Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Huyo Mke ni Shetani na hakupendi.

Utasadiki maneno yangu siku utakapokuwa huna tena msaada kwake kiuchumi, aidha ukiugua na usiweze tena kuhudumia familia ama siku yeye mwanamke atakapokuzidi kipato...
 
Ukimfukuza mke wanao watapata shida.
Ukimuhamisha mtoto ataishi kwa masononeko sana.
Ukiwaacha wote hapo mtoto ataendelea kuteseka coz huyo mkeo ni pepo hata umkamye hatabadilika bali atabadili tu mbinu usijue.

Na je ukimuhamisha mtoto una uhakika moyo wako utaendelea kumpenda huyo mkeo?

Unaweza kweli hata kusimamisha kwa mwanamke anayevunja mtoto mguu kwa tofali?UNAWEZA?

Alichofanya kwa huyo mtoto ni red flag ya mambo mengi sana ila sikiliza moyo wako katika kufanya maamuzi sahihi.
 
Ndiyo wanawake mlivo mna ubinafsi na uchoyo....
 
Kama mkeo hamtaki huyo mtoto wa miaka nane, hata mtaka hata ufanyeje. hapo ni kuchagua mkeo au mtoto wa dada yako.

Ukichagua mkeo utakuwa mpumbavu ni sawa na kumtoa kafara huyo mtoto na ukimchagua huyo mtoto utakuwa umeamua kuvunja ndoa yako. hapo wa kuchagua ni wewe.

ni upumbavu kumtafutia sehemu nyingine huyo mtoto akakae wakati kwako papo na ndugu wa mkewako wapo, mimi naona tatizo ni wewe sababu mkeo anaongea upuuzi mbele yako.

Mkewako anatakiwa kuwa na nidhamu ya hali ya juu, nidhamu haiji tu from no where, nidhamu inatengenezwa. fanya kuitengeneza.


Ingekuwa ni mimi ningemuhamisha huyo mtoto hapo ila ntabalance equation ndugu wote wa mwanamke wanafungasha virago na huduma nakata. mtoto wa dada yako, mama yake katangulia mkeo ndo alitakiwa kuwa mama yake.
 
Ndiyo wanawake mlivo mna ubinafsi na uchoyo....
Nakuheshimu mkuu ila umenikosea sana kunijumuisha na huyo pepo mgonjwa wa akili.

Mimi sio malaika ila inataka uwe na kiwango kikubwa cha roho mbaya ili uweze kuchukua tofali na kumpiga nalo mtu haijalishi ni mtoto au mtu mzima.

Kwanza mimi mtoto atanishindaje hadi nimchukie?Huyo hata kulea halijui.
Mimi hata uniletee mtoto bandidu kiasi gani nitamshape kwa njia sahihi hadi awe aina ya mtoto tutakayependana..
Na huo uchoyo sasa mtoto wa 8 yrs anamalizw nini?

NIKOME hunijui usinifananishe na mianamke yenu ya hovyo
 
πŸ˜…πŸ˜…πŸ˜… pole na samahani, nimeelewa wewe sio kama wale.
 
Wanawake tuna ubinafsi ule wa kuzaliwa nao sema kuna wengine maisha yanafunika hiyo roho, wengine ndo kama hivyo wanajiweka hadharani km mkeo,

Hatokaa ampende huyo mtoto hata ufanye nini, kwanza ndo itamuongezea mateso, cha kufanya kata misaada uliyokuwa ukimpa kwa ndg zake, funga kamera upate ushahidi wa manyanyaso yake kwa huyo mtoto, mpeleke kwenye vyombo vya sheria, huyo ni kiburi pambana nae kijeuri jeuri ukilegeza tu huyo mtoto utamkuta maiti siku moja
 
Kila mwanamke ana roho nzuri hadi utakapoamua kuishi nae πŸ˜‚
 
Wanawake wana choyo ya asili
 
Kusanya ushahidi wa kutosha kisha nenda ustawi wa jamii,kapeleke taarifa na ushahidi huo, nao watafika eneo hilo na kufanya uchunguzi ,watamuita na kumuhoji ,na kufunguliwa mashitaka, hiyo Ni njia sahihi ya kumuondoa, au nenda kwa court kaombe taraka.

Kimafia rudisha kwao akafundwe malezi, akigeuka wahuni wameshawahi siti ya mbele
 
Hapo hauna mke ndugu yetu.
Ikitokea umedondoka gafla uko kitandani huyo mwanamke atakufanyia manyanyaso hujawai ona.
Kama mama ako yupo mpeleke huko
 
Mjomba ni mama , unaruhusu vipi mkeo kumtesa mwanao
 
Au ampeleke mtoto kwa Baba yake mzazi, au kwa mashangazi zake!alafu inakuwaje mnagawana watoto wa.Dada yenu wakati baba au baba zao wapo!?
 
Au ampeleke mtoto kwa Baba yake mzazi, au kwa mashangazi zake!alafu inakuwaje mnagawana watoto wa.Dada yenu wakati baba au baba zao wapo!?
kuwepo sio issue, nadhani uwezo/kipato na anayetaka kulea, ndo maana wakagawana watoto.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…