Mke wangu ananidharau nifanyeje?

Mke wangu ananidharau nifanyeje?

Hilo tatizo ulitakiwa ukishughulikiwa mapema baada ya kuoana na siyo sasa,huyo samaki kashakauka kwa sasa ukimkunja atavunjika
 
Mke wa mengi, billgate,nk waume zao hawana pesa? Huu ni msemo wa kuwafariji masikini.
Uwe na pesa usiwe na pesa mke akiamua kaamua
Umeona wanawadharau,tofautisha dharau na kuchepuka au kuachana.
Kwanza mke wa bill gate nae ni tajiri usidhani ni masikini.
Kibongobongo ukiwa na hela mke atakuheshimu japo utachapiwa tu utake usitake
 
Kwahiyo kama anakaa keko akaoge mto Msimbazi? AU kama anakaa Kongowe ya Mbagala akaoge mto Mzinga?
Vyovyote iwavyo akaoge mtoni,ziwani,bwawani au baharini.Na kama yupo Bunda atembee hadi Nyamuswa,Manyamanyama,Pida au hata Kyawazaru atafute bwawa ajiogeshe.Mwanaume gani anaanzisha uzi wa kijiliza kwamba hajawekewa maji ya kuoga?
 
Hakuna linalo shindikana,lisilotatulika kwa heri basi litatue kwa shali
 
abari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kijitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe
Msaidiane majukumu, yeye amefanya kazi kubwa kufua nepi za watoto na hata nguo zingine za watoto, naamini humsaidii kupika, kuosha vyombo na kufanya usafi wa nyumba, ukimsaidia shughuli zingine unaimarisha afya yako na yake pia
 
We jamaa iyo miaka yote ulikuwa wali mpk mnapata watoto watatu hukuiona iyo tabia yake? We pambana ivyo ivyo mpk kifo kiwatenganishe
 
Tafuta hela dogo, nguo peleka kwa dobi. Maji peleka mwenyewe, hama chumba. Safiri bila taarifa. Hela ya kula kabidhi watoto au house girl. Atakaa sawa tu. Wala usimfokee
nakazia hapo kwenye safiri bila taarifa "rudi ukiwa umeshiba
 
Nidhani huenda akabadilika kitabia huko mbele ya safar lakini imekuwa tofauti
 
Sijaamini maneno ya mleta Mada........miaka 8 bila kufuriwa Wala kuwekewa maji chooni ..


Tea
 
Habari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kujitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe mke nikimwambia anifulie wakati mwingine anajibu kabisa kuwa sifui hali hii inanishangaza na kunisikitisha sasa naombeni ushauri nioe mwingine au nifanyeje upendo kwake kiukweli haupo kutokana na anavyonidharau naomba ushauri wenu.

Nawasilisha.
Wenyeji wa Dodoma wanakwambia ukikutana na nyoka na mrangi kwa pamoja porini, bac maamuzi sahihi unayotakiwa kufanya ni kuuwa kwanza mrangi then ndo umalizane na nyoka
 
Kwani umesikia mke ni drycleaned kuwa akufulie ngue au make no chief kuwa akupikie... Wanaume tubadilike mitazamo na kusoma alama za nyakati... Sio mbaya mwanamke kukufanyia utakacho ila vingine kama unaweza Fanya mwenyewe tena kwa upendo mkubwa
Kizungu waachie wazungu bro
 
Habari zenu humu kwenye Jukwaa hili pendwa, mimi nimeoa mke ( Mrangi) na tumefanikiwa kupata watoto wa 3 wote wa kike sasa mke huyu mwaka wa 8 huu hajawahi kuniwekea maji bafuni wala kunufulia nguo zangu sasa watoto wangu hatimae wamekuwa na wameanza kujitambua, kinachoniuma ni kuona watoto wakishuhudia mimi kama baba wa familia nikiwa nafua nguo zangu mwenyewe mke nikimwambia anifulie wakati mwingine anajibu kabisa kuwa sifui hali hii inanishangaza na kunisikitisha sasa naombeni ushauri nioe mwingine au nifanyeje upendo kwake kiukweli haupo kutokana na anavyonidharau naomba ushauri wenu.

Nawasilisha.
Hata kama wewe ni Mkristu nakushauri oa mke wa pili na huyo mke wa pili awe ni kabila tofauti na utafute anayekufulia na kukupenda ili mke wa kwanza ayaone makosa yake
 
Kuna yule naye ameoa mrangi, haya mrejesho huo hapoooo
 
Duuh pole sana ila nashangaa kwamba hata mwanzo wa mahusiano yenu hajawahi kuja geto ukampa Nguo afue??? Kama alikuwa anafua why sasa asifueee..??? Bhasi tatizo ni wew sio yeyee.
 
Back
Top Bottom