Mke wangu ana tabia za wizi na udokozi

Mke wangu ana tabia za wizi na udokozi

Hii kitu nishakihisi...mfano zamani nilikuwa nikinunua gunia la mkaa,linakaa hata miezi miwili,,, sasa hivi hata Mwezi haufiki vizuri gunia limeisha
Dadeki so anauza mkaa au !?

Maana hapo kwanza ncheke 🤣🤣
 
Hivyo vikoba anavyofanya,,bila mume kushirikishwa,,,hujui hapo kwa hamna upendo wowote,,,ndo maana anafanya mambo bila kushirikiana na mume?
Naam hiyo ni changamoto Ipo siku anaweza kukuibia millions of money mkaja kuuwana .


Kaa chini umkanye akishindwa kubadilika mfukuze
 
Mkuu Kuna m-pesa, Airtel money,mixx by yass, halopesa,Kuna bank, unaibiwaje Pesa?

Halafu jichunguze vzr usikute Kuna kautaratibu ulimwekea zamani ka kumuhonga na saiv umesitisha? Ujue wanawake huwa Wana kautaratibu ka kuflow na bit?
Embu jichuunguze kwanza ukishindwa fuata taratibu hizi
Kama mke wako ana tabia ya kuchukua hela kwenye wallet yako bila kukuambia, unapaswa kukaa naye chini muongee kwa utulivu. Mwambie wazi kuwa hiyo tabia inavunja uaminifu na si jambo jema katika ndoa. Mueleze umuhimu wa kuweka mipango ya pamoja kuhusu fedha ili kila mmoja awe na nafasi ya kujua na kupanga matumizi. Kama anachukua kwa sababu ya mahitaji au sababu nyingine, ni bora aseme badala ya kuiba kimya kimya. Mazungumzo ya wazi na heshima yanaweza kusaidia kurekebisha hali.
 
Kuwa na mkwe asiye ridhika ni changamoto nzito
Tunawaonea sana hawa mabinti, shida kubwa ipo kwa mama zao ambao wanawafanya vitega uchumi. Na akiwa binti ni mtoto wa single mother, chamoto itakipata. Mifano ni mingi kwa hawa mabinti wa JF
 
Tunawaonea sana hawa mabinti, shida kubwa ipo kwa mama zao ambao wanawafanya vitega uchumi. Na akiwa binti ni mtoto wa single mother, chamoto itakipata. Mifano ni mingi kwa hawa mabinti wa JF
Mwanamke wa hivyo Kaa chini Kisha umpe Somo afuate muongozo wako mueleweshe namna sahihi ya maisha jinsi ilivyo , Unakuta binti ana mama yake mwenye miaka 45s lakini eti huyo mama hataki kufanya kazi ana Kaa anamtegemea binti yake wakati Bado ana nguvu nyingi tu za kutosha unachopaswa kufanya mpe lecture binti kwamba katk Umri alionao anapaswa kujikita zaidi kutengeneza maisha yenu ( maisha ya family yake)

Baba na mama wanapaswa kupewa support pale tu endapo patakuwa na sababu yenye tija haswaa ya kufanya hivyo Kwa maana umri wao Bado unanguvu so wanapaswa kujituma nasio kukaa kuomba omba Kwa watoto as if hao wazazi ni vilema au ni wazee ,

Binti kama nimuelewa na ana akili atabadilika ila kama nilikilaza hato kuelewa so utakuwa huna budi Cha kufanya ni kumpiga chini ukishindwa kumpiga chini kitakacho kukuta Usije kulaumu watu
 
Nampa,,,hata matumizi ndani najitahidi kila kitu kimo ndani
Kaa nae chini umuulize shida iko wapi halafu umwambie asiibe na akiwa na shida akuambie. Ongea nae kirafiki sana na hata mwisho wa maelezo yake usipaniki bali mezea. Akiendelea kuiba uje utuambie
 
Mwanamke wa hivyo Kaa chini Kisha umpe Somo afuate muongozo wako mueleweshe namna sahihi ya maisha jinsi ilivyo , Unakuta binti ana mama yake mwenye miaka 45s lakini eti huyo mama hataki kufanya kazi ana Kaa anamtegemea binti yake wakati Bado ana nguvu nyingi tu za kutosha unachopaswa kufanya mpe lecture binti kwamba katk Umri alionao anapaswa kujikita zaidi kutengeneza maisha yenu ( maisha ya family yake)

Baba na mama wanapaswa kupewa support pale tu endapo patakuwa na sababu yenye tija haswaa ya kufanya hivyo Kwa maana umri wao Bado unanguvu so wanapaswa kujituma nasio kukaa kuomba omba Kwa watoto as if hao wazazi ni vilema au ni wazee ,

Binti kama nimuelewa na ana akili atabadilika ila kama nilikilaza hato kuelewa so utakuwa huna budi Cha kufanya ni kumpiga chini ukishindwa kumpiga chini kitakacho kukuta Usije kulaumu watu
Kubadilisha mtu fikra za mtu ambaye amezaliwa na kulelewa na jamii tofauti ni kazi kubwa. Mfano, mabinti wa kichagga hutumiwa na ndugu wa kiume kuwafanya kitega uchumi chao. Kwa kuwafunza tangu wakiwa wachanga kuwa asimwamini mume, anaweza kufukuzwa wakati wowote. Hivyo lazima ajenge nyumbani kwao. Kuwa damu ni nzito kuliko maji. Ingawa akipata shida huwa wana dhulumiwa tu.

Njia rahisi ambayo tumetumia na inafanya kazi, ni kuhakikisha mkeo anapata kipato na humuingilii katika matumizi ya kipato chake! Hata wewe hakuingilii katika matumizi ya kipato chako.

Kubaliana wote majukumu Yenu tangu mwanzo wa safari.

Usiwe na wivu wa kirejareja maana akikosa hela anatumia k kuzisaka hasa akiwa binti wa kichagga
 
Acha ubahir mpe mkeo pesa yake ya matumiz binafs na ya familia uone kama atadokoa tena.
Mwenzio anajua hizo ni pesa zenu wote coz nyie ni mwili mmoja.
 
Kama siyo kicheche tulia broo
Sahih, Mimi mwenyew huwa naona Tabia mbaya zaid kwenye ndoa ni Ukahaba na kutoa au kugona kubeba mimba labda na ile ya kujarb kukuua.
Hizo zingine zinavumilika hata Mama zetu wanazo.
 
Huyo siyo Mwizi ametumia vilivyo vyake!
Katika ndoa,Mali ya Mme ni Mali ya Mke! Hali kadharika Mali ya Mke ni Mali ya Mme. Wana milki pamoja.
Kwa hiyo hapo Mke akikuta pesa kwenye Wallet akatumia,ametumia Mali yake,anachotakiwa kufanya nikukupa taarifa tu kwamba amechukua kwa matumizi ya kifamilia.
Angalizo:
Usimfiche Mke mapato! Pangeni bajeti pamoja.
Akikueleza matatizo yake msikilize usipuuze.
Ni hayo tu kwa uchache!!
 
Sasa si akuombe, au na wewe ukiombwa unampiga kalenda sio za nchi hii
 
Mwambie kazi yako ili ajue , sio kumdanganya kumbe unapokea laki moja kwa mwezi mwambie ukweli kazi yako.
Mwanaume yoyote pesa zake zipo kwenye matumizi haijalishi anafanya kazi gani.
Wewe angalia, hapo nyumbani wote mnamtegemea mtu mmoja (mwanaume) alishe familia, awatibu, alipe kodi, ajenge nyumba n.k ndiyo maana familia nyingi mwanaune akifa mambo huyumba
Unafikiri sisi wanaume hatupendi pesa zetu?
Kuna wakati wanaume huwa tunaangalia matumizi ya msingi tu Unaomba hela ya kununulia nguo ndani ya siku 15 unatakiwa ulipe kodi. Lazima unyimwe tu
 
Huyo siyo Mwizi ametumia vilivyo vyake!
Katika ndoa,Mali ya Mme ni Mali ya Mke! Hali kadharika Mali ya Mke ni Mali ya Mme. Wana milki pamoja.
Kwa hiyo hapo Mke akikuta pesa kwenye Wallet akatumia,ametumia Mali yake,anachotakiwa kufanya nikukupa taarifa tu kwamba amechukua kwa matumizi ya kifamilia.
Angalizo:
Usimfiche Mke mapato! Pangeni bajeti pamoja.
Akikueleza matatizo yake msikilize usipuuze.
Ni hayo tu kwa uchache!!
Usije ukajidanganya mali ya mwanamke ni ya mwanaume😀😀😀😀
Usihalalishe wizi, subiri mkeo kaweka pesa ukachukue kisa ni zako😀😀😀😀😀
Kama ni mwili mmoja kwanini amtumii simu moja? Kuna wengine hawashiki simu za wapenzi wao😀😀😀
 
Back
Top Bottom