Mke wangu ananidharau nifanyeje?

Mke wangu ananidharau nifanyeje?

hili ndio tatizo la kutaka fananisha maisha ya wengine na yako,miaka yote mmeishi wote ulikuwa una jiwekea maji wala hauja ona taabu leo umekaa kijiweni umeskia wenzako wana pelekewa maji na kufuliwa boxer na wewe unataka, kumbuka hata mbuyu ulianza kama mchicha na samaki mkunje angali mbichi. Mkeo ulitakiwa mfundisha toka mko kwenye uchumba leo usha mtumia ana watoto wa tatu una taka mvunja kiuno tena abebe maji kwenda bafuni ungekuwa una taka haya unge mwambia toka unataka mwoa angejipanga. So siku shauri uoe mwingine maana mpaka hapa inaonyesha hauna kipato cha kutosha utakuwa una jipa presha zaidi ya kudaiwa matumizi nyumba mbili.
Kumaliza tatizo sio mke mpya jibebe maji yako fuo boxer zako kama ulivyo kuwa unafanya wanao fanyiwa waachie wao hayo.
 
UZI ULITAKIWA UISHIE HAPO KWENYE UMEOA (MRANGI)

UJue vijana tunakosea kujua tabia za makabila,
Huwezi kuishi na mke wa kirangi kama unavyoishi na mke mnyamwezi!

Huwezi ishi na mke wa kichaga kama unavyoishi na mke mzaramo!

Kila kabila lina mbinu zake, Tatizo kubwa lipo kwa waoaji wanaume sisi ndo hatutambui!
Kabla hujaoa kama huwezi kucheza na biti za hilo kabila kwanini unaoa?

Walangi ni wababe na ni watamu na ubabe wao , wachaga ni jeuri lakini ujeuli wao unafaida, wazaramo wana mauno wanafaida na mauno yao!

Ukitaka sofa za huku ulete kule utachemka tu!
Oweni wake wa matamanio yenu bhana mnatusumbua kutoa ushauri
Thread closed
Cha kuongezea pia tazama mwenendo wa Mama yake kama yupo hai ujue aliishi vipi na Baba wa mkeo, akina Mama ndio role model wa wanawake walio wengi kwenye ndoa zao wanaiga mifumo ya zao hivyo kama ukiona mama mtu alikuwa mzinguaji kwa baba mkwe wako basi tegemea na mtoto kuiga hizo tabia.
Bundakwetu
Uliingia kichwa kichwa kwa huyo mrangi na ulichukulia poa sana tabia zake ukijipa matumaini atabadilika, hilo ni kosa sana la kiufundi
 
Kama ni Muislamu dini inaruhusu. Wanawake wanaogopa ushindani tu hofu ya kuletewa mwingine
 
Habari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kijitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe mke nikimwambia anifulie wakati mwingine anajibu kabisa kuwa sifui hali hii inanishangaza na kunisikitisha sasa naombeni ushauri nioe mwingine au nifanyeje upendo kwake kiukweli haupo kutokana na anavyonidharau naomba ushauri wenu.
Nawasilisha.
Msingi wa maisha ya ndoa unatakiwa uanze kuuweka pale tu mnapo anza kuishi pamoja ili mwanamke ajue nini unapenda na nini hupendelei; Ukisha poteza hiyo fursa, kuja kuianzisha baada ya miaka kadhaa umechelewa sana kwani unaonekana kama umebadilika
Labda anzia hapa; Acha nguo zako chafu pamoja na za kwake wakati unatoka kwenda kibaruani; Ukirudi ukakuta amechagua za kwake na kuacha za kwako chafu, ujue hapo kuna tatizo na anzia hapo....
 
Acha mbwembwe hapo uliingia chaka moja ya sifa za mabinti kutoka hilo kabila ni Hawa ni mabinti wengine wazuri sana yaani hawa ndio mungu alicopy & paste the real image yake akawapa yaani mademu wameiva poa, rangi ya mtume figure nzuri lakini ni wafupi, shida moja tu, wao ni washamba sana wamelogewa kazi za bar.

Sasa ndugu hilo ni chaguo lako na kama wasemavyo wazee maji ukishayavulia nguo sharti uyaoge, Pambana ila tafuta mzizi wa hicho kuburi kinatokea wapi?
 
Hujaoa, umewaolea wenzako ana waheshimu
Habari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kijitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe mke nikimwambia anifulie wakati mwingine anajibu kabisa kuwa sifui hali hii inanishangaza na kunisikitisha sasa naombeni ushauri nioe mwingine au nifanyeje upendo kwake kiukweli haupo kutokana na anavyonidharau naomba ushauri wenu.
Nawasilisha.
 
Kwani umesikia mke ni drycleaned kuwa akufulie ngue au make no chief kuwa akupikie... Wanaume tubadilike mitazamo na kusoma alama za nyakati... Sio mbaya mwanamke kukufanyia utakacho ila vingine kama unaweza Fanya mwenyewe tena kwa upendo mkubwa
Siku Majukumu yote ya ndani mnawaachia dada wa Kazi kwani tumeoa dada wa Kazi. Kazi yenu kubwa ni kuweka rangi kucha, kuchat na kuangalia tathmilia tu.
 
Hivi KILA mwanaume akiweka changamoto ya ndoa yake humu huyu mbona hana changamoto kihivyo.
 
Back
Top Bottom