Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Huwajui Wanawake Mkuu...!

Kwa jinsi huyo Mwanamke alivyo hawezi kujenga Upendo na huyo Mtoto hata Kwa Bunduki...!

Just imagine na huyo ni Mtoto wa Marehemu Wifi yake, vipi kama ndo ingekua Jamaa alizaa nje ya Ndoa ama kabla ya Ndoa, si angeua Kabisa....!

Ni Ngumu kweli kumwacha Mke Kwa sababu Hiyo, ila ningekua Mimi....!

Ningemwambia Mke Kwa sababu ameshindwa kuishi na Mtoto wa Dada yangu ambaye ni Marehemu.
Na Kwa vile Mimi naishi Vizuri na Ndugu zake ama Watoto wa Ndugu zake ikiwepo kuwalipia Ada...! Na nafanya bila Kinyongo...!

Namwamisha huyu Mtoto hapa Nyumbani, na pale ninapomwamisha huyu Mtoto hapa Nyumbani, na yeye atafute pa kuwapeleka Ndugu za Mke wake,, Yani sitaki kuona Mtoto wa Ndugu yeyote hapa Nyumbani, na Huduma ya Ada nasitisha, sikuoa kuja kkutatua matatizo ya Ndugu zako, wakati wewe umeshindwa kuishi na Mtoto wa Marehemu Dada yangu...!

Huo ndo ungekua Msimamo, na siku namuondoa Mtoto wa Ndugu yangu ndo Siku Watoto wa Ndugu ya Mke wangu nao wataondoka...!

Na itakua marufuku kuishi na Watoto wa Ndugu zaidi ya Wageni wataokuja na Kukaa siku mbili ama tatu.

Kama ataona Utaratibu ni Mgumu, basi aondoke na Watoto wa Ndugu zake.
 
Nimeipenda sana hii
 
Unabishanaje na mtu ambae haogi kichwa mwezi mzima?
Fukuza hiyo mbuzi ikikuletea ujuaji Kwan hajui wapo wengi mtaani wanalilia ndoa?
 
Pole sana mkuu.

Huyo mkeo ni mshamba sana, ana roho mbaya kuzidi shetani, ni mshenzi kuliko ushenzi wenyewe.

Anastahili kuwepo ndani sasa hivi maana ana kesi ya kujibu.

Madhara ya kutokea familia masikini na kujipata kidogo ndio hayo, mkeo anaona keshamaliza maisha kabisa.
 
Halafu kaka zetu kuna muda mnatufelisha sans, hiki kitu sio cha kuomba ushauri!!

Wewe ni Baba, kichwa cha familia kuwa na maamuzi ya kiume
 
Mpeleke shule ya boarding mtoto wa dada yako mambo yasiwe mengi.

Ww ndio mwanaume kuwa na sauti mwanamke mwenye roho mbaya hivyo hana tofauti na mchawi.
 
Fukuza kunguru .
 
Nini?? Huyo mwanmke mbona muuaji!!
Hivi unaweza kumpiga mtoto na tofari?
Kaka huyo mkeo hakufai anaweza kumuwekea hata sumu huyo mtoto.!!

Ninavyopenda watoto halafu nikisikia kesi km hizi naumia sana.!
Hebu kuwa na maamuzi ya kiume, mwambie km anaenda kwao aende tu.!
 
Huo ni ukatili dhidi ya mtoto kamripoti kituo cha polisi dawati la watoto na jinsia.

Ama mpeleke muonye mke wako kwamba akiendelea na ukatili dhidi ya huyo mtoto utamripoti kwenye mamlaka ya serikali kama ustawi wa jamii ili achukuliwe hatua nadhani ataogopa na ataacha ukatili.

Usishuhudie ukatili ukifanyika ama hata kwa kuhisi tu na sawa na wewe kushiriki ukatili huo kama hukutoa taarifa.
 
Mkeo ni mjinga sana ashawaza siku na yeye akitangulia mbele za haki watoto wake nao wateswe hivyo.

Kuna WANAWAKE ni wapumbavu sana kwenye hii Dunia, akili zao huwa zina funza.
 
Dah yaani
Aisee nina mtoto wa mume wangu anakujaga likizo umr wa miaka 12
Aiseee sionagi baya lake japo wanaokujaga ndo wanasema mtoto mkubwa hivi hajui hata kutoa chombo
Akimaliza kula,naonaga sawa tu maana hata wanangu naenda nao hivyo hivyo
Nasema kama wa kiume hawajui hizo kazi why mdogo hivi kisa wa kike awe anafanya hizo activities
Mi napenda watoto wa kike sana
Wa ndugu zangu natamani kuja kumchukua ni ishi nae kabisa

Aisee mtu anae enda physical kwa mtoto wa miaka nane si ni la pili??
Kwa nini anamkokota namna hiyo??
Dah aiseee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…