Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Nimesomea ujinga 🤣🤣
 
Huyo mwanamke ana roho mbaya sana aisee ila ndivyo wanawake wengi walivo ukiona nduguzako hawapendi hata kuja kukusalimia ila ndugu wa mkeo wamejaa hapo kwako na wanakaa ujue umeoa shetani
 
Hilo ndio chaguo lako na ushazaa nae watoto wawili utakapomuacha fikiria mustakabali mzima wa watoto wako na wewe , Kama unaweza mtafutie shule nzuri ya boarding akakae awe anakuja nyumbani likizo tu. Na wewe uanze kuweka mipaka Kwa ndugu zake
Huyo hafai iko siku atamshindilia bisu mana anaroho kama jambazi...anampigia mtoto mdogo tofali hiyo n8 roho mbaya aliyonayo mtu mzima habadiliki
 
Mwanamke asiyeijali familia yako hafai hata kidogo.
Siku hata wewe usipokuwa na uwezo kifedha/ kumuhudumia basi jua utatendewa unyama pia
 
Binafsi naamini huyo mwanamke atakuwa ameshafanya matukio mengi tu yanayofanana na hili, huyo anaonekana ana mkono wa kupiga na mdomo mchafu... yes, mtu mgomvi siku zote lazima awe na mtu wa matusi matusi.

Na hii tabia mbovu jamaa mwenyewe ndio atakuwa ameilea kwa kupuuza zile redfrags mwanzoni mwa mahusiano yao... yes, mwanamke mchoyo na mbnafsi asiyependa ndugu wa mume huwa anaonekana tu tangu awali.

Kitakachofuata endapo kma huyu jamaa ataendelea kubaki na huyo mwanamke ni dharau za wazi wazi na siku ikitokea akapitia tu changamoto zozote za kiuchumi kiasi cha kushindwa kutoa mahitaji hapo nyumbani na kumsomeshea hao ndugu wa mkewe, basi utakuwa ndio mwisho wa hiyo ndoa yao.

Kuhusu hilo tukio la muhasibu wa HESLB kwakweli inasikitisha, vijana wengi wanaangamia kutokana na machaguzi mabovu ya mke.... na bahati mbaya sana hata wakija kugundua mbeleni huyo mke waliyenaye hafai, wao wanaamua kukaza roho tu na kuendelea nae na matukio yake ndio tunakuja kuskia haya.
 
Nina kanuni za kusikiliza pande mbili linapokuja suala la migogoro ya wanandoa, lakini kwa kesi hii namna ilivyo, ninasikiliza upande mmoja tu na kushauri.

Huyo mamsap wako ana roho ya kuku jike ama ng'ombe ya kupenda watoto wake tu, ana tabia ya kinyama.

Kama umeshaelewa tabia yake halisi, basi na wewe mme badilika namna ya kuchunga na kuilinda familia yako.

Ingawa unashinda kazini, jipe jukumu la ufuatiliaji wa karibu wa kila siku usio na kikomo.

Maelezo yako yamejitosheleza, huyo mtoto ni wako 100% hauna pa kumpeleka, kumuondoa hapo nyumbani kwako kwa ajili ya mkeo ni kukikimbia kivuli chako ama kutishwa na kinyago ulicho kifinyanga kwa mikono yako.

Nimeona wadau wakishauri utafute pa kumpeleka ama boarding school!

Kumpeleka boarding ni mipango, lakini aende kwa heri na si kwa shinikizo la ukatili wa mke.
Mume utakuwa umeshindwa kuyatumia madaraka yako kama kichwa cha familia ipasavyo.

Kwa ufupi toa maelekezo kwa mkeo na akuelewe namna ya kuwalea watoto bila chuki.

Na pia aelewe kwamba, mtoto anayepata hifadhi ya malezi yenu hapo nyumbani, si mtu tegemezi wa muda wote maishani mwenu, awe wenu wa kuzaa ama yeyote mnayemlea ni wa muda mfupi, baadaye atajitegemea na maisha yake, hivyo kaeni nao kwa upendo, maana mtapozeeka nao watawasaidia.

Maana ya Mungu ni mengi, je ukipoteza maisha leo, huyo mwanamke anaweza kuilea kwa amani familia utakayokuwa umemwachia?

Kama hataweza kukuelewa na kukutii, basi atakuwa ni sikio la kufa lisilosikia dawa.
 
mpeleke kituo cha watoto yatima ! huyo mkeo n shetan
 
Nimeipenda hii
 
Huyo mkeo anaroho mbaya,Huyo ni kama mwanao.wengine kama Mimi nimelewa na mke wa mjomba hadi nina familia kwa Sasa na watoto wa huyo mjomba niliwalipia ada ya high school!Kaa nae mkeo Aacha roho mbaya .
 
Yes, Ulifanya uamuzi wa maana sana family is everything na usiruhusu mpuuzi yeyote anayeonesha kutojali kuhusu familia yako adictate maisha yako.

Huyo mchumba wako si ajabu wakati anakambia hivyo siku za nyuma yake alikuomba umpe hela akachangie harusi za mashoga zake kwa kisingizio cha kwamba na wao wangekuja kuwachangia kwenye harusi yenu.
 
Nashauri jamaa ampige mkewe kwa tofali mguuni kama mtoto alivyofanyiwa... Ili mkewe ajue uchungu wa mfupa wa mguu kusogea na kuvalishwa P.O.P.. Akili ya huyo mwanamke itakaa sawa na kuheshimu watoto wa wanawake wengine.
 
Nashauri jamaa ampige mkewe kwa tofali mguuni kama mtoto alivyofanyiwa... Ili mkewe ajue uchungu wa mfupa wa mguu kusogea na kuvalishwa P.O.P.. Akili ya huyo mwanamke itakaa sawa na kuheshimu watoto wa wanawake wengine.
Akiondoka atampgiga sumu
 
Nakubaliana na wale wote ambao wamasema huyo umuhamishe hapo,tena fanya fasta,,hali ilipo fikia kuna makubwa yanakuja,usije kusema ningejua

Hapo ni hayo machache uliyoona na kusikia,je ni mangapi hujasikia?

Hapo huyo mkeo hata umwambie vipi hatobadilika,litakuja kichwani kwake,huyo mtoto na yeye nani ni bora kwako?

Natamani na ninakuomba mhamishe huyo malaika wa Mungu,mhudumie sehemu nyingine ambayo atapendwa na kuthaminiwa,na hakikisha unampeleka kwa mtu sahihi

Nimeguswa sana,je usingemsikia usiku huo unadhan ingekuwaje kwa huyo mtoto.

Nawapenda watoto sana,kwahiyo huwa nahumizwa na habar kama hizi

Bro tafadhali muhamishe huyo mtoto
 
Hii ya kutishia imenikumbusha mshikaji wangu mmoja,mke mwingine wa baba yake alitishia kuondoka,baba yake akamwambia nakuwekea mafuta kwenye gari kama unataka kuondoka,mke kwani aliondoka? Alijua mwamba hataki ujinga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…