Mke wangu ananipiga vijembe WhatsApp

Mke wangu ananipiga vijembe WhatsApp

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
613
Reaction score
313
Habari wenzangu.

Jamani ukweli nimebaini mke wangu anamatumizi mabaya ya simu, nilikutana sms yeye anasema ni rafiki yake ila mie sikuipenda kwa hio nikakosana naye akaenda kwao nami nikabaki kwangu sasa ni zaidi ya miezi 4 basi vikao vikawekwa akakubali kurudi ila naona amekua mkali ukisema kitu anakijia juu na maneno maneno ya shombo kibao.

Sasa juzi nilikua nakarabati nyumba yetu wakati yeye yuko kwao basi nikawa napiga plasta na rangi baadhi ya vyombo vikarukiwa na tope na rangi alikuja kuchukua kitu akaona kua imekua hivyo katukana huyo kwa kusema nimemfujia vyombo vyake akatukana sana na kukata simu.

Leo ni siku kama ya 6 hatujawasiliana mimi sijampigia na yeye hajapiga ila huko whatssap huko vijembe kibao yeye ni mzuri mie sijui kukea namjibu jeuri mambo kibao.

Sasa naona kwa kosa hilo tunafikiana huko jee akirudi tukikosana si atanimalizia maneno huyu.
 
Kwani huyu mke wako si mlishaachana mkuu?

Na vipi huyu jini ulishaachana naye?

Sit and talk with her. Try to understand your wife and solve your marriage's challenges before you drop them here. Ikishindikana kwa njia zako utakazoziona za busara, tafuta msaada. Usije tafuta msaada kabla ya kuchukua hatua yoyote ulioiona kwako ni bora.
Atafutaye msaada kabla ya kuushirikisha ubongo wake katika kuamua huyo hubaki kuwa tegemezi katika kila jambo limtokealo.
 
  • Thanks
Reactions: _ly
Kwani huyu mke wako si mlishaachana mkuu?

kwanza ndio mke huyu huyu mwenye mkasa huuu nilienda kwao katika ugonvi huu nikajishusha basi akarudi tukaishi na akaondoka tena mapema mwezi wa saba kwa kosa hilo la kimtandao
 
Sit and talk with her. Try to understand your wife and solve your marriage's challenges before you drop them here. Ikishindikana kwa njia zako utakazoziona za busara, tafuta msaada. Usije tafuta msaada kabla ya kuchukua hatua yoyote ulioiona kwako ni bora.
Atafutaye msaada kabla ya kuushirikisha ubongo wake katika kuamua huyo hubaki kuwa tegemezi katika kila jambo limtokealo.
kaka nishasema ila tatizo anaonekana kua na misimamo ya kutojali
 
mblock watsup kwa muda then kaa kimya..

akichoka kukaa kwao atakutafta

usijichoshe,
kama mamake na babke walishatengana basi huyo nae atakusumbua tu
 
Back
Top Bottom