Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbona mnashidwa mtetea mwanamke mwenzenu?[emoji1][emoji1][emoji1]Mkuu wewe ni mpole sana man up tafadhali.
Halafu mbona mkeo ni mkoloni sana? Anataka kuonekana yeye kuwa yuko juu zaidi yako, na dini haisemi hivyo hata msamaha kwenye maandiko hauko hivyo, hapo changanya na za kwako.
Sasa naweza kuwaelewa wanaume kwa nini wakitukosea makosa wanabadilika wanakuwa wakali ni kwa sababu ya wanawake kama mkeo.
Upo sahihi boss we tia mgomo mambo ua kurekodiana tutakuona whatsapp unazagaa ovyo umepiga goti unaomba msamaha kanisa.
Kwa swali kama hili..wewe ni wa kiume tu!Haaaa, haaaa, mbona umepaniki sana tatizo ni nini?
Hahha afu itabidi tu uoe mnyaki; unatukubali sana kimoyomoyoM
Mkewe atakuwa akina Atuganile Mwakifulefule,,,unamkosea dada msamaha unaomba ukoo mzima [emoji23][emoji23][emoji23] pambana na hali yako.
Mkeo atakuwa anacopy kwa Jiwe ambaye misamaha lazima iombwe mbele ya camera. Fanya kama ulivyopanga na si vinginevyo.Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu.
Safi mwanamke gani huyoNenda nae kanisani,
Muombe msamaha na yote anayotaka uyafanye,
Hii itafanya upime ujinga wa mkeo,ujinga wa viongozi wa kanisa,
Halafu ukisha Fanya anayotaka tangaza hapo hapo kuachana nae mbele ya hao hao anaotaka waone unavyomuomba msamaha
Kwani akimuomba mkewe msamaha wakiwa ndani kuna ubaya gani?Inawezekana kafanya makosa makubwa sana alafu humu watu wanampa kichwa[emoji3][emoji3][emoji3] inawezekana mtaa mzima unajua uovu wake,, mke lazima ampeleke mbele ya kadamnasi ili apate amani ya moyo na amwamini tena.. mbona siku ya harusi walienda humohumo kanisani.
Kwani kumwomba msamaha umpendaye mbele ya watu kunashida gani? Ninachojua kutakua kuna shida kama maombi hayamaanishwi.
Safi sana ampige chini na yy mbele ya kanisaNenda nae kanisani,
Muombe msamaha na yote anayotaka uyafanye,
Hii itafanya upime ujinga wa mkeo,ujinga wa viongozi wa kanisa,
Halafu ukisha Fanya anayotaka tangaza hapo hapo kuachana nae mbele ya hao hao anaotaka waone unavyomuomba msamaha
Wakuu nawasalimu,
Niko katika hali hii kwa sasa.
Ni kweli nilimkosea mke wangu. Nilifanya dhambi kama binadamu wengine wafanyavyo dhambi. Nimejutia kosa langu na nikaamua kumuomba msamaha mke wangu ili maisha yaendelee.
Jambo la kushangaza ni kuwa mke wangu huyu wa ujanani amekataa kunisamehe. ametoa mashariti kadhaa ili niweze kupata msamaha wake. Mashariti hayo ni haya.
1. Jumapili hii twende kanisani nikaombe msamaha mbele ya kanisa.
2. Turekodi mkanda wa video ili hata watu wengine ambao hawatakuwepo kanisani waweze kuona tukio hilo hapo badae.
3. Amesema pia nikiwa namuomba msahama mbele ya kanisa nimuite mama na wala siyo mke huku nikiwa nimepiga magoti.
Wakuu, nimefikiri sana swala hili. Nia hasa ya mke wangu ni nini. Hivi ndivyo msamaha unavyoobwa?
Nimejiuliza tena kwani atapungukiwa nini kama atanisamehe tukiwa wawili tu bila kamera?
Nilichopanga ni hiki , nataka kugoma kufanya kitendo hiki. Ninagoma kwa sababu nataka kulinda utu wangu. Kufanya dhambi au kumkosea mke wangu hakuondoi utu wangu hata kidogo.
Siko tayari kuuza utu wangu kwa gharama ya kulinda ndoa. Utu huwekwa na Mungu ndani ya mtu. Kuuza utu wako kwa mtu ni kumfanya mtu huyo kuchukua nafasi ya Mungu katika maisha yako. Siko tayari.
Msamaha una misingi yake. Moja ya misingi hiyo ni kulindiana heshima.Msahama ni upendo .Upendo haudhalilishi wengine.
Kama ndoa ni ndoano , basi ndoano hii haitaninasa.
Ngoja nikanunue spikaEeeee sauti haiko clear dada.
Kama hawezi masharti si aache, inawezekana mke hataki kumsamehe ndio maana kampa conditions asizoweza kufanya[emoji1][emoji1]Kwani akimuomba mkewe msamaha wakiwa ndani kuna ubaya gani?
Msamaha unatolewa kwa masharti hili la wakristo wa wapi??
Kwa hiyo anataka watu wote wajue mumewe ni mkosaji ili iweje??