Shikamoo wakuu,
Basi jana nikiwa nmejilaza kitandani kwangu naperuzi jukwaa la siasa humu si ghafla ikaingia text whatsup kuchek namba geni(imeandikwa nakusalimia tu,nikajibu asante nani lakini" kanijibu me mke wa nokia8 (he was my boy friend tulipokuwa chuo huyo nokia8) tukachana yeye akaoa mwaka jana bonge la harusi na mie nilienda cheza kwaito sana)mke wa nokia 8.
Najua ushawahi date na nokia 8 ina maana hamkuachana?
Mi nikamuliza kivipi sikuelewi?
Akanijibu nimeona chating zenu whatsup means mnakumbushiaga...
Me nikamwambia kama umeona chating kila kitu chajieleza mumeo ndiye anantaka me simuhitaji naheshimu ndoa yenu,nakupenda siwezi fanya hivyo mwambie mumeo aache kunisumbua"
Yule dada akanpigia simu
Nikapokea akaanza aisee kama mume nimepata sijui kama naweza"inavyoonekana huyo mke wa x wangu aliona mengi katika simu ya mumewe,mie nilichomwambia ndoa yenu ni changa sana kumbuka uliyoahidi kanisani siku ile,ukae utulie akanijibu siwezi!
Basi for sure nIlifili vibaya sana yani kama vile ndo mie yamenkuta alafu mie nikamwambia kama vipi mamii na wewe tafuta mchepuko ujitulize utajakufa siku siyo zako kwa presha,,hakunijibu
Sasa nyie wanaume niwaulize hivi mnakuaga mnalazimishwa kuoa?
Kabinti ka watu ndo kwanza kadogo kukaliza kila siku kama ulikuwa hujamaliza kuchovya hilo dunguso lako why uoe?
Mnaboa sana me nlichomshauri huyo dada nmemwambia nae atafute mchepukooo.