Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Mwanaume unatakiwa kua na authority kwako, mi siwezi kukaa na mwanamke eti kitu kidogo anatishia aende kwao, ungemuacha aende huko na usimfate mpaka arudi mwenyewe, la sivyo ashajua udhaifu wako, Kila mkigombana atakua anatishia kwenda kwao

Kuhusu huyo mtoto, kama Kuna ndugu mwingine anaweza kukaa nae basi fanya mpango huo wewe ugharamikie Kila kitu kwa makubaliano kabisa, kuanzia mavazi,elimu,chakula,matibabu etc... Mtoto kukaa sehemu anaponyanyaswa huathirika physiological.... Mnamletea shida tu za badae huyo mtoto

Hilo lishemeji ulilitoa wapi?
Mkuu umesema kila kitu
 
Aseee,hivi hawa wanawake wana pepo gani?apumzike kwa amani dada
 
😂😂😂 umefanya nikumbuke ya home kwangu.!!
Nna vijana wa dukani kuna siku niliwarekodi walichokuwa wanaongea sikutaka tena kuwafatilia nahisi ningekufa na presha.!!
Huku nyumbani ndio usiseme nna kijana wa kiume alimshawishi dada wa kazi akubali wanaume wanaomuita ili awachune wapate pesa.!! Nilipiga hiyo siku, halafu baadae huruma ikanijia nikaanza kumbembeleza.!!

Dada na kina kaka wa dukani nikianza kuongea mpk nachoka, kuna muda nasema au mnaniona mdogo ndiomana mnanidharau?? Au kwa vile sina mume hamnisikilizi?? Ila ndio hivyo nawapenda na jana wote tumeenda kutazama mpira wa Simba na Yanga. Tuko na furaha.!!

Sasa huyo mwenzetu ataweza kuishi na watu wengi ambao sio ndugu zake km sisi??
Mara nyingi hao wa hivyo wachoyo na waficha vyakula, hao km unaenda kusalimia utamuona kanuna.!!
Yaani huyo akikutana na hawa Genz atatembea na MK47😁😁 maana ni pasua kichwa lakini tunaishi nao mimi wa dukani mmoja huyo anajulikana na wateja kuliko mimi ila ni Genz yaani ni heka heka
Yaan mtoto wa miaka nane anabeba tofali nimetafakari sana
All in all huyo dada ana majini
That is beyond human being
 
Achana nae huyo sio binadamu ni katili Sana mtoto wa miaka nane si Malaika huyo ana shida gani Anza kukataa kumusaidia mtoto wa kaka yake na nduguze ila ushauri wa Bure Achana nae ushauri wa kuwa umpeleke boarding Achana nao bado utakuwa hujatibu tatizo kwani hatorudi je nduguzo hawatokuja kwako usiangalie tu Tena anakutishia kuondoka usijipe stress za Bure kwa huyo jambazi achana nae Achana nae
 
She/He is only 8years jamani.
Dah.. dah kwa umri anahitaji malezi ya ndugu wa karibu ili kimjenga kwenye misingi Bora...
Lakini kama haiwezekani Bora apekekwe tu huko...mbn Kuna shule zinapokea tu...
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni jumamosi na jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani
Mkuu, Sijui kama utanisikiliza!
Tuliooa ni kama tunapata kapicha flani hivi.

Kuna watu wanakushauri umpige mkeo, Hapana.
Kuna watu wanakushauri umfukuze mkeo, Hapana.

Njia nzuri ya kulimaliza hili ni kuzungumza, mweleze mkeo hayo matendo anayofanya ni anawafanyia watoto wake pia.
Watoto wenu hawako salama hata kidogo kwa kutesa watoto wa wenzio.

Mwanamke kuwa na roho mbaya ni jambo la kawaida kabisa.
Hapa nakushauri uwe Kiongozi.
Ongoza hilo gurudumu la familia yako kwa Amani, umejua sasa hali ilivyo, inapaswa kukoma.

Nakwambia tu wanaoathirika zaidi na hiyo torture ni watoto wenu wenyewe!! Huyo mtoto wa Dada yako, anadhurika mwili tu.
Wakwenu waathirika in all perspectives!!

My brother be a man!! 💪
Play your part.
Tupunguze watoto wa Mitaani!!
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni jumamosi na jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani
Tumia madaraka yako vizuri mkuu, usiruhusu huyo mkeo akupande kichwani.
 
Back
Top Bottom