

1.nilimwambia jana mbona nguo chafu na hapo jikoni hapako vizuri na nasema hivyo coz kulikuwa ma wageni watakuja kututembelea akaniambia mwanaume wewe una gubu

2.ananiambia nimemweka kifungoni nimemfanya mjinga sana kwa mda mrefu ila sasa ninajitambua
ananiambia hivyo baada ya kumwambia tuweke mahesabu sawa kati ya fedha take na yangu kwa ajili ya maandalizi ya watoto shule january alikuwa mkali kama pilipili na hajawahi kuniambia maneno aliyoniambia
mfano;

Miaka yote pesa yangu sina uhuru nayo nimesomeshwa na wazazi wangu kwa ajili ya faida yao na siyo kwako na matoto yako kwa ujue utawapeleka vipi matoto yako shule pesa yangu achana nayo kabisa kama unataka uje uniombe
hapa nikamjibu haitatokea kumwomba kama amechoka watoto anipe wanangu

3.Ongeza hawezi mapenzi ya kubembelezana bembelezana sijui nikupetipeti sijui nikulambe wapi ukiyataka hayo katafute wenye nayo kwangu hutoyapata na ukitaka kaoe kabisa ila ujue watoto wao na akaongeza siogopi kuachwa hata kidogo na ungejua kilichopo moyoni mwangu(kwake mke) ungenyamaza tu

Huwa nina kawaida ya kumsaidia kazi za ndani kama kuchota maji,kufua,kupika, sasa jana kaniambia wala sitaki unisaidie vikazi unavyonisaidia.

then wenzangu mlioko kwa ndoa na mna watoto siyo chini ya watatu nguo zenu zinanyooshwa na wake zenu au nyie wenyewe,viatu au makobazi yanafuta na kupakwa ranging na mke au nyie wenyewe.
je maji ya kuoga mnapeleka wenyewe au mnapelekewa mimi nafanya vyote hivyo mwenyewe .

Anasema hayo yote then asubuhi analia tu na kusema yaishe nashindwa hata kuelewa anataka nini anafikiri nini na matarajio yake nini
Achana naye. Huyo yupo tayari kukua sasa ukichelewa utaleta thread mbaya ya hatari. Kwanza huna mke huyo atat..bwa nje na anajituma sana.
 
Tafuta Fimbo nzuri hifadhi mahali. Mchokoze halafu akikujibu tu funga mlango mlabue za kutosha then mwandikie kabarua mwambie ndio talaka sijibiwagi na wanawake hivi. Ila hakikisha watoto umewapeleka kwa bibi yao. Huyo takataka amepata mashauri ya ibilisi bila fimbo hazitoki. Pia inatakiwa aende kwao akiwa na ma alama ili asiwe na haraka ya kurudi pia mtishie kuwa unamkata unanoa Sime hadi iwe kali au nunua toi la bastola. Akiona heshima itakuwepo hawa watu ni pasua kichwa hasa akichafukwa.


Na siku zingine acha upumbafu mwanamke hasaidiwagi kazi zake hata kama anaumwa. Labda uone amezidiwa sana. Ishini nao kwa akili. Hii ndio akili acha maujinga yako
 
Wewe ni zao la Beijing mkuu
Sijui nisemaje lakini kukunyima mshahara wake ni haki yake ....pesa za mwanamke ni za kwake yeye mwenyew ..kama ataamua kukusaidia majukumu sawa vinginevyo hutakiwi kuzipangia matumizi zile ni zake....kakwambia kweli kasomeshwa na wazazi wake ili awafae baadae hakusomeshwa sababu nyingine ....kingineee kupeleka maji bafuni sio kazi yake labda aamue kukupelekea kwa mapenzi yake tu .....kufua pia labda aamue kukufulia kwa mapenzi tu vinginevyo tafuta dobi ...samahani kama utakwazika lakini habari ndiyo hiyo

Somesha wanao usimtegemee yeye wewe ndie kichwa na kiongozi wa familia
 
Sio sahihi kabisa sasa si bora aache kazi nijue ni mama Wa nyumbani Mimi Mke wangu awe anafanya kazi then hela yake iaionekane home namfyekelea mbali bora akae nyumbani anilelee watoto
Kwanza, ndio watu wajifunze kwamba huo utaratibu wa kuishi kimada na mwanamke kwa miaka hata minane ili ati kusomana tabia hausaidii kumjua mwanamke vilivyo. Mwanamke utamjua akishakuwa ndani ya ndoa na kukita mizizi kwa kuzaa nawe watoto kadhaa.

Pili, mkeo ktk habari ya pesa yake yuko sahihi. Inaonesha alikuzoeza maisha ya kitamthilia ya kukufanya uwe na amri na pesa yake. Wakati ule alikuwa atafuta ndoa. Sasa alishaipata. Anahitaji atumie pesa yake anavyotaka mwenyewe akiwasaidia wazazi wake waliomsomesh, na kwa hili yupo sahihi. Ni jukumu lako kuhudumia watoto wako kwa mavazi, chakula, makazi na elimu. Ukikwama kopa kwa rafiki zako.
 
Siku hizi wanaume wanataka haki sawa na wanawake

Nawachek nasema hihihiii
Shida ni kwamba wanataka watoe hela pasu pasu na mkewe afu bado anyenyekewe (mikazii yoote)
Wanashindwa kuelewa mwanamke Hamna Kitu kinachomuuma Kama hela afu ukute huyo kaka hahudumii mahitaji ya bidada ajinunulie mwenyew ,hapo lazima ataona mume mbinafsi

Aisee wakitaka warambwe mpaka unyayo,kupendwa mpaka ncha y'all unywele wahudumie familia yao bila kupiga jicho hela ya mwanamke..... Huyo dada atakupenda mpaka uhisi anaigiza


Kwa wanaosema kaanza jeuri sababu ya kuchepuka sio Kweli .... Mara nyingi mdada akiolewa kuchepuka Labda anatafuta amani ya moyo, attention, care.!!! Na si vinginevyo
 
Kabisa Mkuu mile bora akae nyumbani nijue moja kuliko ahamke asubuhi daily halafu asichangie kitu home no big no
Huu ujinga wa kusema pesa ya mwanamke ni yake na ya mwanaume ni ya familia ni mojawapo ya factor inayochangia umasikini kwenye familia nyingi za kiafrica.
 
Haaaa katito kazuri upo
Amechoka hayo maisha wenzake wanamaisha mazuri nyie ni mko pale pale wala hampigi hatua ndio maana anagomba na wewe wala huoni sasa ndio anareact wenzie wanaume zao kila mwaka wanajitahidi wanapiga hatua wewe hujitumi chapa kazi acha kujishaua jf ni ya vijana ambao hawana majukumu.
 
Nikupe uhalisia katika ndoa yangu! Hela ya mke wangu ni kwa matumizi ya sasa na ya kwangu ni kwa ajili ya development tu! Hata simu namnunulia ila chakula, mavazi ya familia including me juu yake! Likija suala la kujenga, hata kutengeneza gari lake ni juu yangu. Siamini naweza kuulizwa hela ya kitunguu! Kuhusu kufua nguo na kupika ni jukumu lake! Sijui anapata mshahara kiasi gani? Na mimi hajui napata nini kutokana na kusukuma mkokoteni stendi ya ubungo. School fees juu yangu! Kuna mgawanyo wa majukumu ila hawezi sema ujinga kuwa amesomeshwa na wazazi wake kwa ajili ya kuhudumia wazazi wake!!! Siku hiyo ntamweleza wakamuoe wao basi! Hata mie nilisomeshwa na wazazi wangu pia
Mgawanyiko wako ni sawa, sababu haupo nusu Kwa nusu majukumu ya mkeo ni madogo madogo na ya kinyumbani zaidi hivyo hata iwaje mke lazima ajiongoze
ila sio hadi Ada za watoto cjui Kodi ya nyumba mchangie pasu pasu hapo ndo Shida ya mleta thread ilipo
 
Kwani kabla ya dini kuja watu waliishije. He wangapi wamefunga ndoa makanisani mwisho wa siku zimevunjika. Ni jinsi mtakavyoweza kuishi pamoja na kuvumiliana. Utandawazi pamoja na haki Sawa ndio iliyoleta madhara
Ndoa hazifanani na shetani anafurahi mnapokataa kuamini zinaa ndio chanzo Cha uharibifu wa ndoa, zinaa inabadilisha nafsi ya mwanamke:hamjui nafsi ya mwanamke anayezaa nje ya ndoa huwa inapitia mawazo ya Aina gani hata watoto wanaozaliwa nje ya ndoa wanabeba dhambi ya zinaa asili ya kuzaliwa kwao. Watu weng hawajui asili ya kuzaliwa kwao kunawapa Aina ya mawazo na uchaguzi/maamuzi ya baadae. Kama mkristo mwenye hili suala dawa ni maombi tu mengine unayolinganisha hapa hayana tija, shetani aliakwa hapo.
Zamani wanawake walikuwa hawawezi kuzalisha Mali walivumilia hata yasiyovumilika kwa sasa mabadiliko hayakwepeki na shetani anayatumia.
Tunajifanya tunajua kutest mitambo ila ndo tunapopanda mbegu itakayotumaliza.
 
Mkuu sijakupata kusomesha watoto wake sio moja ya malengo ya mwanamke mkamilifu?
Tatizo wanaume huwa mnafikiria sana juu ya mambo yenu
Kama hapo umezungumzia mambo unayoyataka wewe!

Yeye je?
Inawezekana kuna matarajio alikua nayo kwenye maisha, wewe hujayafikiria ila umehitaji kutimiza yale yaliyo ya kwako!

Hapo anakua anakuona ni mbinafsi na yeye anajiona ni looser!
Jaribu kuongea nae juu ya malengo yake na yeye pia
 
Wanampotosha daaaah MPE adhabu Kali kabla ajapotea ukimchekea utavuna mabua
Then yeye kwa kinywa chake kaniambia sasa ameelimika wanawake wenzie wamemwambia pesa yao na ya mime in anga na mbingu yaani pesa ya mke in mke na mume ni ya familia KANIAMBIA KATIKATI YA MGOGORO
 
Kila mtu aki amua ku act ivo ndoa ina kwenda kuvunjika... sasa kama ata maji najipelekea bafuni mwenyewe.. nakua nime muoa kwa ajili gani? Au kunizalia watoto tu?
Ishi nyumba yenye maji ndani na heater ya maji iwepo, hutahitaji kupelekewa maji bafuni. Hamna ugomvi Tena 😎
 
Back
Top Bottom