Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Mke wangu anamtesa sana mtoto wa marehemu dada yangu

Akirudi likizo si ndio atampa sumu kabisa.
Vitafunwa vimesababisha apasuliwe mguu, na tumeambiwa shule haendi ili awe mtumwa hapo nyumbani.
Bahati mbaya jamaa kaoa shetani maana hata yeye anatetemeshwa.

Nilishawahi kupiga kofi mke wangu miaka 27 iliyopita mpaka hivi leo analikumbuka.
Akirudi kutoka boarding ndo atajua atumie mbinu gani ili kumsaidia huyo mtoto aishi kwa amani hapo nyumbani. Ila kwa sasa atumie hiyo njia ya haraka ili kumuokoa huyo mtoto asizidi kuumia na kuharibika kisaikolojia zaidi
 
Akirudi kutoka boarding ndo atajua atumie mbinu gani ili kumsaidia huyo mtoto aishi kwa amani hapo nyumbani. Ila kwa sasa atumie hiyo njia ya haraka ili kumuokoa huyo mtoto asizidi kuumia na kuharibika kisaikolojia zaidi
Umeeleweka mkuu.
 
Pole sana ndugu,
Wanawake wengi wana roho mbaya sana naweza kusema hivyo,nimeona wengi wanaoishi na watoto wa watu ni mateso matupu,mimi nikiwa mmoja wa niliopitia changamoto hiyo miaka hiyo,

Ikibidi aende kwao ama akatafute pa kuishi kuliko yote hayo,kuna wakati mwanamke anatakiwa kujua sio kila kitu anaweza kuzungumza mbele yako,
Kama kuna kitu mke wangu hatowahi rudia maisha yake yote ni kutishia kwenda kwao.
 
Wanajua ndugu ni wa upande wao tu,
Ushauri : kumtafutia mahala pengine/kwa mtu mwingine ni tatizo labda bibi yake
Ukiweza mpeleke shule ya kulala likizo kwa bibi
 
Yaani huyo akikutana na hawa Genz atatembea na MK47😁😁 maana ni pasua kichwa lakini tunaishi nao mimi wa dukani mmoja huyo anajulikana na wateja kuliko mimi ila ni Genz yaani ni heka heka
Yaan mtoto wa miaka nane anabeba tofali nimetafakari sana
All in all huyo dada ana majini
That is beyond human being
Mimi wakaka nilikuta wanaongelea madem zao, kuna mtu akaniambia hapo pesa zako ndio zinahonga hao madem 😭😭
Mkinga pesa inavyoniuma mbona niliacha kurekodi nisije kukutana na mazito na hao ndio wananisaidia kiasi kikubwa hapo shop.!!

Huyo mwanamke mwenzetu kwa kifupi roho mbaya yake imepitiliza anaweza kuua km huyo mumewe asipofanya jambo.!!
 
Pole sana ila huyo mke ana roho mhaya sana
Nashukuru mdogo wangu ana msimamo alimuambiaga mkewe bora niishi single na wanangu kuliko kukaa na mke asiyependa watoto wa dada angu...!!

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ongea na mkeo umuulize mtoto ana shida naye gani labda Kama ana muona jeuri na Kama kuna changamoto nyengine muitatue
Na umsisitize awe na upendo kwa huyo mtoto,inawezekana akabadilisha tabia yake
Ila ikishindikana chagua kumpa likizo mke au kumuhamisha mtoto
Jani jeuri ndo ampige na tofali huo ni ukatili mnoo
Wa kwake anaweza mpiga hvyoo kweli
Mtoto wa miaka mi 8?!

Hilo ndo limeonekana yasioyoonekana je
Huyo mwanamke ni mnyanyasi mnooo
Ana bahati kapata mume mstaarabu angekuta kichaa mda huu yuko kwao

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Mwanamke mkatili wala sio wa kumchekea!
Unampigaje mtoto na tofali?
Si uuaji huo?

Wanawake baadhi yetu ni kama mapepo vile , mxiiiiiiiieee!
kutesa malaika wa watu hana mama pengine wala baba, af we unalala ndani sijui wanawazaga nn!
BEEN AN ORPHAN so najua hii hali inavyoweza kujeruhi kabisa nafsi kiukweli!
Yaani nimeumia mnoo
Haya hvyo huyu jamaa mpole sana aseehh au ndo anampenda mkewe kupitiliza anahisi akiondoka hapati mke mwingine ila honestly mwanamke sio huyuu ana roho ya kichawi

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tukiacha unafiki hii ndio tabia halisi ya wanawake ila kwa juu ya uso watajionesha ni wema sana na wanaonewa ila mwanamke hawezi kuishi na mtoto hata wa miaka 2 kama hawana dam moja
 
Kama mjuavyo sisi wanaume mara nyingi ni kuamka asubuhi na mapema na kuondoka, na kurudi ni usiku, muda ambao Mimi nashinda nyumbani ni Jumamosi na Jumapili.

Usiku wa kuamkia Jana alhamis mtoto wa marehemu dada yangu alianza kulia sana chumbani, akalia sana mpaka ikabidi niamke niende chumbani kwao Ili nione Kuna nini, nilivyo fika nilimkuta kakaa chini huku wenzie wamelala, nikamwuliza Kuna nini? Akanijibu mguu unamuuma sana, ikabidi niuangalie mguu, aisee nilijikuta nalia na Mimi, mguu ulikuwa umevimba sana, nikamwuliza ilikuwaje? Akaniambia mke wangu alimpiga na kipande Cha tofali.

Pale pale nikaenda kumwamusha mke wangu kumwuliza hiki alicho fanya, akawa amekataa na kuanza kumfokea mtoto eti anataka kutugombanisha, Nikasema sawa, ila kwanini mguu unafikia hatua hii ina maana alikuwa hamuoni? Akawa amezidisha hasira eti natafuta sababu kama nime mchoka niseme arudi kwao, nikaona maneno yasiwe mengi ikabidi nimpakie mtoto kwenye gari nikampeleka hospital usiku ule ule, iligundulika kuwa mfupa wa mbele wa mguu uliachia kidogo akafungwa P.O.P.

Nilivyo rudi nyumbani asubuhi Jana hiyo asubuhi ilibidi nishinde nyumbani, ikabidi nifanye upelelezi mana Kuna vitu niliiona haviko sawa, ndo mpangaji wangu mmoja akaniambia kama Kuna sehemu naweza kumpeleka huyu mtoto Bora nimpeleke vinginevyo itatokea hatari kubwa, mtoto anateswa mno na mara nyingi shuleni haendi, na siku alivyo mpiga na tofari alikuwa amemtuma vitafunwa asubuhi akachelewa kurudi, tofari alimpiga mbele ya wapangaji siku tatu nyuma, na siku zote hizo hakwenda shule.

Nawaza mtoto nimpeleke wapi, marehemu dada yangu baada ya kufariki 2022 tuligawana watoto sisi ndugu zake, hili tukio limefanya nimkumbuke marehemu dada yangu aliye fariki Kwa maumivu makubwa ya kansa akiwa mikononi mwangu, nawaza Bora kuachana na mke wangu kuliko kuacha mtoto wa dada ateseke ntakuwa nimemkosea dada.

Mke wangu alimchukua mtoto wa kaka yake anaishi hapa na anaelekea kumaliza form 4 Kwa Gharama zangu, ila mtoto wa upande wangu kashindwa kumlea Kwa miaka miwili tu,hii ni sawa kweli?

Halafu baada ya mtoto kuniambia kuwa yeye ndo alimpiga, muda wote saivi ni kumuangalia Kwa jicho Kali sana na kumwambia eti ametumwa aje kutugombanisha, mtoto wa miaka 8 anawezaje kutugombanisha?

Sikuwahi kumfikiria mke wangu kuwa anaweza fanya hiki alicho fanya kutokana na mambo ninayo wafanyia ndugu zake, na ndiyo maana huyu mtoto nilimleta hapa Kwa kuamini atamsimamia kama mwanae na kama anavyo wasimamia watoto wetu wawili.

Mpaka naogopa kwenda kazini na huyu mtoto kumuacha hapa, nahisi atampiga Yani

MKUU
1. MWANAMKE ANAYOYAFANYA KWA MTOTO WAKO WA DADA NI ALAMA ZA KULE UZEENI ATAKAVOKUFANYA
2. FUKUZA HUYO MWANAMKE TAFTA MWANAMKE ASIE NA WAZAZI OA
3. USITHUBUTU KUMUACHA MTOTO HATA DAKIKA MOJA NA HUYO MAMA UTALISHWA HATA SUMU
 
Mpeleke boarding school
Hapana huo utakuwa ujinga, huyo mwanamke anatakiwa awe somo kwa wanawake wengine;

1.Aende kwao kwa miezi 6
2.Asiondoke na mtoto yoyote
3.Kurudi inabidi kifanyike kikao kikubwa cha wazazi wa pande zote.
4.Mda wote wa miezi 6 hakuna kuwasiliana nae.
5.Akikaribia kurudi funga kamera nyumbani.
6.Usimuamini tena kuhusu huyo mtoto.

Yote kwa yote jamaa yangu acha ubwege, ishi kiume,simamia nyumba yako kama baba na dogo asiende popote hakuna boarding wala kwa ndugu huyo bado malaika hakuna kumpeleka popote.
 
Back
Top Bottom