Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Mke wangu anatazama Cartoon kuliko Watoto wetu

Mchunguze vizuri nayeye sio katuni kweli!? Maana usije ikawa unamzuia mwenzio kuwapenda ndugu zake .
Hapana mkuu, uhuru anao kabisa, familia yake yenyewe walizaliwa wawili tu...
 
Unataka awe anashinda Facebook na insta,tiktok na matakataka kama hayo?
Katuni ni stories and i don't see anything wrong there except you have the Best wife..

Tatizo wewe haupendi katuni basi na wewe unataka wife awe hivyo.
 
😎, kumbe kuna hasara yake, ya watoto kuwafungia ndani ya gethi lenye mbwa mkali 😄

😃😃kulea watoto kwa kuwatunza ndani sio lazima kuwe na geti kubwa na mbwa.
Ni mazingira tu ya mipaka mzazi unawawekea watoto wako na wanakua kwenye makuzi hayo.
 
Hababa Bellerin, toma and jerry zile classic sio hizi za sasa, marsha and the bear, ziggy and sharko plus animation kibao kama pussy in the boots, rango, n.k ni poa sana
Muda fulani zinanitoa ulimwengu huu wa matabaka na kunipeleka hadi ulimwengu wa furaha isiyo kifani nacheka mwenyewe tu.... let's enjoy muda mchache wa ulimwengu huu...😄😄😄😄
 
Mimi hakuna character maarufu wa kwenye cartoon simjui, nazijua na kuzipenda sana.
Na niko mbele kufuatilia, ikitoka tu mpya naruka nayo napeleka home tunaangalia.

Tofauti na mpira na drama za kikorea, napenda sana animation.
Hizo Cinderela, Barbie Mariposa, Little Mermaid n.k ndio kama sala ninavyozijua 😂😂
• 🤔, Duh hatari sana, basi na huyu ngoja niachane naye tu.
Nifah kwani kuna uzuri gani huko kwenye katuni? 😎
 
Angekuwa anapiga umbea huko barabarani ama kuongea na simu mara kwa mara ungeshamnasa vibao

shukuru amepata faraja ya moyo wake, manake unaonekana humpi mkeo muda wa kutoshaa kuongea nae
 
mimi pia nina uraibu wa kutazama katuni kupita vipindi vyote vya TV. Simu imejaa cartoon na sina mpango wa kuacha leo wala kesho.
Kumbe, hawa watengeneza katuni wanapiga hela hivi, Maana nikiangalia idadi ya wanawake wapo wengi sana.
 
• 🤔, Duh hatari sana, basi na huyu ngoja niachane naye tu.
Nifah kwani kuna uzuri gani huko kwenye katuni? 😎
Ni nzuri sana, hasa animation ni kama movie tu.
Ukipata yenye story nzuri hutokaa uache.
 
Kawaida tu hiyo, ngoja nikutajie ninazo zipenda mimi...

-Tom and Jerry (normal).
-Bellerin.
-Pikapau.
-Makarao.(Kenya)
-Ed,Edd and Eddy.
-Masha and the bear.
-Katoto (Ug).
-Shrek.
-The croods.
-The lion king (Hakuna matata).
-Small foot.
-Luka.
-The lorax.
-Hotel translavia.
-Rango.
-Peter rabbit.
-
Aisee, hasa nikitaka niangalie zile movie za vita, Dah hapendi kabisa, anasema najifundisha ujangili 😎.
 
Habari wana JF, poleni na majukumu ya hapa na Pale [emoji1666].
• Kuhusu hili suala, naona kama ni uraibu wa mke wangu kutazama katuni na watoto kila dakika. "[uende - urudi ni katuni kwenda mbele na michezo ya hapa na pale.] "

• Mke wangu huwa anafurahia sana kutazama na kuimba pamoja na watoto wetu pindi wanapongalia katuni hiyo, na endapo watoto wetu kama watakua hawajaangalia hiyo katuni huwa akiwasimulia hadithi hizo baada ya watoto kuludi kutoka shule au kutoka maeneo yao ya kucheza. Kila nikiangalia hili suala la katuni, naona kabisa kuna kitu hakipo sawa kabisa.

• Kuhusu katika majukumu yake kama mke na mama wa watoto wetu, kwa kweli yupo vizuri sana analea watoto safi kabisa, ila kinachonipa wasiwasi mkubwa ni kuhusu hili suala la kuangalia katuni bila kupumzika. Yani wamegeuza nyumba kuwa nyumba ya katuni. [ uende - urudi ni katuni kwenda mbele ] na michezo ya hapa na pale.

• Kama kutakuwa na njia au namna yeyote ile naomba msaada wa kurekebisha hili tatizo la katuni.
"Nahisi kuna kitu kibaya, maana simuelewi kabisa kuhusu mke wangu, wakati mwingine hata haangalii sinema ninazotaka tuangalie pamoja, isipokuwa tu atajilazimisha kishikaji lakini moyo wake unakua unawaza katuni tu. Hata tukiwa tumekaa kama familia yeye na watoto wetu huendelea kupiga stori za katuni.


• "Mke wangu, mwenye umri wa miaka 33 sasa, anafurahia sana kutazama katuni zaidi kuliko hata watoto wetu. Mvulana wetu wa kwanza ana umri wa miaka 11 hadi wa mwisho ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 4.

• Naona kama mke wangu amepatwa na uraibu wa katuni hivi , wao ni kuimba nyimbo za katuni , kupiga ngoma zao na kujadili mambo ya katuni kila wakati.


• Nimejaribu kumweleza kuwa sipendi kabisa tabia ya kuangalia katuni kila sekunde lakini wapi!!! , silalamiki kwa sababu wanafurahi lakini sielewi uraibu wa mke wangu ni nini hasa?. Hata wakati watoto wakiwa hawapo karibu, yeye ataendelea kutizama filamu za katuni peke yake. Watoto Watakapofika nyumbani , atawasimulia yote aliyoyatazama na hata kuwaonyesha kwa vitendo matukio ya kuchekesha/yenye hisia.

• Tafadhali kumbuka kuwa, ameajiriwa kikamilifu na bado anafanya kazi zake kama mke na mama. Sina tatizo lolote kwa upande huo, je amezoea filamu za katuni au kuna kitu kimejificha? Au nimuache akikua ataacha mwenyewe, Maana sielewi kabisa."

• Je, kitu gani ninaweza kufanya ili kumsaidia mke wangu ? Inanisumbua sana akili yangu kwa namna fulani.



[emoji41]Hii ni story ya kijana Mwenye familia ya watoto wa tatu [emoji3578][emoji3578][emoji3578][emoji3578].


View attachment 2856301View attachment 2856302View attachment 2856303
Mkuu Nyafwili fikisha pole zangu kwa huyo kijana ila mwambie azoee haina namna japo mimi nilidate na Jese alipenda sana katuni na mwisho akawa ananiletea ukatuni nikambwaga chini

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tubadiliahane mimi ni mme napenda sana animation huyu mpenzi wangu yeye ni mpenzi wa tamthilia za kifilipino na uturuki huyo dada nipe mimi kisha we njoo umchukue huyu kivuruge wangu yanii hapo kuanzia asubuhi hadi jioni ni mwendo wa animations tu mpaka watoto tutawabadili majina tuwape majina ya cartoons
kisha we njoo umchukue huyu kivuruge wangu

• 😄 Kwenye kivuruge hapo ndo atanivuluga kabisa, Ebu tuma picha yake nimuone kwanza 😎,

• Kwa hiyo na wewe mkuu, unapenda cartoon?
 
Back
Top Bottom