Mwanamke wa mithali 31
JF-Expert Member
- Apr 10, 2024
- 1,159
- 2,577
Nilikua nashida hii imenitesa MIAKA 2 maisha yangu yalikua ni kutumia bisacodl ilikua bila kutumia dawa bas siendi huko toilet,ilifika mahali nazo zikadunda, hapa ilibd niende hospital namshukuru yule dactar kwasababu hakunipima Chochote,akaniambia niludi nyumbani mimi ni mzima, akaniambia niseme mimi ni mzima kuanzia Sasa,Habari za usiku huu wana JF, naomba msaada wa haraka, mimi na mke wangu tupo mbali kidogo, leo ameniambia hajapata choo kwa siku saba, nimechanganyikiwa hapa sijui nifanyeje na tumbo linamuuma hatari
Toka mwezi wa 9 mwakajana napata choo kawaida,ila baada ya kubadlsha style ya maisha + vyakula na Kuna baadhi ya vyakula nimeacha kula kabisa
Dactar aliniambia hivi
Nile ugali wa dona mlaini sana,
Mboga za majani zizidi ugali, na maharage,
Nakunywa maziwa fresh au mtindi kilasiku,
katika Milo yangu mi 3 kwa siku m,Moja uwe matunda pekee hasa parachichi na papai,
Nisile wali,nisile vyakula vya ngano kama chapati,maandazi,tambi au chochote kinachohusu ngano,
Nakunywa maji mengi,
Kwahyo sasahvi napata choo kawaida,bila kutumia dawa tena