We unampigia sana magoti ndo mana anajua upo weak hata akifanya chochote anajiamini,Be strong na ujiamini,halafu ushawahi kujua siri zake kuwa hajatulia so hiyo ndo chance ya kumgandamiza.Mi girlfriend wangu alikuwa ananifuatilia sana fb na nikamwambia huwezi ukanilinda kama sintakuwa mwaminifu,maana kama akinizingua fb nitaenda myspace,akijua nitaenda tagged,akigundua Jf,akigundua badoo,so ni kazi bure tu
Jamani waungwana naomba msaada wenu huyu mke wangu mie simuelewi kabisa.
mwanzoni mwa mahusiano yetu alikuwa na tabia sana ya kuchunguza simu yangu na hakuwahi kugundua message yoyote mbaya ingawa hata msg isiyo ya kimapenzi ikiingia kwenye simu yangu so long as inatoka kwa mwanamke basi siku hiyo ni vurugu kupita kiasi akidai huyo mwanamke atakuwa bibi yangu ama mpenzi wangu tu. siku mie niliposhika simu yake siku moja, nikagundua msg nyingi za kimapenzi toka kwa wanaume wawili tofauti, anaomba radhi nikamsamehe.
Baada ya muda alikuwa akinisumbua kwa kudai kuwa mimi nina uhusiano na wanawake chungu tele kuanzia wale ninaofanya nao kazi hadi mtaani. Baada ya kuchunguza nikagundua kumbe yeye ndio ana mahusiano ya kimapenzi na rafiki yangu. mini ni mvumilivu nilimsamehe ingawa ni baada ua kukana sana na mwisho wa siku akakubali. hayo yakaisha mwaka jana.
Sasa hivi amekuja na mpya. Anasema kila mwanamke ambaye ni rafiki yangu facebook kwamba ni bibi yangu na anakomaa kwelikweli. mie nashindwa hata nimwambie nini ili aamini kuwa mawazo yake sio kweli maana kuna wasichana zaidi ya 1000 kwenye orodha ya marafiki zangu fb na wavulana kama 1000 wengine. kila comment yangu kwa mwanamke yoyote inakuwa ugomvi hauna mfano, kisa eti na comment kwa bibi yangu. kwakweli sina amani kabisa na hali hii inanikosesha raha.
Naomba waungwana mnisaidie nifanye nini maana nahisi kama anaanza tena kuficha uovu wake kwa kunipakazia mie, nahisi tu hilo sijafanya uchunguzi tena.
Shantel inawezekana nikakubaliana nawe. Lakini upole wangu sio uzezeta, tatizo langu huwa sipendi kabisa ugomvi wa kurushiana maneno kwahiyo huwa na-opt kukaa kimya na kisha kumwambia baada ya kuwa ametulia. Pili siwezi kabisa kumpiga kwa sababu najijua nina nguvu na naweza kuua yawe matatizo mara mbili. Tatu dini inanisumbua sana maana tumefunga ndoa vinginevyo huwa nasema bora ningekuwa mwislamu, angeshakula talaka long time. lakini naufikiria ushauri niliopewa humu maana ni kweli hata Mandela alikuwa na ndoa, why kwangu ishindikane. nadhani inaweza kuwa suluhisho kwa njia moja.
Usisingizie dini hapo. Kwenye suala la uzinzi talaka inaruhusiwa kwenye biblia tena ni Jesus mwenyewe aliyetoa kibali.